Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Mojawapo ya vitu ambavyo labda vitahitaji majibu baadaye ni kwa vipi CDM wakati wa uzinduzi wao hawakumgusa kwa uzito unaotosha aliyekuwa Rais wa Tanzania wakati matukio mazito ya ufisadi yanatokea yaani B. W. Mkapa. Katika thread hii mengi yamejadiliwa kumuhusu Mkapa: MKAPA ABOVE THE LAW? Chama cha Demokrasia na Maendeleo kilitambua kuhusika kwa Mkapa katika maamuzi ya kifisadi kiasi cha kumuweka namba 10 katika ile "Orodha ya Aibu" akiwa miongoni mwa kina Ballali, Rostam, Lowassa n.k. Katika maelezo ya orodha hii ilisemwa hivi:
Hiyo ni sehemu kidogo tu kwani baadaye tumeweza kuona mengi sana yaliyotokea wakati wake kama Rais na hasa wakati wa mwaka wake wa mwisho. Ikumbukwe ndiye aliyewakingia kina Ballali, Rostam na wengine. Ninajiuliza maswali yafuatayo:
a. CDM inamhofia au kumheshimu Mkapa kiasi kwamba yawezekana hakiamini kabisa kuwa anahusiana na ufisadi mkubwa kabisa uliowahi kutolewa nahivyo wananchi hawapaswi kukumbushwa?
b. CDM inaamini kuwa Mkapa hagusiki kwa vile Rais Kikwete alisema "muacheni mzee wetu astaafu" wakati hataki kustaafu anapenda kujihusisha na siasa? Kama anajiingiza kwenye siasa kwanini yeye mwenyewe naye aliyoyafanya yasiwe issue kwa Watanzania?
c. CDM inafikiria kwa mfano atakaposimama leo kuzungumza huko Arumeru Mkapa atawaonesha huruma wapinzani na viongozi wao? Hivi akizungumza na kuwabeza wapinzani na kuwaita majina ya ajabu ajabu na kuwafanya duni viongozi wao atakuwa amewaonea au anafanya kile kinachotegemewa kama mwanasiasa wa CCM? Kama yeye hatowaheshimu - tayari kwa kukubali kushiriki kampeni hizi ameonakana hajali sana mambo ya upinzani - kwanini wao wanafikiria kumheshimu katika hili?
Nini cha kufanya basi?
a. CDM ioneshe kuwa CCM inamtumia mmoja wa viongozi waliosimika mfumo wa utawala wa kifisadi nchini mtu ambaye ana damu ya Watanzania mikononi mwake.
b. CDM ioneshe kuwa matatizo mengi ya madini nanishati yamejengwa kutokana na sera na sheria ambazo zilipitishwa na Mkapa.
c. CDM ioneshe vile vile jinsi kiongozi huyo huyo alivyoendelea kawaida ya kubeba na kubebana na kutolea mifano watumbalimbali. Ikumbukwe pamoja na yote yanayosifiwa kuhusu Mkapa bado leohii tunavuna mavuno ya uongozi wake.
d. CDM ioneshe kuwa mojawapo ya mambo ya ubaguzi wa rangi nchini kufanywa na wanasiasa yalifanywa wakati wautawala wake kuhusiana na Salim na jinsi gani yeye Mkapa kama kiongozi aliyelelewa na Nyerere alishindwa kuwazuia wale waliokuwa nakiu ya madaraka hadi kutupatia viongozi wa sasa. Kwa kifupi ioneshe kuwa viongozi wanaopigiwa debe na Mkapa ni utangulizi wa ufisadi!
e. CDM ioneshe kuwa CCM ilikuwa na nafasi nzuri ya kuonesha imeamua kweli kujivua gamba lakini yale yaliyotokea leo hii huko Arumeru na hasa kuhusishwa kwa BWM kunaonesha tu kuwa gamba limegoma na sasa limeganda na gamba likiganda linakuwa donda! Wapo baadhi ya watu wazuri sana ambao CCM ingewez akuwatumia lakini kwenda kumtumia mfalme wa magamba ni kosa kubwa la kimkakati!
CDM isiposhambulia pasipo huruma CCM na sera zake, isipoonesha kuwa matatizo yanayowakabili watu wa Arumeru (na sehemu nyingine nchini) yanatokana na kushindwa kwa sera za CCM (siyo kutekelezwa tu bali kushindwa in substance) basi itajikuta inaletwa karibu na kilele nakuachwa hewani! CDM ni lazima ichore mstari, iwagawe wananchi na kuwachochea wananchi kugawanyika kifikra. Pasipo kugawa fikra, hawatagawa kura!
Orodha ya Mafisadi (List of Shame)A. USHIRIKI WA MOJA KWA MOJA KATIKA VITENDO VYA UFISADI
10. BENJAMIN WILLIAM MKAPA
Benjamin William Mkapa alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia mwaka 1995 hadi 2005 alipomaliza kipindi chake cha pili. Ufisadi wote ulioelezewa katika waraka huu ulitokea wakati wa utawala wa Rais Mkapa na anawajibika nao moja kwa moja ama kwa kuubariki au kwa kuunyamazia. Zaidi ya hayo, kuna ushahidi unaoonyesha kwamba wakati akiwa madarakani Rais Mkapa alishiriki moja kwa moja au kwa kutumia ndugu na/au washirika wa karibu wa familia yake katika ufisadi mkubwa na uliolipotezea taifa fedha nyingi. Kwa mfano, wakati akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mkapa alitumia wadhifa huo kuhakikisha kwamba kampuni iitwayo Tanpower Resources Limited inamilikishwa asilimia 85 ya hisa za kampuni ya Kiwira Coal Mines Ltd. inayochimba mkaa wa mawe huko Kiwira Mkoani Mbeya. Hisa zilizobaki asilimia 15 zinamilikiwa na Serikali. Tanpower Resources Ltd. ni kampuni iliyoanzishwa kwa ajili ya kuinuifaisha familia ya Rais Mkapa na washirika wake wa karibu. Taarifa za BRELA zinazonyesha kwamba wakurugenzi wa Tanpower Resources Ltd. ni Anna Mkapa, mkewe Rais Mkapa, Nicholas Mkapa, mtoto wa Rais, Bwana Joseph Mbuna, wakili wa kujitegemea na baba mkwe wa Nicholas Mkapa, Daniel Yona, Waziri wa Nishati na Madini wakati wa utawala wa Rais na bwana Joesph Mapundi. Baada ya Tanpower Resources Ltd. kutwaa umiliki wa Kiwira Coal Mines Ltd. kwa nguvu za Ikulu ya Rais Mkapa, iliingia mkataba na Shirika la Ugavi wa Umeme nchini TANESCO wa kujenga mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia mkaa wa mawe na kuiuzia umeme TANESCO. Mkataba huo utainufaisha kampuni ya Kiwira Coal Mines Ltd., na kwa hiyo Rais Mkapa, familia na washirika wake wa karibu kwa kiasi cha dola za Marekani milioni 271 kwa wakati wote wa mkataba.