Namnywea rafiki yangu

Wa Nyumbani

JF-Expert Member
Mar 31, 2011
438
65
Jamaa mmoja kila akienda baa alikuwa anaagiza bia mbili na glasi mbili. Anamimina bia kwenye glasi zote na kunywa moja halafu nyingine hadi zinaisha. Anaagiza zingine mbili na kuzinywa kwa mfumo huo huo mpaka anapomaliza na kuondoka. Wahudumu wa baa wakawa wanajiuliza maswali kwanini jamaa anafanya hivyo. Siku moja mwenye baa akaamua kumuuliza. Jamaa akasema,
"Unajua, nilikuwa na rafiki yangu mpenzi, tulikuwa tunakunywa bia pamoja kwa miaka mingi. Rafiki yangu huyo ameshafariki. Kwa kumkumbuka, kila ninapoagiza bia moja namwagizia na yeye. Nakunywa yangu namnywea na yeye" Mwenye baa akashangaa sana.
Baada ya swiki moja, jamaa akawa anaagiza bia moja na glasi moja tu. Mwenye baa akamuuliza kulikoni mbona amebadili utaratibu? Jamaa akamjibu,
"Aaa unajua, mimi nimeamua kuacha kunywa pombe. Hivyo sasa naagiza bia moja tu kwa ajili ya kunywea rafiki yangu"
 
Back
Top Bottom