Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,985
- 20,263
Wadau wa JF,
Kama kichwa cha uzi huu nilivyokieleza, hiyo ndiyo dhamira yangu ya dhati.
Nikiwa muhafidhina wa siasa za kisasa na zenye ukwasi wa muono wa juu, nimekuwa muhanga wa kusikia na pengine kuona kwa vitendo harakati zinavyopamba moto ndani ya chama mufilisi cha ccm za kuwania kupeperusha bendera ya kijani na njano kwenye uchaguzi wa 2015.
Wanaotajwa au kujionyesha wazi kwa mienendo yao kuutaka uraisi ni wengi lakini kinara wao ni Waziri Mkuu aliyejiuzuru kwa aibu ya karne baada ya kuthibitika na tume huru iliyoundwa na Bunge la Tz kuwa alihusika kuliingiza Taifa katika hasara kubwa ya mabilioni kwa kuipa kampuni ya mfukoni na isiyonasifa ya Richmond tenda ya uzalishaji wa umeme.
Lakini wanaoitwa waangalizi wa siasa na sheria za nchi hii walisema kuwa ushahidi wa tume hii hauna nguvu ya kumtia mtu hatiani mpaka wenye mamlaka ya dola wajiridhishe.
Baada ya kuwekwa kando kimamlaka, Bwana Lowasa alianza kujiumba kwa simenti ya iron still ndani ya chama na sasa anajongea mbele ya siasa za kitaifa tena akibeba kundi la wapumbavu na werevu wanaosumbuliwa na njaa za msimu!
Yeye kama Lowasa hajatangaza mahali popote iwe ndani ya chama au nje kuwa atagombe urais 2015 lakini mtazamo wangu wa siasa za kiafrika unaniambia kwa mwenendo wa Lowasa kwa sasa ni kuwa anaitaka dola kwa gharama yoyote ile na hata kwa damu!
Hilo tu linanipa nguvu ya kumwangalia Lowasa kama mwanasiasa aliyefutika katika siasa kwa uozo wake na sasa anaefufuka kwanjia KHARAMU.
Watanzania wenzangu tukubali tukatae, ukweli ni kuwa kuelekea uchaguzi mkuu 2015 taifa linahitaji mtu makini na msafi wa nje na ndani kisiasa.
Japo kuwa ndani ccm hakuna aliyemsafi hata chembe, lakini vivyo hivyo wanatofautiana kwa uchafu.
Sasa naomba mtu yeyote mwenye ushahidi wa wazi zaidi ya ule wa Mwakyembe juu ya ufisadi au uhujumu uchumi wa Lowasa,Membe,Sita,na wengine wanaotajwa kuwania urais ndani ya ccm aushushe hapa,
Ushahidi huo uwe unajitosheleza kumfikisha mahakamani muhusika, na kwakuepuka matumizi ya rushwa, atapelekwa katika mahakama ya kimataifa, iwe Afrika au nje ya Afrika!
Kama hana hatia basi na asafishwe ili ifikapo 2015 awe mweupe kama nyota chini ya bendera ya ccm!
Tunataka ifikapo 2015 taifa liwe na wagombea wa vyama vya siasa walio wasafi na wasio na doa kisia kama ilivyo kwa chama cha ukombozi wa pili dhidi ya mkoloni mweusi ccm, na si kingine ni Chadema chini ya Daktari na gwiji wa siasa za kisayansi W.P.Slaa!
Uwanja wa siasa utakuwa mzuri ikiwa wagombea wote wa vyama vya siasa watakuwa wasafi kama Dr Sla,Mbowe,na wengine wengi ndani ya Chadema!
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki CHADEMA, Mungu ilaani CCM ife kamili kabla ya 2015.