Namna ya Kuanzisha na Kufanikiwa katika Biashara

Nkandi

Member
Nov 20, 2010
83
42
Katika maisha haya tunayoishi,niliwahi kuambiwa mafaniko ni matokeo ya utekelezaji wa mawazo na utumiaji wa fursa sahihi katika wakati sahihi,yaani kwa ki ulaya "money follows great ideas", katika kupitia magazeti ya 'kizungu' nikakutana na sentensi hii pia "The starting point of all achievement is desire. Weak desire brings weak results" yenye maana chanzo cha mafanikio ni ile hamu ya kufanikiwa,hamu hafifu uleta matokeo hafifu,yawezekana tafsiri yangu isiwe sawa ila kwa jinsi ilivyo hapa kwetu itakuwa imeeleweka

Kufanikiwa kibiashara katika ulimwengu wa sasa kuna maanisha uwepo wa wazo lenye kuleta suluhisho kwa wengine yaani falsafa ya tatizo lako kipato changu, uwepo wa wazo lenye kurahisisha kazi kwa wengine linaweza kukuhakikishia kukuwa kwa biashara yako kwakuwa kunahakikisha uwepo wa wateja wa uhakika

Uwezekano wa kuwapata wateja unafanya uhitaji wa biashara kusajiliwa kwenye mamlaka mbalimbali ilikuweza kuwa na 'uhai wa kisheria' hapa itategemeana na aina ya biashara ambayo mtu ameamua kuianzisha,uhai wa kisheria unatoa fursa biashara kuwa huru kutafuta fursa sehemu yoyote ile na hapa ndiyo hatua ya biashara inapoanza.

Kuanza kwa biashara hakumaanishi kufanikiwa katika soko husika; siri ya kufanikiwa katika soko ni kufahamu aina ya wateja unaowataka na uliowachagua,kufahamu upatikani wao na mahitaji yao;gharama ya wao kupata huduma,namna unavyoweza kuwahudumia tofauti na wafanyabiashara wengine,namna unavyoweza kuheshimu muda wao na jinsi unavyoweza kuwa 'flexible' katika huduma zako kulingana na aina ya mteja.

'Flexibility' inakuhakikishia wateja wa uhakika kwakuwa kila atakayekuja anajua tatizo lake litapata ufumbuzi.Jukumu la kuitangaza biashara linaweza kuwa dogo kwakuwa waliowahi kuwa wateja wako watakuwa mabalozi wazuri na kukutengnezea 'customer network' ambayo ni muhimu kuliko matangazo.

zipo namna nyingi za kufanikisha biashara, Kwa leo,naomba niishie hapa wanajamii.

maswali na majadiriano kkmarketing61@yahoo.com

Nawasilisha.
 
somo lako zuri sana. tafadhali tushushie na nondo nyingine zaidi maana nina hamu na hii elimu ya ujasiriamali kupita kiasi
 
Mkuu, Nkandi, umeeleweka sawia mfumo wa biashara ulimwenguni umebadilika sana na hasa kwenye sekta ya huduma (service industry), hapa lazima kutengeneza mtandao unaoigusa jamii kwa upana na kuleta suluhisho katika jamii husika. Kwa mfano hua ninaguswa sana na kichwa kilicholeta idea ya Mobile money maarufu kama M-Pesa, kwa jinsi jamii inavyoguswa na hii huduma na mtandao wake ulivyo sambaa, Hela lazima ikufuate mpaka uvunguni penda usipende. Naupenda sana huu msemo, Think global and act Local.
 
Ni kweli kabisa Mafanikio siku zote ni Matokeo ya kazi, Na ukiangalia hata wakina Biligate wakati wanaanza Biashara hakuanza ili afanikiwe, Ila mafanikio yamekuja kuwa matokeo ya Kazi aliyo fanya, Mtu kama Henery Ford lengo la kugundua gari si ili awe tajiri ila ugunduzi wake ukaja kufanya Henery ford kuwa Tajiri na ingawa alisha kufa lakini Familia yake watakuwa wana enjoy matunda ya baba yao.

Kwa Tanzania yetu watu wengi sana wamekuwa wakiingia katika biashara kwa malengo tofauti kabisa, Mtu anaingia kwenye biashara ili Anunue Gari, Mtu anaingia kwenye Biashara ili awe tajiri, mtu anaingia kwenye biashara ili awe kama Jirani yake, Mtu anaingia kwenye biashara ili kuwafurahisha ndugu jamaa na marafiki, Matokeo yake ni mtu kufanya business za ajabu kabisa kwa lengo la kutajirika,

Angalia Upangaji wa Bei za Bidhaa hapa Bongo, hii ni jibu tosha kabisa kwamba watu Bongo wanaingia kwenye biashara kutafuta pesa na kutajirika, na hapa wanapo kuja wawekezaji wa nje tunaanza kulalamika,

Angalia kule Kariakoo, Watanzania wanawalaumu wachina kuuza Vitu bei ya CHINI ilahali wote wako eneo moja, wote wanalipa kodi na bei ya umeme inafanana, sasa inakuaje WACHINA WAUZE VITU VYAO BEI YA CHINI? ukiangali utagundua kwamba WACHINA wanaangalia mbali sana na lengo lao ni kutoa huduma kwa wateja na matoke ya kutoa huduma nzuri na ya bei ya chini kwa wateja ni wao kutajirika,

Watanzania ni lazima tubadilike tusifanye biashara kwa lengo la Kununua Magari ya Kifahari, Utakuta mtu anauliza kama biashara fulani inalipa au la, Kwa Dunia ya sasa tutakuja kubakia watazamaji, hatutaweza kushindana na Wachina wala wazungu kwa staili hizi za kusaka utajiri wa harataharaka
 
Ni tips za msingi sana hapa tatizo ni kuwa huwa unakuja mara chache sana hapa jamvini!!!!
 
kweli kaka, ideas watu wanazo...hata mimi niliwahi kupeleka proposal sehemu,imeibiwa....ingawa haijafanikiwa lakini aliyepeleka kwa mlango wa nyuma aliwauzia pesa nzuri....Tabia ya watu wenye access kuwadhulumu watu kwa hapa kwetu imekuwa ni tabia inayojiimalisha na ubaya hata ukisajili,wanabadili mambo mengine hili na wao wasajili pia...so ni tatizo kubwa ambalo litatakiwa kupatiwa ufumbuzi
 
Ni tips za msingi sana hapa tatizo ni kuwa huwa unakuja mara chache sana hapa jamvini!!!!

Kiongozi, nipo mara nyingi sema huwa nasoma vya wenzangu zaidi....ingawa sasa natajitahidi kuwa naandika pia...yale machache nijuayo...
 
Mkuu, Nkandi, umeeleweka sawia mfumo wa biashara ulimwenguni umebadilika sana na hasa kwenye sekta ya huduma (service industry), hapa lazima kutengeneza mtandao unaoigusa jamii kwa upana na kuleta suluhisho katika jamii husika. Kwa mfano hua ninaguswa sana na kichwa kilicholeta idea ya Mobile money maarufu kama M-Pesa, kwa jinsi jamii inavyoguswa na hii huduma na mtandao wake ulivyo sambaa, Hela lazima ikufuate mpaka uvunguni penda usipende. Naupenda sana huu msemo, Think global and act Local.

Mwanahisa,siri kubwa ya mhindi kufanikiwa ni faida ya Tshs.100 ambayo akihudumia wateja 10000...ni sawa na 100*10000=1,000,000 kwa hiyo mzunguko wake unakuwa mzuri kibiashara,sisi tunapenda faida ya hela nyingii hivyo tunaona biashara kitu kigumu sana..kumbe siyo
 
Mkuu hii yakwako nimeipenda sana. Inashangaza watu wengine wanaipita hivihivi wakiona yenye mvuto wa kimapenzi lundo wataisemea. kwa kweli njoo na nyingine nyingi za namna hii tufaidi. Naona pia hii elimu ya ujasiria mali iwe sehemu muhimu katika mitaala yetu. tugeuze vitu na huduma viwe mali.
 
Katika maisha haya tunayoishi,niliwahi kuambiwa mafaniko ni matokeo ya utekelezaji wa mawazo na utumiaji wa fursa sahihi katika wakati sahihi,yaani kwa ki ulaya "money follows great ideas", katika kupitia magazeti ya 'kizungu' nikakutana na sentensi hii pia "The starting point of all achievement is desire. Weak desire brings weak results" yenye maana chanzo cha mafanikio ni ile hamu ya kufanikiwa,hamu hafifu uleta matokeo hafifu,yawezekana tafsiri yangu isiwe sawa ila kwa jinsi ilivyo hapa kwetu itakuwa imeeleweka

Kufanikiwa kibiashara katika ulimwengu wa sasa kuna maanisha uwepo wa wazo lenye kuleta suluhisho kwa wengine yaani falsafa ya tatizo lako kipato changu, uwepo wa wazo lenye kurahisisha kazi kwa wengine linaweza kukuhakikishia kukuwa kwa biashara yako kwakuwa kunahakikisha uwepo wa wateja wa uhakika

Uwezekano wa kuwapata wateja unafanya uhitaji wa biashara kusajiliwa kwenye mamlaka mbalimbali ilikuweza kuwa na 'uhai wa kisheria' hapa itategemeana na aina ya biashara ambayo mtu ameamua kuianzisha,uhai wa kisheria unatoa fursa biashara kuwa huru kutafuta fursa sehemu yoyote ile na hapa ndiyo hatua ya biashara inapoanza.

Kuanza kwa biashara hakumaanishi kufanikiwa katika soko husika; siri ya kufanikiwa katika soko ni kufahamu aina ya wateja unaowataka na uliowachagua,kufahamu upatikani wao na mahitaji yao;gharama ya wao kupata huduma,namna unavyoweza kuwahudumia tofauti na wafanyabiashara wengine,namna unavyoweza kuheshimu muda wao na jinsi unavyoweza kuwa 'flexible' katika huduma zako kulingana na aina ya mteja.

'Flexibility' inakuhakikishia wateja wa uhakika kwakuwa kila atakayekuja anajua tatizo lake litapata ufumbuzi.Jukumu la kuitangaza biashara linaweza kuwa dogo kwakuwa waliowahi kuwa wateja wako watakuwa mabalozi wazuri na kukutengnezea 'customer network' ambayo ni muhimu kuliko matangazo.

zipo namna nyingi za kufanikisha biashara, Kwa leo,naomba niishie hapa wanajamii.

maswali na majadiriano kkmarketing61@yahoo.com

Nawasilisha.

Mkuu nashukuru sana kwa elimu yako ya ujasiriamali toa.
Nimejifunza na nimeambulia kitu.
Naomba uendelee kutupa burudani zaidi nakutuelimisha.
 
Mawazo mazuri sana

Nashukuru mkuu...tuendelee kushirikiana,binafsi naamini mtu atakapoweza kuwa huru kiuchumi ni rahisi sana kufanikiwa katika nyanja nyingine...nimedhamiria kuwa sehemu ya kuielimisha jamii kadri niwezavyo kwa ushirikiano na wengine pia
 
Ni kweli kabisa Mafanikio siku zote ni Matokeo ya kazi, Na ukiangalia hata wakina Biligate wakati wanaanza Biashara hakuanza ili afanikiwe, Ila mafanikio yamekuja kuwa matokeo ya Kazi aliyo fanya, Mtu kama Henery Ford lengo la kugundua gari si ili awe tajiri ila ugunduzi wake ukaja kufanya Henery ford kuwa Tajiri na ingawa alisha kufa lakini Familia yake watakuwa wana enjoy matunda ya baba yao.

Kwa Tanzania yetu watu wengi sana wamekuwa wakiingia katika biashara kwa malengo tofauti kabisa, Mtu anaingia kwenye biashara ili Anunue Gari, Mtu anaingia kwenye Biashara ili awe tajiri, mtu anaingia kwenye biashara ili awe kama Jirani yake, Mtu anaingia kwenye biashara ili kuwafurahisha ndugu jamaa na marafiki, Matokeo yake ni mtu kufanya business za ajabu kabisa kwa lengo la kutajirika,

Angalia Upangaji wa Bei za Bidhaa hapa Bongo, hii ni jibu tosha kabisa kwamba watu Bongo wanaingia kwenye biashara kutafuta pesa na kutajirika, na hapa wanapo kuja wawekezaji wa nje tunaanza kulalamika,

Angalia kule Kariakoo, Watanzania wanawalaumu wachina kuuza Vitu bei ya CHINI ilahali wote wako eneo moja, wote wanalipa kodi na bei ya umeme inafanana, sasa inakuaje WACHINA WAUZE VITU VYAO BEI YA CHINI? ukiangali utagundua kwamba WACHINA wanaangalia mbali sana na lengo lao ni kutoa huduma kwa wateja na matoke ya kutoa huduma nzuri na ya bei ya chini kwa wateja ni wao kutajirika,

Watanzania ni lazima tubadilike tusifanye biashara kwa lengo la Kununua Magari ya Kifahari, Utakuta mtu anauliza kama biashara fulani inalipa au la, Kwa Dunia ya sasa tutakuja kubakia watazamaji, hatutaweza kushindana na Wachina wala wazungu kwa staili hizi za kusaka utajiri wa harataharaka

Mkuu pongezi kwa kutoa mawazo yako kulingana na hali halisi ya soko letu hapa nyumbani. Lakini naomba nitofautiane nawe kidogo katika mistari niliweka rangi nyekundu. Definition yoyote ya "business" ina element ya faida (profit or return on investment), hivyo kwa tafsiri yako kuwa watu wasiingie kwenye biashara kwa ajili ya kutengeneza pesa sio sahihi. Biashara yoyote ina uwekezaji na hakuna mtu anayetaka kuwekeza rasilimali bila kupata zaidi ya alichowekeza. Labda kuiweka sawa tunaweza kusema, tatizo la wafanyabiashara wa kitanzania wanataka hiyo faida kubwa isivyo na uhalisia (high expectations which are incompatible to the reality). Kuhusu, Wachina kuuza bidhaa zao kwa wateja wao kwa bei nafuu, inaweza kuelezewa na mambo mengi ikiwepo aina ya soko (market segment) wanalolihudumia, ubora wa bidhaa wanayoiuza katika soko hilo na mkakati wao wa masoko (marketing strategies) nk. Hata hivyo hili ni somo pana katika uhalisia wake.
 
Mkuu heshima kwako,

Nadhani alicho kua anamaanisha ni kuwa, watu tunataka profit margin kubwa sana mpaka tunakumbiza wateja... usimpe mtu huduma anaondoka analalamika kuwa kitu chako ni ghali sana lakiniafanyeje..... akiondoka ananung'unika basi ujue umeshapoteza huyo....! Pamoja na kuwa Focus yako ni kutoa huduma inaambatana na ujira...wako (faida), focus yako ilkiwa ni faida ili uwe tajiri utauza ghali ili uwe tajiri
 
Tatizo na biashara za "mswahili" zinaendeshwa kijanja janja zaidi. Mfano bei ya biadha au huduma inategemea muonekano wa mteja! Ukionekana mtu wa vijisenti basi bei itapanda maradufu. Binafsi nilihamia supermarket kwa mahitaji yote vyakula/consumer electronics/nguo etc. Hapa Kila kitu transparent na biadhaa zote zimetiwa price tag, hivo kuokoa bugdha ya kuuliza bei.
 
Back
Top Bottom