Nimeshtuka kidogo kusikia muswiba wa Mohamed Makani au wengi walivyozoea kumuita (Bob Makani). Kwa kweli ni mswiba mkubwa sana na Tz wamepoteza jabali lisiloteteleka wala kutingisika.
Binafsi nilimfahamu Mohammed Makani mwaka 1974 wakti huo akija nyumbani kwa ammi yangu marhum Eng. Abdullah Salem Al harthy, mtaa wa mazengo upanga ambaye alikuwa rafiki yake kipenzi sana na walipenda sana kuongea kisukuma.
Na alinisaidia sana katika utendaji wangu wa Kazi wakti nikiwa Wizara ya fedha na hata nilipopelekwa Mwanza wakti akiwa BOT kama naibu gavana (Bara) na vile akiwa naibu wanasharia mkuu.
Ni mtu makini sana na asiyyemung'unja maneno na masema kweli daima. nakumbuka mara ya mwisho nilikutana nae siku nilipokwenda Mbazi beach kumwangalia Brig General Mwakanjuki mwezi mei 2011 nilipita mpaka kwake jioni na tuliongea sana. Nakumbuka neno lake la mwisho ni kuwa lazima Tanzania itabadilika na ukweli utawala. WaTz wameshaelimika na kuchagua ukweli kuachana na batili.
Nakukumbuka sana Mohamed Makani.
Inna Lillahi wainna illaihi rajihunna.
I concur with you sir.RIP Mohamed Makani.