Nampenda lakini hanijali

Gorgeousmimi

JF-Expert Member
Jun 21, 2010
9,296
7,666
Niko kwenye mahusiano ya Takriban miaka minne na mwanaume ambae nimezaa nae mtoto mmoja.Tulikutana ktk chat tukapendana..baada ya kuonana Nikabeba ujauzito wake which is irresponsible i know coz tunaishi sehemu Tofauti.
Hanisaidii kwa huduma yoyote coz hana kazi thats fine Ila hata nikiwa nae hanisaidii hata ktk malezi ya mtoto(tupo nje ya nchi),anasema anataka kunioa na ananipenda lkn tatizo hanijali wala hajali feelings zangu akinikera,haoneshi mapenzi na mimi na Sifeel kama ananipenda coz hata nikiumwa hanijulii hali nampigia Simu mimi ananikemea Eti namuamsha usingizini na kuumwa naumwa mimi!!yaani kuna vituko vingi sana amenitendea huyu mwanaume siwezi kuvieleza vyote!!
sasa nimeamua kuachana nae Ila bado nampenda sana na namuwaza saa zote!!mnadhani nimechukua uamuzi mzuri kuachana nae au nifuate moyo wangu niendelee kuwa nae na niendelee kuumia?
 
Dada, huyo ni mpenzi wako na umesema uko nae kwa miaka 4.. Dah, kwa ninavyoelewa mimi miaka 4 ni mingi sana kwa wapenzi kuwa mmeshafahamiana vya kutosha..Ina maana huwa hampati muda wa kukaa pamaoja na kuongea kuhusu mahusiano yenu? Kwa nini usimweleze nini kinakukwaza kuhusu yeye? Nakushauri umweleze kinaga ubaga maana inawezekana na yeye hajui kwamba anakukwaza.
 
Eeh!
Sasa unataka tukushaurije na wewe kakuonyesha maisha hadharani? Hamna cha uhaba wa wanaume wala nini! Ukiamua kujitwika msalaba huo ujue golgota ni mbali na kuutua unahitaji winch! Akikuoa ndo atatafuta kazi ama ataanza kukujali? Ngoja niende desktop mode nibonyeze report abyuzi!
 
Pole sana,je ushawahi kukaa na kuongea naye unayotueleza kuhusu yeye? Au ndo unampenda hadi unamwogopa?...lol..,ongea nayeatabadirika.
 
Haaaaaaaaaahh! pole sana lakini mwenzangu ivi inakuwaje una jitoa muhanga kwa mwanamme kiasi hicho,yani condom zilizo jaa tele matangazo mpaka kwenye vituo vya basi bado tuu una mpaa hivi hivi? na miaka yote minne anakusugua roho bado tuu kwani hujiamini kua wewe na mwanamke na ungeweza kupata bora zaidi,
Sikia shosti kama umeweza kulea huyo mtoto peke yako mpaka sasa nadhani utakua ushazoea,achana na mshenzi watabia huyo na usonge mbele,na nilazima useme na moyo wako kua huyu sie mwanamme, mwanamme niyule anae jali majukumu yake asiwe hodari kukuchanua miguu tuu,na ivi unaweza kunambia kubwa unalompendea ni kitu gani? michezo yake,sura yake,mwanya akicheka au anavyo kubinjua anakufikisha na unakubali kua mtumwa wa penzi lake? au unasubiri mpaka akawambia sikutaki au umkute na mwanamke mwengine kitandani ndio utajua sasa kweli alafu unywe sumu?
shosti hujachelewa bado time unayo na niamini utampata mbora kuliko yeye achana na hicho kituko HARAKA SANAAA.
samahani kama itakua nimesema nikapitiliza....
 
ushauri wangu kwako ni huu miaka 4 imetosha kukufanya umjue na ukweli ni umri wa mtu kufikia hatua ya kuamua kwa dhati. he is wasting your time piga chini mshukuru kwa kupata mtt carry on with your life atakuja mwingine tu. but kama uko nje na si mswahili uwe makini sana asije akakuua wewe na mwanao manake naskiga ndo revenge zao
 
Nimeshaongea nae sana lakini habadiliki nimeshaongea na watu wake wakaribu Pia wakaongea nae lkn bado hali ni ileile.Najua miaka minne ni mingi na tunafahamiana vizuri usemavyo ni kweli Ila nafeel we r nt meant to be together ndio maana hatuendani na ndio maana hajali!na ana ile tabia ya kununa,nikimkera mimi atanuna nimbembelezee weeee lakini akinikera mimi Pia atanuna yeye na niombe msamaha mm wala hajali yaani kama nimekerekwa mimi!!
 
Nimeshaongea nae sana lakini habadiliki nimeshaongea na watu wake wakaribu Pia wakaongea nae lkn bado hali ni ileile.Najua miaka minne ni mingi na tunafahamiana vizuri usemavyo ni kweli Ila nafeel we r nt meant to be together ndio maana hatuendani na ndio maana hajali!na ana ile tabia ya kununa,nikimkera mimi atanuna nimbembelezee weeee lakini akinikera mimi Pia atanuna yeye na niombe msamaha mm wala hajali yaani kama nimekerekwa mimi!!

Sasa usaidiwe nini tena.....kusoma hujui hata picha huoni
 
Nimeshaongea nae sana lakini habadiliki nimeshaongea na watu wake wakaribu Pia wakaongea nae lkn bado hali ni ileile.Najua miaka minne ni mingi na tunafahamiana vizuri usemavyo ni kweli Ila nafeel we r nt meant to be together ndio maana hatuendani na ndio maana hajali!na ana ile tabia ya kununa,nikimkera mimi atanuna nimbembelezee weeee lakini akinikera mimi Pia atanuna yeye na niombe msamaha mm wala hajali yaani kama nimekerekwa mimi!!
Pole sana...Kama umeshahangaika nae namna hiyo..Achana nae, usije ukafa kwa presha wakati mwenzio anakula bata..Move on with with your life.. Mungu atakupatia mwanaume anayekufaa.
 
Pole sana dada,
Mi nakushauri umaintain an open mind about him. Kama umempa vitu anavyostahili kwenye uhusiano na si kumbebesha mizigo tu na yeye akaona thamani yako basi he will remember and come back and if not then why would you want him?
We all make mistakes na hata kama mwanaume anataka kukuoa when he feels pressured by the kid, family and his life mind yake hubadilika kisaikolojia na akaanza kuitazama hiyo ndoa tarajiwa as a marriage of convenience rather than marriage of love.
Anaweza kuwa anakupenda more than any other woman na anataka kweli kukuoa but upande wa pili anahisi ana moral obligation ya kukuoa because of the kid. Now akiwa under much pressure mind yake huhamia upande wa pili na akaanza kutafuta namna ya kutoka kwenye hayo mahusiano.

Honestly, Its not fair for you to bring up the child alone but jitahidi kupunguza pressure then anaweza akaona ule upande wako uliomfanya akupende na akarudi tena (aka Try to love him over again).

Remember when some things break we mend them and not throw them away
 
ushauri wangu kwako ni huu miaka 4 imetosha kukufanya umjue na ukweli ni umri wa mtu kufikia hatua ya kuamua kwa dhati. he is wasting your time piga chini mshukuru kwa kupata mtt carry on with your life atakuja mwingine tu. but kama uko nje na si mswahili uwe makini sana asije akakuua wewe na mwanao manake naskiga ndo revenge zao​


wewe unamuongopea mwenzio ampige chini! mwenzio kasema kamuacha ila bado anampenda so hawajaachana, utaonekana mmbeya - mpe confidence mwenzako aendelee kumpenda mwenzake coz bado anampenda, pia, I thought ungemshauri azidi kumvumilia coz she had him for over 4 years, kwa nini amshindwe sasa? Mwambia nadhani huyo shemeji yetu hana kazi, so ukiwa too demanding kwa vitu vikubwa ambavyo ni zaidi ya uwezo wake ataona kama unamcheka/unamsanifu - hasa hayo mambo ya matibau kwake una maanisha bill na anatakiwa kulipa, awe anamwambia kuwa anaumwa ila "I have gone for medical check up and dr. kasema nitapona kama nitamaliza dose", keep praying for him apate kazi, and mind you sijasikia anasema huyo shemeji anam-cheat...mshauri avumilie please ni mambo ya uchumi tu hayo


 

Similar Discussions

Back
Top Bottom