Namlilia FARAJI H.H. KATALAMBULA wa Igalula Tabora

Mzizi wa Mbuyu

JF-Expert Member
May 15, 2009
7,320
6,806
Jamani katiaka kupitia pitia magazeti niliyonunua leo baada ya kutoka kwenye ibada, nimekutana na habari ambayo imenishtua na kunitia majonzi makubwa.
Habari hii nimeipata toka ktk gazeti la Mwananchi kwenye makala inayoandikwa na mwandishi Freddy Macha(Kalamu toka London). Habari hii imeandikwa "Kifo cha mwandishi mashuhuri Faraji Katalambula - 2)

Mwenzenu sina habari kabisa kuwa huyu mwandishi amefariki...na kinachonisikitisha zaidi ni nimepata habari baada ya karibia mwezi mzima kupita tangu afariki! lakini nimeumia zaidi na zaidi mno kuona hata mwandishi anakiri kuwa kifo hicho kimepita kimyakimya!!!! Vipi wana JF habari hii ilitoka humu? mbona sijaiona?

Huyu alikuwa ni mwandishi wa hadithi zenye kusisimua mno...! ukiacha hadithi za utotoni katika maisha yangu hadthi za Marehemu katalambula zilikuwa kati ya hadithi za mwanzo kabisa kuzisoma na kuzikubali mno....ilikuwa kila wakati natafuta vitabu vyake na kuvisoma na wakati mwingine kuzirudiarudia hadithi zake....zilikuwa nzuri mno!

Mfano; kulikuwa na vitabu vingi naweza kuvikumbuka hata sasa na kimoja cha SIMU YA KIFO ninacho hata sasa kwenye kabati langu la vitabu.

Simu ya kifo kilikuwa na Stori ya Inspekta Far Katy Wingo aliekuwa anapeleleza ..kifo cha mzee jacob..ambaye alikufa akivuta sigareti.. kisa hiki kimsumbua mno Inspekta Wingo.. na kila alipokuwa napiga hatua mtu ambaye angemsaidia kupata ufumbuzi alikuwa anauliwa! yaani ilikuwa balaa wengine walipigwa risasi n.k.......mwisho wa mkasa huu ilikuwa Inspekta Wingo nae auawe akapigigiwa simu na mtu aliyekuwa anamsumbua sana kumtambua kwani alijitamtulisha kama FAMBO tu na kumpa taarifa mbalimbali za mauaji..... Lakini katika hatua ya mwisho jamaa ajitambulisha kama Fransis Andrea Mbozia!!!!
.......bwanawee hadthi hizo zilikuwa zinatukolea mno wenzenu tuliokuwa tuna kua enzi zile za mwalimu! zilkuwa ndiyi sinema zetu.n.k

Pili Pilipilipili...ni kitabu kingine ..kilichokuwa kinamuelezea bwana mmoja aiepata mihela Dar akaamua kwenda kwao Igalula Tabora kuoa then arudi dar ajende nyumba au anunue motokari. Lkini alipokuwa kwenye garimoshi kwenda kwao Tabora alikutana na msichana mmoja alieitwa Pili Pilipilipili! ahuyu dada alikuwa mzuri ajabu!!
Jamaa akakolea kiasi cha kushindwa kushuka nyumbani kwao Igalula! huku akiwaona mama yake , wadogo zake, mchumba wake na ndugu zake wengune wakichungulia nkwenye madirisha ya treni huko Igalula....akapitiliza hadi Mwanza alikoibiwa kila kitu pamoja na ile pesa yoote aliyopanga kuja kujengea Dar...hakuwa hata na nauli!!

Jamani alitunga vitabu na majarida mengi yaliyokuwa na hadithi nzuri na zenye mafundisho mengi ya kupendeza....
Hata huyu mzee Kipara marehemu aliefariki hivi karibuni pia aliwahi kumtumia katika hadhi nyingi za mapicha....
Hadithi ya mapicha iliyo kuwa maarufi ni Lawalawa...hii ilimhusisha dada mmoja jina lake lawalwa aliekuwa mwnyeji wa Tabora alieolewa DSM na Bwana mmoja aitwaye Dhati(Mzee Kipara)...sasa siku moja Lawalawa alipokuwa nyumbani kwa Tabora akaandika barua mbili kwenda DSM ...
Moja akaiandka kwa mumewe akimwambia atarudi muda si mrefu na numbani tabora hawajambo. Ya pili akaiandika kwa Hawara yake anaeishi Dsm pia akimweleza anavyompenda basi tu kaolewa na libwana libaya! na maneno mengine mengi yenye huba huku akimalizia jinsi walivyokula maraha alipomdanganya mumewe kuwa anaenda moja kwa moja Tabora kumbe anashuka kituo cha njiani ambapo alikaa na hawara huyu karibia wiki!!!....sasa ktk kuzituma akachangaya bahasha barua ya hawara akaiweka kwenye bahasha yenye anuani ya mumewe!! akajagundua baadae kuwa amekosea....akaanza kuifuatilia posta tabora waapi! akasafiri hadi dara ghafla ili aiwahi kabla mumewe hajaisoma aagh!!!!.....

Zilikuwa hadithi nzuri mno!

Kwa watakao soma thread hii hadi mwisho nawapongeza, hasa vijana wa kisasa kwa udadisi tafuteni hadithi za watu wa zamani enzi za mwalimu someni mlinganishe ubora wa kazi kuna mengi ya kujifunza...
Hata sisi enzi zetu tulitafuta hadithi walizosoma watu wa zamani na takafurhia waliyasoma walitutangulia na kutambua kuwa zilikuwa tungo nzuri mno hadi kama Safari ya bwana Alan Quterman na wenzake, Kisiwa chenye hazina , Mashimo ya Mfalme Solomon n.k

BWANA alilaze mahali pema roho ya Hayati Fraji Hussein Hassan Katalambula!...

Kizazi hiki kimeshindwa kukuomboleza na kukuenzi lakini naamini kuna kizazi cha uongozi bora kinakuja kitakacho tambua na kuenzi kazi yako wewe na magwiji wengine mlio tufungulia taifa letu changa wakati huo kwa tungo nzuri zenye kutunza maadili na utamaduni wa mwafrika na mtamzamia kwa ujumla....

AMINA!!
 
Back
Top Bottom