Namna ya kupata cheti na transcript udsm bila kupoteza muda!

Saskatchewan

Senior Member
Oct 16, 2011
148
21
Kwa kawaida ukienda udsm kuchukua transcript unatakiwa usubirie siku kumi na nne(14) za kazi ili uweze kuipata. Hata kama una ishu ya maana na inayohitaji transcript kwa haraka itakwama! Pamoja wanasema rushwa ni adui wa haki lakini wakati mwingine inabidi utoe kitu upate kitu! Ukitoa kitu ndani ya saa 1 unapata kila kitu! Na sidhani kama rushwa itakuja kuisha!
 
Nenda ofc no. 104 ukatoe elfu 10000 takipata mapema......lol.....
 
Nenda ofc no. 104 ukatoe elfu 10000 takipata mapema......lol.....

umeona eeh! Lakini wanatusaidia sisi wenye haraka na ambao sio wakazi wa Dar es salaam kuokoa muda na kupunguza gharama! Big up mia na nne(104)
 
Mimi nimemaliza mwaka 2005 AVU-Learnig Centre Course ya Comp. Science mpaka sasa cheti changu nazungushwa tu,mara njoo kesho mara leo muhusika hayupo rudi baada ya wiki, mpaka sasa nimechoka. Kwa kuwa niliamua kuanza kozi kama hiyo chuo kingine na sasa nimehitimu na nafanya kazi zangu, nilichoamua nashaurina na mwanasheria wangu kufungua mashtaka dhidi ya wahusika.

Na wahusika wenyewe kama watasoma thread hii wajiandae, ingawa wanajifahamu kwa kifupi cha majina yao tu ni haya: Ng na wenzako M.M, JM.
 
Hahaha pale udsm upande wa vyeti ni kero mbaya!! watu wenyewe wanatakiwa kwenye management lakini wameng'ang'ania kazi za vijana!! watu wakijaa wanaanza kuhemea juu juu!!
 
Cheza muziki wao kaka. Ile sehemu noma japo kuna mtu kanambia eti pamerekebishwa. Mi namlaumu au nampongeza mama mmoja sijui chumba 105 kama sijakosea. Ukiwa na pesa utachukua cheti kwa kuvunja taratibu yaani before 2weeks. Kama huna basi subiri muda halali.
 
Mimi nitaenda straight 104 na 10,000/= yangu, nisaidieni nimuone nani anisaidie fasta?
 
Udsm room 107 ndio mpango mzima wa kutoa transcript au cheti, room 105 inquiries na hapo ndio kuna vituko na usumbufu hasa huyo mama mweupe mfupi..lol.
 
10000 ndo nini? Sidhani kama atakukubali. Shika walau 20000 mkono mtupu haulambwi. Yule mama anamake I see maana wanaotaka short cut wengi sana kama si wote.
Mimi nitaenda straight 104 na 10,000/= yangu, nisaidieni nimuone nani anisaidie fasta?
 
Hiyo 105 unapoenda kulipia transcript au kuclear madeni ili ugongewe muhuri wa bursar wana nyodo ile mbaya. Utafikiri ndio wao peke yao wana uwezo wa kufanya hiyo kazi Tanzania nzima. Wanahudumia watu kama wanalazimishwa wakati bila ya watu wanaoenda kupata huduma kwao wao wasingekuwa na kazi! Kutokana na nyodo inafanya watu walipe hela zaidi ya wanazodaiwa na chuo. Na udsm ukizidisha hela mpaka uje urudishiwe ni bora usamehe!
 
udsm maana yake ndio nini kirefu chake au ndio
kirefu chake usafili dar es salaam........
 
no wonder nchi masikini, yaani mtu amesota kusoma, bado anazungushwa kupatiwa cheti chake. Wala rushwa udsm someni hapa mubadilike.
 
...kusema ukweli ile ofisi ya kutoa vyeti imeoza na inatoa harufu mbaya kabisa RUSHWAAA laiv. Kama PCCCB wanataka kukamata wala rushwa HADHARANI ...I MEAN hadharani, mchana kweupe basi watinge zile ofisi No. 104 na 108 wakajionee wenyewe. Manake nahisi hata kama huku-GRADUATE pale but ukatoa chochote wanaweza wakaendelea kuprocess cheti ambacho HAKIPO ilimradi tu wachukuwe huo 'MWEKUNDU wa MSIMBAZI' wako. Ukitaka cheti haki ya nane bila kutoa chochote utasoteshwa tu hata kama cheti kipo meza hiyohiyo waliyokaa. Hupati cheti.

Sina uhakika kama VC au DVC wanalitambua hili.
 
Halafu kila siku lazima wapate wateja. Jamaa wanakusanya hela kama hawana akili vile! Haina haja ya kusubiri mshahara!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom