Namna ya kumkamata mwanaume!!

sio kweli,ukimuaga mumeo/mkeo uendapo mahali ni heshima na sio uoga
Niko na wewe si unajau uoga kama haupo pia heshima hamna...na kama heshima hakuna uoga haupo pia.

Hatuongelei uwoga wakumtishia mtu au unaogopa kitu sababu kinaweza kukudhuru.

Uoga tunao ongelea ni ule wa mwanamke kuiogopea ndoa yake isitokee kasoro yoyote, nadhani sasa umefahamu :A S shade:
 
@Mama Ashrat Mmh safi sana na ni ukweli mtupu.

Jamani mdada yeyote anayeweza kuwa na sifa hizo tuwasiliane tafadhali . . . . ? Au ndo wote wameshaolewa?
 
Si unajua mtu aliye ona mwezi anaweza kusema unamulika kuliko jua.

Kukosa kujua, ni swa sawa na usiku wa giza.

Hao wanawake wote mara nyingi sana wanaonewa kwa kutaka wao...wawe ma bibi zetu, mama zetu, dada zetu hakuna sheria inayo sema mwanaume amtukane mke wake.

Una maana kwamba wanaomba kichapo kutoka kwa waume zao?

Wewe huna ndugu hata mmoja ambaye aliwahi kunyanyaswa katika ndoa?

Babu DC!!
 
kumbe ndo mana mimi nimeweza kumkamata wangu.....asante kwa kukumbusha mambo muhimu kama haya
 
dah siamini nimemkosa mke kama wewe mama ashrat,sijui ntaoa lini..
 
King'asti,

Nakubalina na wewe ila timing ya kuongea hayo mambo ni muhimu sana. Kuna mambo ya kuongea mwanzoni mwa mahusiano especially yale ambayo yanahusu maisha yenu binafsi. Ila mambo ya familia zenu ni vizuri yakaja baadaye sana kama mnaona kuwa mahusiano yenu yana dire na mwelekeo. Na bado, kuna mambo ya familia ambayo si lazima mwenzi wako ajue..!!

Katika hili, watu wanatakiwa kuwa makini ili asijeuza silaha za maangamizi!!

Babu DC!!

...Babu DC mie naomba kuuliza hapo kwenye bold...ni wakati gani muafaka wa kuongea mambo yanayohusu familia zenu? hasa kama kuna dosari/tuhuma dhidi ya wale waliomo ndani ya familia?

naomba nimsaidie mkuu DC kujibu, ....mfano kuna "ugonjwa wa wazimu kwenye familia"...
mwache akishaingia kwenye uhondo wa ngoma, aicheze.
 
Una maana kwamba wanaomba kichapo kutoka kwa waume zao?

Wewe huna ndugu hata mmoja ambaye aliwahi kunyanyaswa katika ndoa?

Babu DC!!
Tatizo hatuelewani, hakuna mwanamke anaye omba kichapo kutoka kwa mme wake, na hakuna sheria inayo sema wakubali kupigwa sasa vipi wanyamaze? Hawana mdomo wa kulalamika kwa nini wana nyanyaswa.

FYI, Mwenyezi mungu anasema hapendi wajinga....Sheria za mungu ziko wazi, mwanamke anaye nyanyaswa asikae kwa mme wake sababu mme wake hathamini kuwepo kwake.

Kumshakia mke wako anafanya kitu kibaya ni kosa, vipi ukampige makofi na kumnyanyasa....

Hayo yanayo zabuliwa vibao na kupigwa ni majinga lolo tu, hata kama angekuwa bibi yangu :A S shade:
 
...Babu DC mie naomba kuuliza hapo kwenye bold...ni wakati gani muafaka wa kuongea mambo yanayohusu familia zenu? hasa kama kuna dosari/tuhuma dhidi ya wale waliomo ndani ya familia?

BAK

Mahusiano hayana kanuni yoyote ambayo watu wote au walio wengi hutakiwa kuifuata. Ila kuna mambo ambayo watu wengi wanajikuta wakiyafanya bila hata kufundishwa. Kama ambavyo huwezi kumweleza mgeni mambo mengi yasiyomhusu, ndivyo ambavyo hutajisikia amani kumweleza mpenzi wako mpya details za familia yako. Kwa hiyo binafsi ningeshauri mtu aanze kuongea mambo ya familia yake endapo anaona kuwa huyo mwenzi wake anaelekea kuwa kwenye mahusiano ya muda mrefu. Watu watumie muda mwingi kujiongelea na kufahamiana kabla hawajaanza kuunganisha ndugu, jamaa na koo katika relationship zao. Kama kila GF/BF utamueleza habari za familia yenu (especially zile ambazo si nzuri), utawambia wangapi?

Babu DC!!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
naomba nimsaidie mkuu DC kujibu, ....mfano kuna "mna ugonjwa wa wazimu kwenye familia"...

..Hapo nakubaliana nawe kabisa Mkuu Mbu. Nikitumia ule mfano wa King'asti kwamba labda mzazi mmoja au ndugu wa karibu sana ameshatuhumiwa uchawi . Mapenzi yenu yamepamba moto kiasi ambacho wote mnaona umuhimu wa kuwa pamoja kimaisha mpaka kifo kiwatenganishe...je hili halina umuhimu wa kumwambia mwenzio badala ya yeye kuja kulisikia pembeni ambapo linaweza kabisa kuondoa imani yake kwako?
 
BAK

Mahusiano hayana kanuni yoyote ambayo watu wote au walio wengi hutakiwa kuifuata. Ila kuna mambo ambayo watu wengi wanajikuta wakiyafanya bila hata kufundishwa. Kama ambavyo huwezi kumweleza mgeni mambo mengi yasiyomhusu, ndivyo ambavyo hutajisikia amani kumweleza mpenzi wako mpya details za familia yako. Kwa hiyo binafsi ningeshauri mtu aanze kuongea mambo ya familia yake endapo anaona kuwa huyo mwenzi wake anaelekea kuwa kwenye mahusiano ya muda mrefu. Watu watumie muda mwingi kujiongelea na kufahamiana kabla hawajaanza kuunganisha ndugu, jamaa na koo katika relationship zao. Kama kila GF/BF utamueleza habari za familia yenu (especially zile ambazo si nzuri), utawambia wangapi?

Babu DC!!

...Siyo kila GF Babu DC!!! bali yule ambaye unaona kabisa kwamba kuna kila dalili ya wote kufikia maamuzi ya kufunga pingu za maisha.
 
...'bahati mbaya' na kwa makusudi kabisa, tunapokuwa tu wahitaji hasa kwenye mapenzi...tunajitahidi kwa kila liwezekanalo kutojionyesha tuna dosari yeyote....
 
...Naam mara nyingi huwa hivyo. Watu hawafikirii kile ambacho wamejaribu kukuficha huweza kumfikia mwenzio kupitia source tofauti na hapo kupunguza imani ambayo alianza kuijenga kwako na hili linaweza kuharibu na hatimaye kuuvunja kabisa uhusiano mzuri wa kimapenzi uliokuwepo.
 
....inategemeana na utavyojibu baada ya ukweli kubainika. Dont Panic...!
Sote tuna maskendeli na maskeletoni kabatini...mfano, unapohojiwa kwamba unatabia
mbaya ya uzinzi, upigaji, nk...jielezee vizuri tu Umejifunza na umebadilika ili kumjengea imani mpya
mpenzi wako...

Lakini ukijidai kupandisha hasira, Ooohh, "nani kakwambia....sio kweli!"...hapo unatengeneza mazingira
ya mwenza wako mpya ku doubt ukweli wako..Likewise, mapungufu mengineyo ya familia yenu, mfano
mawifi washari,....au 'wanga!'
 
...to be on the safe side ili usiwekwe kiti moto na kuanza kujihami ni bora tu pale ambapo mapenzi yameshamiri kuanika kila kitu unachoona mwenzako anastahili kukijua kwa wakati huo.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Back
Top Bottom