Namfagilia January

makandokando

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
299
20
Wadau, kwa kweli ingawa baba yake huju kijana anaharibu mbaya, lakini mi namkubali sana huyu jamaa.

Nadhani tukiwa na viongozi kama hawa Tanzania ijayo itakuwa nzuri sana. Anaonekana kuwa amesoma, ameelimika na anajua anachokifanya.

Ni bahati mbaya tu yupo kwenye upande ambao sio wenye (CCM), otherwise mambo yake bomba.

Tuangalia tu huko Bumbuli baada ya miaka mitano kutakuwaje. Sidhani kama nahitaji kulist mambo yake, kwa sababu, tofauti na viongozi wetu wengine wenye longolongo nyingi na walioamua kuendelea kukaa karne za enzi za mawe, huyu jamaa ana website (moja ya kitu ninachomfagilia, wabunge wetu wengine sijui kama wanawebsite zitakazotupa habari kuhusu mambo wanayoyafanya) na ukienda kwenye website yake unaweza kumfahamu vizuri.

Ila big up January, keep it up....proud of you.
 
endelea kumfagilia kwa kuwa ana website mmwombe kabisa akubusu na kukuchum.
 
Jamani MODS tafadhalini sana, JF imeboleshwa na ina muonekano wenye mvuto zaidi, naomba sana msiishie hapo tu, muanze na kuchuja thread za members wa JF. sasa mtu kama huyu anayetuandikia upupu wake hapa eti Janualy ana website, so what! ni wakazi wangapi wa Bumbuli wanaojuwa kutumia computer? na ni wangapi wenye internet access? please remove this CRAP. Tunataka kuambiwa hapa amejenga barabara ya lami kilomita ngapi, visima vya maji salama vingapi, zanahati ngapi, madarasa mangapi, sio upupu kama huu RUBBISH.
 
Website tu ndio inamfanya kuwa kiongozi bora !!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Yeye anajua maendeleo ni simu tu kwa vile dada yake yuko Vodacom? Watu wa Bumbuli shida yao kweli ni mawasilianoau anataka kuisogeza Vodacom kwa masikini?Soma hii makala toka Mwanachi:

Zulfa Msuya,aliyekuwa Tanga

MBUNGE wa Bumbuli, Januari Makamba, amezindua huduma ya mawasilino na wakazi wa jimbo lake ambao watakuwa wanatuma ujumbe mfupi katika simu zao na gharama za malipo zinakuwa chini yake.Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Makamba alisema mawasiliano ya simu ni muhimu katika kuharakisha maendeleo.

Alisema kwa kuzingatia hilo , wananchi wa Bumbuli lazima wawe miongoni mwa mamilioni ya Watanzania wanaopaswa kuwa na mawasiliano hayo, ili nao wapige hatua za haraka maendeleo."Nimefanya mazungumzo na kampuni za simu,lengo ni kuleta mawasiliano karibu ili wananchi wangu waweze kunufaika na mpango huo. Nitafanya semina elekezi ya viongozi ili waweze kuwahamasisha wananchi wa Jimbo la Bumbuli kuhusu mpango huo,"alisema Makamba.

Mbunge huyo wa Bumbuli aliandaa semina ya viongozi wa kata, viti wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa lengo la kupangiana majukumu ya kutekeleza Ilaani ya CCM.Alisema kwa kipindi kirefu, wananchi wa jimbo hilo wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali za kimaendeleo na kwamba hadi sasa bado wako nyuma.Alisema kwa msingi huo, kuna kila sababu za kubuni mikakati ya kujiletea maendeleo kwa haraka."Kwa miaka mingi sasa tumekabiliwa na tatizo la kutafuta maendeleo na bado hatujafanikiwa, lakini nadhani wakati umefika wa kutoka kwenye boksi na kufanya kazi kwa bidii ili tupate maendeleo,"alibainisha.Kwa mujibu wa Makamba, wajibu wake kutekeleza ahadi alizotoa kwa wananchi wa jimbo hilo, ambalo kabla ya uchaguzi wa Oktoba mwaka jana, lilikuwa linawakilishwa bungeni na Wiliam Shellukindo ambaye alishindwa katika kura za maoni ndani ya CCM.

Mbunge huyo wa sasa, aliwataka wananchi kushirikiana na viongozio wao, ili iwe rahisi kutekeleza mikakati ya kujiletea maendeleo katika nyanja mbalimbali.Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Sophia Mjema, aliwataka viongozi wote walioko madarakani, kutekeleza ahadi zao kwa wakati.Hali kadhalika aliwahimiza watendaji wa vijiji, kuwasomea wananchi mapato na matumizi ya fedha wanazochanga, ili kusaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Alisema kufanya hivyo, kutawafanya wananchi wawe na imani na viongozi hao.
Wakati huo huo, baadhi ya wananchi walitoa malalamiko yao kwa uongozi wa Jimbo hilo kuwa, baadhi ya watendaji wa kijiji wamekuwa wakiwatoza fedha katika kupata huduma mbalimbali.

Huduma hizo ni pamoja na kupigiwa mihuri, kuandikiwa barua na kadhalika.

Kuhusu hilo, Mkuu wa Wilaya alionya viongozi wa vijiji kuacha mara moja kuwatoza wananchi gharama za mihuri au kuandikiwa barua.
 
Huyu Hapa

IMG_0325.jpg
 
Hahahaaa, ningekuwa sijafika na siifahamu bumbuli, ningekubaliana na mtoa mada, bahati mbaya sana, nimefika huko na nilifanya kazi huko, wanamaisha magumu sawa na any rural area ya bongo, wana umeme kwa sababu ya bumbuli hospital (KKKT) na kwa sababu ya coffee plantation kwa wenye kumbukumbu za histori na RC Fathers-Sakarani panapotengenezwa wine, kua na website hata mimi nina yangu, je niende kwetu nitakua mbunge? Januari hakuzaliwa wala kukulia bumbuli, no issue
 
hivi watu kwa nini mna hasira hivyo? too emotional! kumbukeni hili ni jukwaa la great thinkers na sio jukwaa la watu wenye jazba za kinanihii.....

punguzeni jazba, toeni hoja.....vinginevyo hatutafika tunakokwenda.
 
Sasa wewe hapo ndio umetoa hoja gani? THIS HERE WE CALL A CRAP
 
Jamani tumwache mwanzishaji mada yuko kazini! Hii ishu ya website tulishawahi kuichambua naona wameileta kwa staili mpya. Ila tujue kuwa kijana huyu ni full of hotair! It will take more than a fancy website to convince us otherwise!
 
Wadau, kwa kweli ingawa baba yake huju kijana anaharibu mbaya, lakini mi namkubali sana huyu jamaa.

Nadhani tukiwa na viongozi kama hawa Tanzania ijayo itakuwa nzuri sana. Anaonekana kuwa amesoma, ameelimika na anajua anachokifanya.

Ni bahati mbaya tu yupo kwenye upande ambao sio wenye (CCM), otherwise mambo yake bomba.

Tuangalia tu huko Bumbuli baada ya miaka mitano kutakuwaje. Sidhani kama nahitaji kulist mambo yake, kwa sababu, tofauti na viongozi wetu wengine wenye longolongo nyingi na walioamua kuendelea kukaa karne za enzi za mawe, huyu jamaa ana website (moja ya kitu ninachomfagilia, wabunge wetu wengine sijui kama wanawebsite zitakazotupa habari kuhusu mambo wanayoyafanya) na ukienda kwenye website yake unaweza kumfahamu vizuri.

Ila big up January, keep it up....proud of you.

Yaani mbunge kuwa na website ndo imekuchanganya??? bado namlaani kwa mabaya aliyoyafanya akiwa ikulu ana roho mbaya sana huyu jamaa.
 
Wadau, kwa kweli ingawa baba yake huju kijana anaharibu mbaya, lakini mi namkubali sana huyu jamaa.

Nadhani tukiwa na viongozi kama hawa Tanzania ijayo itakuwa nzuri sana. Anaonekana kuwa amesoma, ameelimika na anajua anachokifanya.

Ni bahati mbaya tu yupo kwenye upande ambao sio wenye (CCM), otherwise mambo yake bomba.

Tuangalia tu huko Bumbuli baada ya miaka mitano kutakuwaje. Sidhani kama nahitaji kulist mambo yake, kwa sababu, tofauti na viongozi wetu wengine wenye longolongo nyingi na walioamua kuendelea kukaa karne za enzi za mawe, huyu jamaa ana website (moja ya kitu ninachomfagilia, wabunge wetu wengine sijui kama wanawebsite zitakazotupa habari kuhusu mambo wanayoyafanya) na ukienda kwenye website yake unaweza kumfahamu vizuri.

Ila big up January, keep it up....proud of you.

Wewe huko diagnostic hata kidogo.Ukweli ni kwamba unampenda kwa sababu ya his material accomplishments.Wengi walioko vijijini wangepata nafasi kama yake wange-perform wonders.To me kijana huyo ana mapungufu mengi sana ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya na nafasi ya baba yake ambayo imemsaidia kupata ubunge.Mwenye busara angesema mimi na baba yangu we are okay, nafasi hii tuwaachie wengine!
 
wadau, kwa kweli ingawa baba yake huju kijana anaharibu mbaya, lakini mi namkubali sana huyu jamaa.

Nadhani tukiwa na viongozi kama hawa tanzania ijayo itakuwa nzuri sana. Anaonekana kuwa amesoma, ameelimika na anajua anachokifanya.

Ni bahati mbaya tu yupo kwenye upande ambao sio wenye (ccm), otherwise mambo yake bomba.

Tuangalia tu huko bumbuli baada ya miaka mitano kutakuwaje. Sidhani kama nahitaji kulist mambo yake, kwa sababu, tofauti na viongozi wetu wengine wenye longolongo nyingi na walioamua kuendelea kukaa karne za enzi za mawe, huyu jamaa ana website (moja ya kitu ninachomfagilia, wabunge wetu wengine sijui kama wanawebsite zitakazotupa habari kuhusu mambo wanayoyafanya) na ukienda kwenye website yake unaweza kumfahamu vizuri.

Ila big up january, keep it up....proud of you.

kweli umekanda
 
duuh!hiyo picha ndio ya the so called mbunge january makamba, pole mnaomfagilia
 
endelea kumfagilia kwa kuwa ana website mmwombe kabisa akubusu na kukuchum.
:

Mwancheni mwaya, hata mimi namfagilia maana anamiliki gari aina ya X5 alilopewa na mafisadi kwa sababu ya ku-facilitate kuingiza vi mem:hungry:eek: vyao mezani kwa mkulu.
 
Hiyo huduma ya sms kwa wanajimbo lake na website vimetolewa kwa hisani ya 6telecom aka rashidi shamte
 
Back
Top Bottom