Namna ya kumjua mwenza mtulivu au mcharuko

Tutor B

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
9,025
6,554
Wapendwa nimeona kwa leo niwashirikishe katika hili.
Wengi wenu mnapoanzisha mahusiano na wapenzi wapya mnajenga mazingira ya kuficha ili jamii isijue mahusiano yenu. Hilo ni kosa kubwa katika mahusiano, ona mfano huu!

Wakati nimemaliza chuo, nilienda kuishi na kaka yangu ambaye alikuwa ameoa. Marafiki wa shemeji yangu walipokuwa wakija kumtembelea nilikuwa na tabia ya kutoongea nao, wakawa wanamwambia shem kwamba najisikia. Na sikuwa na mchumba wala girl friend. Katika kusambaza habari za kujisikia kwangu, siku moja nikiwa beach, na kiredio cha mkononi nikisikiliza nyimbo za 2Park (enzi hizo), alijitokeza mdada mmoja na kunisalimia, ukweli moyo wangu ulimpenda ghafla. Niliondoka naye hadi hotel moja nzuri ambapo vijana wengi walikuwa wanapenda kustarehe pale.
Niliongea naye mda mrefu; akanikubalia ombi langu na nilipogusia suala la ku-Do alikubali haraka. Nilijenga mazingira ya kuahirisha hadi W-end ijayo, naye alikubali. Ndani ya wiki hiyo nilijitahidi kila siku niwe naonekana naye wakati wa lunch na mida ya jioni baada ya kutoka dukani kwa kaka. Tuliendelea kwa takribani wiki 3 pasipo kushiriki kimwili, michezo yetu ilikuwa kupapasana tu, na mimi kwa kuwa nilikuwa bado maji ya moto (kijana) nilipopapaswa tu nilimaliza mumo kwa mumo.
Siku moja alinijia mdada mmoja mwenyeji wa pale pale mjini (mganda) na kuwa mjasili wa kunieleza yale alokuwa ameyapanga. Alinisalimia na baada ya hapo alinambia hivi
Mganda: "Kaka nakupenda ndo maana nimekuja tuongee mawili matatu, si kwamba nakupenda kwa ajili ya mahusiano ya kimwili"
Tutor: Una maana gani na nia ipi?
Mganda: Nina maana nzuri na nia nzuri pia, naomba nikuulize swali;
Tutor: Uliza tu;
Mganda: Hivi xxxxxx ni nani yako?
Tutor: Ni mpenzi wangu
Mganda: Naamini meishatembea wote!
Tutor: Si rahisi ki- hivyo;
Mganda: Kama kweli - basi, xxxxx ni mwathirika, Mume wake alishakufa, mtoto wake alishakufa, na wewe atakuua!

Nisiwachoche na story, kikubwa ni kwamba kama ningefanya mambo ya kuficha, na nilivyokuwa nimemzimikia, hakika nisingekuwa hai! Ukiwa na mpenzi mpya ukakaa naye wazi - lazima utaambiwa kama umepata au umepatikana.

Wengine mnatumia mbinu gani kuwajua walotulia na micharuko?
 
Haya mambo hayanaga formula for sure,sometimes ni kama bingo tuyaache tu kama yalivyo!
 
Kwahiyo wewe hukuwa na mtu ila ukabeba mtu uliekutana nae beach
upo juu sana
OTIS
 
what if hao wadada wanajuana na wana ugomvi wao tu
so kaamua kumharibia mwenzie?
what if hakuwa mwathirika ni uwongo na fitina?
 
Mmh sawa japo katika selection yako nawewe ulibugi, utachukuaje mtu beach na kukurupuka nae bila hata kupima.
 
Kuna vi2 viwili nimevipata from this, "kuwa wazi" na "kuwa mkweli". Wazungu wanasema the truth will set u free.
 
kwa enzi hizo,inawezekana,ila siku hizi,kupima kwanza,mambo mengine baadae.juu ya yote,soksi muhimu
 
Mmh sawa japo katika selection yako nawewe ulibugi, utachukuaje mtu beach na kukurupuka nae bila hata kupima.

kijana alijitosa kama mwanajeshi,si unajua hata Bble inasema taifa langu linaangamia kwa kukosa maarifa?
 
what if hao wadada wanajuana na wana ugomvi wao tu
so kaamua kumharibia mwenzie?
what if hakuwa mwathirika ni uwongo na fitina?

Lkn si inakuwa imemkumbusha umuhimu wa kupima, kabla ya kungonoka? Angeweza tu kusema; nimemuona katulia so tuendelee tu!
 
kwa enzi hizo,inawezekana,ila siku hizi,kupima kwanza,mambo mengine baadae.juu ya yote,soksi muhimu

kujihakikishia usalama wenu, pimeni kabla ya kila tendo la kungonoka....but kwa vile this is not feasible, tukubali matokeo kwamba there is always a chance kwamba mtu anaweza kuvaa mkenge...
 
Mi nadhani tuhamasishane tu, tuanzapo mahusiano tujitahidi kulipia Tbc kipindi cha chereko tunatangaza full-stop.
 
Back
Top Bottom