Namba 10 kwenye Orodha: .... BENJAMIN W. MKAPA... Anaachwa vipi kusimama Jukwaani?

CDM wameanza lini kumuogopa Mkapa na ni kwa nini kama wanamuogopa walimpa namba katika ile 'list of shame'.Something must not be okey hapa!
 
Mkjj hayo yalifeli Igunga...........
BTW wananchi wanataka kusikia sera za CDM na si mipasho na ngojera ya miaka nenda rudi "UFISADI" na wakishindwa ninyi akina Mkjj ndio wakwanza kuja kusema CDM hawana sera zaidi ya ufisadi
 
Mojawapo ya vitu ambavyo labda vitahitaji majibu baadaye ni kwa vipi CDM wakati wa uzinduzi wao hawakumgusa kwa uzito unaotosha aliyekuwa Rais wa Tanzania wakati matukio mazito ya ufisadi yanatokea yaani B. W. Mkapa. Katika thread hii mengi yamejadiliwa kumuhusu Mkapa: MKAPA ABOVE THE LAW? Chama cha Demokrasia na Maendeleo kilitambua kuhusika kwa Mkapa katika maamuzi ya kifisadi kiasi cha kumuweka namba 10 katika ile "Orodha ya Aibu" akiwa miongoni mwa kina Ballali, Rostam, Lowassa n.k. Katika maelezo ya orodha hii ilisemwa hivi:

Hiyo ni sehemu kidogo tu kwani baadaye tumeweza kuona mengi sana yaliyotokea wakati wake kama Rais na hasa wakati wa mwaka wake wa mwisho. Ikumbukwe ndiye aliyewakingia kina Ballali, Rostam na wengine. Ninajiuliza maswali yafuatayo:

a. CDM inamhofia au kumheshimu Mkapa kiasi kwamba yawezekana hakiamini kabisa kuwa anahusiana na ufisadi mkubwa kabisa uliowahi kutolewa nahivyo wananchi hawapaswi kukumbushwa?

b. CDM inaamini kuwa Mkapa hagusiki kwa vile Rais Kikwete alisema "muacheni mzee wetu astaafu" wakati hataki kustaafu anapenda kujihusisha na siasa? Kama anajiingiza kwenye siasa kwanini yeye mwenyewe naye aliyoyafanya yasiwe issue kwa Watanzania?

c. CDM inafikiria kwa mfano atakaposimama leo kuzungumza huko Arumeru Mkapa atawaonesha huruma wapinzani na viongozi wao? Hivi akizungumza na kuwabeza wapinzani na kuwaita majina ya ajabu ajabu na kuwafanya duni viongozi wao atakuwa amewaonea au anafanya kile kinachotegemewa kama mwanasiasa wa CCM? Kama yeye hatowaheshimu - tayari kwa kukubali kushiriki kampeni hizi ameonakana hajali sana mambo ya upinzani - kwanini wao wanafikiria kumheshimu katika hili?

Nini cha kufanya basi?

a. CDM ioneshe kuwa CCM inamtumia mmoja wa viongozi waliosimika mfumo wa utawala wa kifisadi nchini mtu ambaye ana damu ya Watanzania mikononi mwake.

b. CDM ioneshe kuwa matatizo mengi ya madini nanishati yamejengwa kutokana na sera na sheria ambazo zilipitishwa na Mkapa.

c. CDM ioneshe vile vile jinsi kiongozi huyo huyo alivyoendelea kawaida ya kubeba na kubebana na kutolea mifano watumbalimbali. Ikumbukwe pamoja na yote yanayosifiwa kuhusu Mkapa bado leohii tunavuna mavuno ya uongozi wake.

d. CDM ioneshe kuwa mojawapo ya mambo ya ubaguzi wa rangi nchini kufanywa na wanasiasa yalifanywa wakati wautawala wake kuhusiana na Salim na jinsi gani yeye Mkapa kama kiongozi aliyelelewa na Nyerere alishindwa kuwazuia wale waliokuwa nakiu ya madaraka hadi kutupatia viongozi wa sasa. Kwa kifupi ioneshe kuwa viongozi wanaopigiwa debe na Mkapa ni utangulizi wa ufisadi!

e. CDM ioneshe kuwa CCM ilikuwa na nafasi nzuri ya kuonesha imeamua kweli kujivua gamba lakini yale yaliyotokea leo hii huko Arumeru na hasa kuhusishwa kwa BWM kunaonesha tu kuwa gamba limegoma na sasa limeganda na gamba likiganda linakuwa donda! Wapo baadhi ya watu wazuri sana ambao CCM ingewez akuwatumia lakini kwenda kumtumia mfalme wa magamba ni kosa kubwa la kimkakati!

CDM isiposhambulia pasipo huruma CCM na sera zake, isipoonesha kuwa matatizo yanayowakabili watu wa Arumeru (na sehemu nyingine nchini) yanatokana na kushindwa kwa sera za CCM (siyo kutekelezwa tu bali kushindwa in substance) basi itajikuta inaletwa karibu na kilele nakuachwa hewani! CDM ni lazima ichore mstari, iwagawe wananchi na kuwachochea wananchi kugawanyika kifikra. Pasipo kugawa fikra, hawatagawa kura!

uko sawa kabisa!!! Ulijuaje!?
 
Mkapa ni Roman Catholic
Lowasa ni Mlutheran..
Rostam is a Muslim

Just saying!
 
Mkapa ni Roman Catholic
Lowasa ni Mlutheran..
Rostam is a Muslim

Just saying!

And what is so common amongst them? Maana tumeona dini si kigezo cha watu kuungana au kufanya mambo yatakayofanana. Na dini pia inatukumbusha mtu anapata thawabu au kuhukumiwa kutokana na matendo yake.
 
Mwanakijiji,

..sasa hivi mafisadi ni watu watatu; Rostam,Chenge,na Lowassa. Thanks to Nape na "wapiganaji" wa CCM.

..wanachoweza kufanya CDM ktk hizi kampeni ni kumuunganisha Mkapa na matatizo ya ardhi na maji yanayowakabili wana Arumeru kwa miaka lukuki sasa.

..Kwa kifupi Mkapa alikuwa Raisi kwa miaka 10, na hakufanya jitihada zozote kutatua kero kuu za wananchi wa Arumeru.

..zaidi, CDM wanaweza kuwasomesha wapiga kura kwamba CCM[na Tanu kabla ya hapo] imekuwa madarakani kwa miaka 50 na lakini kimeshindwa kutatua matatizo ya wananchi.
 
Mkuu uko sawa kabisa. Arumeru sio rahisi kama watu wanavyojiaminisha. Ukiangalia mgawanyo wake unatenganishwa na barabara ya Arusha - Moshi. Upande wa kusini unaoenda mpaka maeneo ya mererani unamchanganyiko mkubwa sana wa makabila na huku ndiko chadema inaweza kufanikiwa zaidi. Upande wa kaskazini huku kuna wameru peke yao. Sasa kwa mila za kimeru uongozi wa koo una sauti kubwa sana juu ya maamuzi. Mathalan SIYOI na NASARY wako kwenye ukoo mmoja. inamaana kama ukoo mmoja utagawanyika utsababisha na koo nyingine kugawanyika pia.
Kwa sababu hizi CDM ilitakiwa kuua nzi kwa Rungu! CCM wakipata nafasi huwa hawaichezei! Hebu fikiria wewe unapata mafuriko ya watu wanaokuja wenyewe kwenye mkutano wako halafu mwenzio anapata idadi kama yako lakini akiwa amewalipia nauli na chakula unadhani akiipata nafasi ya kukuua ataiacha?
Kingine ninaweza kuwa na hofu ya CDM kuwa corrupted. Sote tunakubaliana kwamba gharama za kuendesha CDM zimekuwa kubwa kupita matarajio. Haraka haraka unaweza kujiuliza watamudu vipi? sasa hapa napata shaka kama baba mkwe hajaamua kumnunulia mwanae ubunge kwa sharti ufisadi na mafisadi wasitajwe!
VIONGOZI WETU MSIANZE KUWA SOFT!

Hapo kwenye nyekundu siyo sawa SUMARI NA NASSARY ni koo mbili tofauti zinazo-originate sehemu mbili tofauti by the way uchaguzi haufanyiki kwa minajili ya koo lakini ukoo wa NASSARY ni mkubwa kuliko sumary
 
Mkuu, tunahitaji BWM atwambie aliko Ballali wakati akiendelea na kampeni za kumnadi mgombea wa CCM.
 
Bila shaka CDM watalifanyia kazi hili pia kwani wamekuwa wasikivu mara nyingi nakumbuka walivolichukua pendekezo la manager wa kampen naamini na hili litashughulikiwa ipasavyo Asante wakuu tuendelee kuwakumbusha CDM na mengineyo kwa faida ya Tanzania na vizazi vijavyo.
 
Kwani Mkapa ndio anagombea hicho kiti? hizi ndio siasa uharo.

Wewe vipi bwana hujui siasa au unaongea tu!!! Hivi hujafikiria kwa nini ankwenda kumpigia kampeni Sioi?? Hivi hukuwahi kusikia wakati Al Gore anagombea Urais na gearge Bush 2000, Clinton alizuiwa kwenda kumpigia kampeni kwa vile alikuwa na kashifa?? Sasa unganisha hayo niliyoeleza hapo juu then utajua kwa nini MKJJ anasema haya.
 
Bila shaka CDM watalifanyia kazi hili pia kwani wamekuwa wasikivu mara nyingi nakumbuka walivolichukua pendekezo la manager wa kampen naamini na hili litashughulikiwa ipasavyo Asante wakuu tuendelee kuwakumbusha CDM na mengineyo kwa faida ya Tanzania na vizazi vijavyo.

CDM wanahitaji msaada mkubwa wa vyombo vya habari kueneza ubaya wa BWM na jinsi alivyowafanya na anaendelea kuwafanya Watanzania wajinga. Juzi CDM waliibua suala la ardhi Arumeru naushiriki wa Mkapa kupokonya ardhi ya Wameru akishirikiana na kina Jeroin wa Kiliflorah na kaka yake Jeroin wa Tanzania Flowers na kuwadi wao mkuu akiyekuwa mbunge wa Arusha Felix Mrema. Ni chini ya utawala wa BWM na Basili Mramba serekali kupitia udhamini wa Bank kuu iliwapa mabilioni ya shs wazungu hawa na Mh Felix Mrema wa La Fleu Da Frique kurestucture makampuni yao. Mkopo huo ambao upo TIB haujalipwa hadi leo hii. Cha ajabu BWM alilijua hili na aliidhinisha mkopo huo kwani ni mabilioni ya shs.
Bila aibu BWM kamkana Jeroin na kuwadanganya wameru kuwa atalifikisha suala la ardhi kwa JK. Upuuzi gani huo? Suala la ardhi ya meru halijaanza jana Mkapa alilijua akiwa raisi mbona hakulifikisha kwake mwenyewe bali akawapa mafedha waholanzi hawa fedha za wavuja jasho wa nchi hii. Bila hofu ya Mungu BWM anasema yeye ni mtetezi wa wanyonge! Kweli nchi imekosa woga wa mungu
Vyombo vya habari fuatilieni hii story mugundue ushiriki wa BWM kwenye kuwapokonya wameru ardhi. Kiongozi anayetanguliza matusi na mkwala bila kujibu hoja ni hatari na anajua analolificha. Kuna siku dhambi hizi zitajibiwa tu
 
Upande mwingine ni kuamua kumuacha tu; si walifanya hivyo Igunga kwanini kuanza Arumeru?
 
Kwa ujinga wa Wadanganyika wataamini Mkapa anaweza zaidi kuwarudishia ardhi zao wakasau ya mbunge...
 
ICHONDI,

..kwa kweli hapo hamna cha kuongeza.

..sasa CDM na Joshua Nassary wawasomeshe wapiga kura kuhusu uovu wa Ben Mkapa.
 
Nini cha kufanya basi?

a. CDM ioneshe kuwa CCM inamtumia mmoja wa viongozi waliosimika mfumo wa utawala wa kifisadi nchini mtu ambaye ana damu ya Watanzania mikononi mwake.

b. CDM ioneshe kuwa matatizo mengi ya madini nanishati yamejengwa kutokana na sera na sheria ambazo zilipitishwa na Mkapa.

c. CDM ioneshe vile vile jinsi kiongozi huyo huyo alivyoendelea kawaida ya kubeba na kubebana na kutolea mifano watumbalimbali. Ikumbukwe pamoja na yote yanayosifiwa kuhusu Mkapa bado leohii tunavuna mavuno ya uongozi wake.

d. CDM ioneshe kuwa mojawapo ya mambo ya ubaguzi wa rangi nchini kufanywa na wanasiasa yalifanywa wakati wautawala wake kuhusiana na Salim na jinsi gani yeye Mkapa kama kiongozi aliyelelewa na Nyerere alishindwa kuwazuia wale waliokuwa nakiu ya madaraka hadi kutupatia viongozi wa sasa. Kwa kifupi ioneshe kuwa viongozi wanaopigiwa debe na Mkapa ni utangulizi wa ufisadi!

e. CDM ioneshe kuwa CCM ilikuwa na nafasi nzuri ya kuonesha imeamua kweli kujivua gamba lakini yale yaliyotokea leo hii huko Arumeru na hasa kuhusishwa kwa BWM kunaonesha tu kuwa gamba limegoma na sasa limeganda na gamba likiganda linakuwa donda! Wapo baadhi ya watu wazuri sana ambao CCM ingewez akuwatumia lakini kwenda kumtumia mfalme wa magamba ni kosa kubwa la kimkakati!
Tumekusikia tumekufikia.
 
Back
Top Bottom