Namna unavyokutana na baba yako baada ya miaka 30 - Story ya Frida

platozoom

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
9,364
11,150
Namzungumzia Annifrid Lyngstad au kwa jina jingine Frida mwimbaji wa kundi maarufu la Abba kutoka Sweden lilovuma sana miaka ya 70 na 80.

Wakati wa vita ya pili ya dunia askari wa kijerumani walikuwa wamepiga kambi katika mji mdogo wa Ballangen nchini Norway na walikuwa wakiogopeka sana nyakati hizo na wenyeji wa mji huo.Katika pitapita za mtaani mmoja wa askari hao wa kijerumani kwa jina la Alfred Haase alikuwa akimuona binti mmoja mrembo akipita kila mara kuelekea kuteka maji..Alivutiwa nae japo ilimchukua muda kiasi kumpata,lakini hatimae alifanikiwa kuingia kwenye mapenzi na binti huyo kwa jina la Synni Lyngstad.

Kutokana na askari hao kuogopewa na kuchukiwa na wenyeji wa mji ule,Alfred (askari) na Synni walikuwa wakikutana kwenye hema lake kwa siri bila ya watu wengine kujua japo baadae mama yake na na Syin kwa jina Agny alistukia mchezo japo alikuwa ameshachelewa – Syn tayari alishapata ujauzito.


La kusikitisha zaidi baada ya wiki kadhaa Alfred alirudi ujerumani na wanajeshi wenzake baada ya Ujerumani kushindwa vita ya pili ya Dunia.Na ikahisiwa kwamba wamefariki wakati meli waliyokuwa wakisafiria ilipozama baada ya kupigwa na dhoruba.
Syin alijifungua salama mtoto anayeitwa Frida au Annfrid Lyngstad mwaka 1945, na baada ya miezi 18 Syin na mama yake (bibi yake Frida) walihamia katika mji wa Esklistuna nchini Sweden.


Baada ya miaka miwili mama yake FRIDA akafariki dunia akimwacha Frida kulelewa na bibi yake –Agny.Taratibu akiwa na miaka 11 Frida akaanza kuonyesha kipaji chake cha uimbaji akianzia na matamasha madogomadogo katika mji wa Esklistuna,baadae katika bendi kadhaa kabla ya yeye na wenzake kuunda kundi lilokuja kuwa maarufu kwa jina la ABBA mwaka 1972 akiwa na miaka 27.


Tayari Frida alishakuwa maarufu na pesa nyingi anapata lakini kuna kitu moyoni kinamsumbua –Baba yake - .Pamoja na kuelezwa na Bibi yake kwamba inadhaniwa meli aliyokuwa akisafiria baba yake ilizama kwenye maji lakini hakuridhika na maelezo hayo.Kila siku alikuwa na shauku kubwa ya kukutana na baba yake na hasa baada ya kuona picha ya mama yake akiwa amekaa kimahaba na askari wa kijerumani. Alitumia gharama nyingi kumtafuta bila mafanikio.


Jioni Fulani miaka ya 80 nchini Ujerumani mzee mmoja aliekuwa amepigika alikuwa amekaa kwenye kijumba chake akitazama televisheni bila kutilia maanani sana kilichokuwa kinaendelea.Lakini ghafla akatega sikio na kukodelea macho TV yake kumsikiliza mwimbaji maarufu wa nchini Sweden toka kundi la ABBA,kwa jina Frida (au kwa jina jingine Anni-Frid Synni Lyngstad).Kilichomvutia sio huyo mwanamuziki (kwa sababu alikuwa akimfahamu sana) bali story ya maisha yake aliyokuwa akiitoa –kuanzia maisha ya mama yake hadi kuzaliwa kwake.


Mzee yule alistuka sana kwa sababu anakumbuka vizuri alivyokutana na msichana wa Ki-Norway alipokuwa mwanajeshi na namna walivyopendana sana kabla ya yeye kuondoka, na ndicho hichohicho Frida alichokuwa anakielezea kwenye mahojiano….Lakini asichokifahamu ni kwamba hakumbuki kumwacha mpenzi wake Syn na ujauzito – lakini mbona maelezo ya awali yanamhusu yeye?Mbona Frida anafanana na mpenzi wake wa zamani?


Huku kijasho kikimtoka akaenda chumbani na kufukua picha za kumbukumbu….Akaipata picha aliyopiga na Syn kimahaba kwenye hema.Akapiga simu kwenye moja ya chombo cha habari huku akiwaeleza kwamba yeye ni Alfred Haas na kwamba ana hakika mwimbaji maarufu wa kundi la ABBA (Frida) ni mtoto wake.


Kifupi habari zilienea kwa kasi na zikamfikia Frida ambae haraka alienda Ujerumani na picha za mama yake. Alipomuona Alfred moyo ukapiga…wakakumbatiana lakini Frida alikuwa Tomaso ilibidi kwanza alinganishe picha alizokuwa nazo Alfred, zake na story za hapa na pale……Ilikuwa ni wazi Alfred alikuwa baba yake Frida,mwimbaji maarufu wa kundi la ABBA.
 
Back
Top Bottom