NALETA UCHUMI UNAOPAA: Jakaya Mrisho Kikwete

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Mar 8, 2010
7,269
675
Haya ndo maneno ya Jakaya Mrisho Kikwete Dec 2005 mpaka sasa hakuna cha maana mpaka uchumi umelegalega.

Mtu anaweza kujiuliza je Jakaya Mrisho kikwete kajikwaa wapi?

Uchumi Unaopaa
Mheshimiwa Spika:
Baada ya mafanikio ya Awamu ya Tatu, haitarajiwi kuwa Serikali ya Awamu ya Nne italegeza kamba na kupuuza misingi iliyotuletea mafanikio tunayojivunia. Najua mengi yamesemwa na watu wanaodai wanamfahamu Jakaya Mrisho Kikwete na jinsi atakavyolegeza mambo. Napenda kuwahakikishieni kuwa watu hao wamepotea sana.

Wakati wa kampeni wapo baadhi ya wapinzani waliothubutu, kwa kukosa shukrani, kusema ati Serikali ya Awamu ya Tatu ilikuwa inatekeleza sera zinazobuniwa Washington. Serikali ya Awamu ya Nne haitaogopa kubuni na kutekeleza sera na mikakati ya maslahi kwa ukuaji wa uchumi na maisha bora kwa kila Mtanzania ati kwa vile zinaungwa mkono au kufadhiliwa na nchi tajiri na mashirika ya fedha ya kimataifa.Hatutafanya lolote lisilo na maslahi kwa taifa letu kwa kuwaogopa au kutaka kujipendekeza kwa wakubwa hao. Lakini vile vile hatutaacha kufanya lolote la maslahi kwa taifa na Watanzania kwa vile tu linaenda sambamba na ushauri wa mashirika ya fedha ya kimataifa. Hatutafanya maamuzi kwa kutaka kupendwa; lakini tutafanya kila maamuzi kwa kigezo cha msingi cha maendeleo na maslahi ya taifa.

Mheshimiwa Spika:
Mbali ya kusukumwa na hoja ya kukuza uchumi haraka ili kupiga vita umaskini, tunasukumwa pia na ukweli wa nguvu za utandawazi na ushindani mkubwa katika masoko ya kanda na ya kimataifa. Hivyo basi, sote tuunganishe nguvu zetu ili tuongeze uzalishaji, tuongeze uwekezaji, tuongeze mauzo nje, tuongeze ubora wa mazao na huduma zetu na tuongeze kasi ya ukuaji wa uchumi wetu ili upae. Hakuna kurudi nyuma. Kasi mpya inayozungumziwa ni ya kusonga mbele na siyo kuserereka na kurudi nyuma kwa kasi.

Update: source http://www.jkikwete.com/speechz.php?id=767
 
Nanukuu hii: Hakuna kurudi nyuma. Kasi mpya inayozungumziwa ni ya kusonga mbele na siyo kuserereka na kurudi nyuma kwa kasi.

Bahati mbaya sana: KASI INAYOONEKANA NI YA KUTUMBUKIA CHINI YA USAWA WA BAHARI

My take: Kashikwa pabaya ??? Siamini hata kidogo kwamba JK ana nia mbaya na nchi hii. Agenda zake nzuri zimeendelea kukwaa visiki tu, licha ya madaraka na uwezo wote alio nao kama Rais wa JMT. Alianza vizuri tu 2005. HUJUMA zilianza muda mfupi tu baadae. Sina uhakika na hili kwa hiyo tafadhali msinihukumu, ila niseme, wapo waliotishika na kasi ya mabadiliko aliyoanza kuleta kwani muda mfupi baadae complications zilianza kuibuka kila kona. Yaliyomo leo ni matokeo ya hayo ninayofikiria kama hujuma dhidi ya Urais wake. Wanaoumia ni maskini wa Tanzania. Nani hataki mafanikio ya wa Urais wa JK?? Kina nani hao?
 
Ratiba ilivurugika kwa vile brain behind ilikuwa Lowasa na labda angekuwepo kungekuwa na mabadiliko. Walizidisha uroho
 
Hapo kwenye Red ni kwamba umejihujumu mwenyewe maana mambo mengi anayosema yamemshinda
 
Inasikitisha sana kwa Mkuu wa Nchi kukosa uelekeo na uchumi wa Taifa letu kuzidi kudidimia kwani hata jana alisikika akisema kuwa kila ahadi aliyotoa itatekelezwa kwani ahadi zote ziko kwenye maandishi.
 
Nanukuu hii: Hakuna kurudi nyuma. Kasi mpya inayozungumziwa ni ya kusonga mbele na siyo kuserereka na kurudi nyuma kwa kasi.

Bahati mbaya sana: KASI INAYOONEKANA NI YA KUTUMBUKIA CHINI YA USAWA WA BAHARI

My take: Kashikwa pabaya ??? Siamini hata kidogo kwamba JK ana nia mbaya na nchi hii. Agenda zake nzuri zimeendelea kukwaa visiki tu, licha ya madaraka na uwezo wote alio nao kama Rais wa JMT. Alianza vizuri tu 2005. HUJUMA zilianza muda mfupi tu baadae. Sina uhakika na hili kwa hiyo tafadhali msinihukumu, ila niseme, wapo waliotishika na kasi ya mabadiliko aliyoanza kuleta kwani muda mfupi baadae complications zilianza kuibuka kila kona. Yaliyomo leo ni matokeo ya hayo ninayofikiria kama hujuma dhidi ya Urais wake. Wanaoumia ni maskini wa Tanzania. Nani hataki mafanikio ya wa Urais wa JK?? Kina nani hao?

Kwa mtazamo kama huu, inaelekea na wewe pia ulirogwa na Yahya kabla hajafa!!
 
Mnamsingizia hajawai toa speech kama hii!
Ninyi ni waongo wazandiki na wapenda umaarufu!
Na kwa taarit=fa yenu alishasema kelele za mlango hazimnyimi usinginzi!
 
Nilikuwa nafikiri ni ahadi mpya maana kwa ahadi hajambo!Halafu ahadi hewa!
 
Nanukuu hii: Hakuna kurudi nyuma. Kasi mpya inayozungumziwa ni ya kusonga mbele na siyo kuserereka na kurudi nyuma kwa kasi.

Bahati mbaya sana: KASI INAYOONEKANA NI YA KUTUMBUKIA CHINI YA USAWA WA BAHARI

My take: Kashikwa pabaya ??? Siamini hata kidogo kwamba JK ana nia mbaya na nchi hii. Agenda zake nzuri zimeendelea kukwaa visiki tu, licha ya madaraka na uwezo wote alio nao kama Rais wa JMT. Alianza vizuri tu 2005. HUJUMA zilianza muda mfupi tu baadae. Sina uhakika na hili kwa hiyo tafadhali msinihukumu, ila niseme, wapo waliotishika na kasi ya mabadiliko aliyoanza kuleta kwani muda mfupi baadae complications zilianza kuibuka kila kona. Yaliyomo leo ni matokeo ya hayo ninayofikiria kama hujuma dhidi ya Urais wake. Wanaoumia ni maskini wa Tanzania. Nani hataki mafanikio ya wa Urais wa JK?? Kina nani hao?
NI kwamba JK hana uwezo wa uongozi. Na hili jambo akina Mangula waliliona mapema kabisa na wakafanya atempt ya kumnyima form ya kugombea urais huyu. Mwinyi ndo aliyetupeleka hapa tulipo. Watanzania tuache unafiki. Mwinyi ni tatizo hapa. Maana yeye ndiye aliyemlazimisha Mangula ampe JK form ya kugombea Urais. Hizi ni habari nilizozipata toka ndani kabisa ya system.
 
Inasikitisha sana kwa Mkuu wa Nchi kukosa uelekeo na uchumi wa Taifa letu kuzidi kudidimia kwani hata jana alisikika akisema kuwa kila ahadi aliyotoa itatekelezwa kwani ahadi zote ziko kwenye maandishi.

Nimewaza sana hivi ni kitu gani kunamsumbua Mkuu, manake suala la kuwepo kwenye makaratasi ni tofauti kabisa na utekelezaji wake ilitakiwa atueleze ahadi alizozitoa zinazokaribia Tsh.90 Trilion, huku bajeti nzima ya nchi ikiwa ni Tsh 12 Trilioni vilevile tukikusanya nusu ya bajeti nyingine tukitegemea misaada, kwa hesabu za haraka haraka ni miaka 7 fedha zote za bajeti zielekezwe kwenye Ahadi tu ili zitimizwe..,hizo fedha nyingine atatazitoa wapi na katika muda gani manake anamaliza ngwe yake miaka minne kasoro ijayo...Hapa ndipo tunaposema ashakum si matusi huu ni usanii tu
 
Ratiba ilivurugika kwa vile brain behind ilikuwa Lowasa na labda angekuwepo kungekuwa na mabadiliko. Walizidisha uroho

Jamani kwani huyo EL ndo peke yake mwenye ubongo kati ya Wa-Tanzania milioni 40? Angalau ningeshawishika kusikia kwamba kuna genge linaloweza fananishwa ma MAFIA, a society of sorts set out to make sure that Tanzania does not rise up to the surface. This implies, external forces aided by our own blood and kin, sucking up to them, their white masters again. same as elsewhere in Africa where there is abundance of riches. Am I paranoid?
 
NI kwamba JK hana uwezo wa uongozi. Na hili jambo akina Mangula waliliona mapema kabisa na wakafanya atempt ya kumnyima form ya kugombea urais huyu. Mwinyi ndo aliyetupeleka hapa tulipo. Watanzania tuache unafiki. Mwinyi ni tatizo hapa. Maana yeye ndiye aliyemlazimisha Mangula ampe JK form ya kugombea Urais. Hizi ni habari nilizozipata toka ndani kabisa ya system.

Na mwinyi ndie aliyemkataza Shein hasigombee maana Shein pia alitaka kujitosa; Lakini Mangula alimuogopea nini Mwinyi kilaza yule? hapa ndipo nashindwa kuelewa nini kilikuwa kinaendelea nyuma ya Pazia maana pia wanasema Mkapa alikuwa ajijui siku hizo na kuwa hata hotuba aliyotowa dodoma aliambiwa kuwa ndio aliyoongea akashangaa sana inasemekana Mkapa aliyekuwa ana hutubia CC na NEC ya CCM kabla ya kupiga kura alikuwa ni jini la Yahya maajabu sana hapa Afrika.
 
Nimewaza sana hivi ni kitu gani kunamsumbua Mkuu, manake suala la kuwepo kwenye makaratasi ni tofauti kabisa na utekelezaji wake ilitakiwa atueleze ahadi alizozitoa zinazokaribia Tsh.90 Trilion, huku bajeti nzima ya nchi ikiwa ni Tsh 12 Trilioni vilevile tukikusanya nusu ya bajeti nyingine tukitegemea misaada, kwa hesabu za haraka haraka ni miaka 7 fedha zote za bajeti zielekezwe kwenye Ahadi tu ili zitimizwe..,hizo fedha nyingine atatazitoa wapi na katika muda gani manake anamaliza ngwe yake miaka minne kasoro ijayo...Hapa ndipo tunaposema ashakum si matusi huu ni usanii tu

Ahadi zingine alitowa kwaniaba ya Rais ajae; kwahiyo Rais anayekuja hana haja ya kutoa ahadi zilishatolewa na Kikwete yeye ni kutekeleza tu!
 
Back
Top Bottom