Namna ya kukabiliana na polisi

Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
13,266
4,716
GT, naombeni msaada na tueleweshe jamii ni namna gani utajilinda ama uta-behave unapakabiliana na polisi. Nimeleta uzi huu kutokana na orodha ndefu ya raia wliouawa na polisi bila hatia yoyote na jeshia polisi na serikali haielekei kutafuta namna ya kumaliza tatizo hili. Tazama orodha ya wahanga(japo sikumbuki majina)

wafnayabiashara ya madini wa mahenge waliuliwa katika msitu wa pande.

Daudi mwangosi.

Kijana -tav driver wa kurasini aliyeitwa katika kituo cha polisi cha chang'ombe na kufariki hapohapo kituoni baada ya dakika chache aihojiwa.

Kasulu

vijana wawili waliokuwa wakinunua mafuta katika kituo cha mafuta kule arusha kisha polisi kuja na kuwamiminia risasi.

Na wengine wengi.

Kutokana na hali hii, huwezi kujua who is next?!, hivyo basi tufundishane ni namna gani utaepuka kuuwa na polisi mara akidhamiria kufanya hivyo.

Nawasilisha.
 
njia pekee ni kutokua kwenye sehemu ya tukio in the first place, mkiambiwa msiandamane au msifanye mikutano basi mnaacha coz hapa sio ulaya..ulaya unabishana na polisi lakini hakugusi kwa sababu haki za binadamu zinafuatiliwa..hapa bongo ni kama vile uko syria, afghanistan,china,russia....hakuna haki za binadamu hapa
 
asante kwa mchango, lakini ukichunguza vizuri raia wengi zaidi wameuawa na polisi nje ya maandamano, tazama msitu wa pande, watu wanaouliwa huku wakihojiwa kwenye vituo vya polisi na wale vijana wa arusha waliopigwa risasi wakiwa kwenye kituo cha mafuta na wengine wengi.
 
Njia nzuri sana ni kuwaelimisha polisi wasifuate matakwa ya vyama bali wafuate sheria na asifuata sheria sheria imhukumu sawa-sawa na mhalifu mwingine na wasimlinde-linde kama walivyokuwa wanamficha-ficha yule muuaji wa Mwangosi.
 
Njia rahisi zaidi ni kuweka msisitizo wa haki ya kukusanyika na kupeana habari kwenye mchakato wa katiba mpya na kuacha kabisa tabia ya kuchagua viongozi kwa rushwa kwani ndio hao ving'ang'anizi madarakani hadi warudishe faida.Mungu ibariki Tanzania na Watanzania.
 
GT, naombeni msaada na tueleweshe jamii ni namna gani utajilinda ama uta-behave unapakabiliana na polisi. Nimeleta uzi huu kutokana na orodha ndefu ya raia wliouawa na polisi bila hatia yoyote na jeshia polisi na serikali haielekei kutafuta namna ya kumaliza tatizo hili. Tazama orodha ya wahanga(japo sikumbuki majina)

wafnayabiashara ya madini wa mahenge waliuliwa katika msitu wa pande.

Daudi mwangosi.

Kijana -tav driver wa kurasini aliyeitwa katika kituo cha polisi cha chang'ombe na kufariki hapohapo kituoni baada ya dakika chache aihojiwa.

Kasulu

vijana wawili waliokuwa wakinunua mafuta katika kituo cha mafuta kule arusha kisha polisi kuja na kuwamiminia risasi.

Na wengine wengi.

Kutokana na hali hii, huwezi kujua who is next?!, hivyo basi tufundishane ni namna gani utaepuka kuuwa na polisi mara akidhamiria kufanya hivyo.

Nawasilisha.

Zenj polisi hanakibri hata siku moja! hata akija kukamata mtu anaomuomba kwanza. Vinginevyo labuda hasiwe anakaa mtaani na hasitembee peke yake! hapa bongo tunawalea wakati wengine tunawapangisha nyumba zetu mtaani!
 
Njia pekee ya kutuawa na askari ni kutunza siri,kama una hela nyingi usiwaambie hata marafiki zako maana hao ndio wanaenda kuchoma kwa maaskari,wale wafanyabiashara wa mahenge walivyokua sinza bar kuna mtu(informer wao) aliwatonya kina zombe kwamba kuna watu wana mipunga ya kutosha wapo bar wanakula ndio kina zombe wakasuka mpango kuja kuwasingizia majambazi ili wavute mpunga.
 
Njia pekee ya uhakika ni kuhakikisha tunaitoa CCM madarakani haraka iwezekanavyo.
Hapo tutakuwa tumetatua tatizo kwa ujumla wake.
 
Njia nzuri sana ni kuwaelimisha polisi wasifuate matakwa ya vyama bali wafuate sheria na asifuata sheria sheria imhukumu sawa-sawa na mhalifu mwingine na wasimlinde-linde kama walivyokuwa wanamficha-ficha yule muuaji wa Mwangosi.

No!The best way is to fight them physically! Like John Rambo(Sylivester Stallone) did in the movie 'First Blood I'. He gave a real 'war they wouldn't believe' and at the end cops in there were flatten to pieces. "They drew First blood not me." he said. Ha! ha! haa!. Siku wakiingia ktk anga zangu,nawafanyia kitu mbaya kwa staili ya Rambo. Ole wao!
 
Wachache waliokufa naamini ni bahati mbaya. Kwa tulio baki dawa ni kufuata sheria za nchi.

Near by Mbozi Mbeya.
 
Zenj polisi hanakibri hata siku moja! hata akija kukamata mtu anaomuomba kwanza. Vinginevyo labuda hasiwe anakaa mtaani na hasitembee peke yake! hapa bongo tunawalea wakati wengine tunawapangisha nyumba zetu mtaani!
Duh!! Yaani jamaa wanadedishwa?? Ile falsafa ya jino kwa jino!!
 
Wachache waliokufa naamini ni bahati mbaya. Kwa tulio baki dawa ni kufuata sheria za nchi.

Near by Mbozi Mbeya.

there are moments i may beg to differ, do you mean majority of the victims were law breakers?!; no, no, not at all.
 
Wachache waliokufa naamini ni bahati mbaya. Kwa tulio baki dawa ni kufuata sheria za nchi.

Near by Mbozi Mbeya.

sheria za nchi kwamba humtakiwi kwenda sheli kununua mafuta mkiwa wawili?? Au tuache kufanya biashara za madini na kujipvmzisha bar?
 
Tatizo la Polisi wa kizazi hiki ni kubwa kuliko tunavyoweza kufikiri. Wengi wanaoajiriwa ni waliofeli masomo, wamejikinai na wakiwa ndani ya kitengo hicho nyeti wanataka kuionyesha jamii kila mmoja kwa wanamfahamu kuwa kushindwa masomo si kushindwa maisha. Hili litafanyika kwa njia halali na njia zisizohalali, na matokeo yake ndiyo hayo. Kumbuka mtu mjinga sku zote atajitahidi kuficha ujinga wake kwa gharama yoyote dhidi ya wanaomjua na wasiomjua.

Kwahiyo, tatizo hilo litarekebika pindi kigezo cha elimu kitakapo zingatiwa katka ajira ya Polisi wetu. Aajiriwe mtu na shule yake ambaye kita atakalofanya atumie akili yake ( reason out why he/she is doing?). Na walipwe vizuri kwa kazi yao ya kulinda situ wananchi na mali zao bali Amani na ultulivu unaohitajika.

Kwa upande wetu, kila unapokuwa kwenye tukio linalokukutanisha na Polisi unapaswa kufahamu unakabiliana na adui (mtu) wa aina gani. Mjinga anataka usijue hilo, anayelipwa kidogo kutokana na elimu yake ndogo, mtu aliyechoka hivyo anakuona wewe ni kitu kimojawapo kinachomsumbua; mwenye tamaa ya maisha mazuri kama ya msomi fisadi, n.k. Ukishamtambua adui yako ni mtu wa aina gani, tumia ufahamu huo kujitengeneza ili muendane - mkabiliane vizuri.

Hayo ni maoni na mtizamo wangu, nawasilisha.
 
Back
Top Bottom