"Nakupenda sana Jack Pemba, SIYO SIRI!"

WomanOfSubstance

JF-Expert Member
May 30, 2008
5,457
956
Najua mtakapoona kichwa cha thread mtashangaa kulikoni tena WoS!

Ndio hivyo tena. Wikiendi ndo inanukianukia.. Hebu nianze kuangalia viwanja gani vinafaa kwenda kutembelea ili kupunguza msongo na kujipa burudani baada ya kazi ngumu ya wiki nzima.

Njia moja wapo ya kurelax ni muziki.. tena muziki wa nyumbani.. Kuna akina Akudo Impact wazee wa masauti, kuna FM Academia wazee wa Pamba Bling bling... Kuna Vibration sounds.....HAAA!

Lakini mbona kuna kitu kinanikuna kuhusu hizi bendi --- athira ya DRC! Haijalishi lakini maana ninachotaka ni burudani.. Sauti nzuri, upigaji mzuri, wanamuziki watanashati, stage performance nzuri ......MHHHH....

Nyimbo nzuri??? Sina uhakika kwa hilo maana maneno mengine humo ndani.. Sijui kama patna wangu wa muziki anajisikiaje yanapoimbwa na mimi kushabikia... JACK PEEEMBA.. MUME WANGU.... NAKUPENDA SANA EHHHHH JACK PEMBA!!!

Wakaka hebu tuambieni.. Mnajisikiaje kwenye hili?

HAYA tuache hayo ya Kumpenda Mume wa wenyewe Jack Pemba,
Kuna ma PDG huimbwa mwanzo hadi mwisho... Tena wenye wasifu wa kutiliwa mashaka! Kina Papa Msofe, Ndama Mtoto wa Ng'ombe, n.k.

Hivi wanaimbwa ili iweje? Kuwapa umaarufu kwa jipi jema wanalofanyia jamii ya watanzania?

MAKUBWA HAYA!
 
They pay kuimbwa so it comes as no surprise. Hata Dotnata alitoa hela kuimbwa na FM Academia na aka shitiki kwenye video ya mwimbo.
 
Last edited:
They pay kuibwa so it comes as no surprise. Hata Dotnata alitoa hela kuibwa na FM Academia na aka shitiki kwenye video ya mwimbo.

Naomba ufafanuzi hapa ina maana ili uimbwe unatoa pesa? Mmmhh jamani na hawa nao wanataka kuimbwa ili wapate nini?mbona sijawahi kusikia mchango wa hawa watu kwenye jamii? au ni kutafuta tu umaarufu usiokuwa na maana?
 
Asante MwanaF1,
Sasa ndugu yangu..hivi hat akama ndio kutoa hela uimbwe... najua hizi bendi zinamilikiwa na watu wenye kuheshimika katika jamii - Akudo kwa mfano nasikia kuna Waziri mmoja anaimiliki... hapo hapo bendi inatukuza wahalifu..inakuwaje hii?Ni ujumbe gani unaifikia jamii - hii connection au unholly alliance kati ya Kiongozi mmiliki, wanamziki na wahalifu
 
Mchango wa wengi wao ni uhalifu ndugu yangu!
 
Naomba ufafanuzi hapa ina maana ili uimbwe unatoa pesa? Mmmhh jamani na hawa nao wanataka kuimbwa ili wapate nini?mbona sijawahi kusikia mchango wa hawa watu kwenye jamii? au ni kutafuta tu umaarufu usiokuwa na maana?

Unatoa mkwanja hata wewe Msindima una paishwa kwenda juu.
 
Asante MwanaF1,
Sasa ndugu yangu..hivi hat akama ndio kutoa hela uimbwe... najua hizi bendi zinamilikiwa na watu wenye kuheshimika katika jamii - Akudo kwa mfano nasikia kuna Waziri mmoja anaimiliki... hapo hapo bendi inatukuza wahalifu..inakuwaje hii?Ni ujumbe gani unaifikia jamii - hii connection au unholly alliance kati ya Kiongozi mmiliki, wanamziki na wahalifu

Njaa dada angu. Wewe una fikiria kwa nini ni rahisi kuawala na kudanganya watu masikini? Ni aibu tupu.
 
Siyo siri... napenda sana wimbo wa Safari siyo Kifo wa Akudo - lakini maneno yake huwa yananifanya nishangae kidogo... yaani wanaume wazima wanamsifia mwanaume mwenzao Jack Pemba mwanzo hadi mwisho!
Atakuwa kawalipa kiasi gani?
 
Tukirudi kwenye mfano wa Dotnata, I'm not sure but if memory serves me right alisema aliwapa FM $100 kumpaisha.
 
Pesa kama hizi zinaingia kwenye mfuko wa bendi au mtunzi au inakuwaje?

Now that is the question even I want the answer to. Maana kama ni kwa mmiliki bendi zina tengeneza pesa nzuri so it doesn't make sense wao kutaka vijihela hivyo na kama ni wanamuziki je mabosi wao wana waruhusu?
 
Unatoa mkwanja hata wewe Msindima una paishwa kwenda juu.

Nionavyo ulimbukeni wa maisha na kupenda sifa zisizo na mpango ndivyo vinavyowasumbua,kuliko kutoa pesa uimbwe si bora hiyo pesa wakawape yatima,tuna mayatima na wajane wangapi ambao wanahitaji misaada wetu?

hapo unaweza-kuta yeye anatoa pesa ili aimbwe lakini wapo ndugu zake wana shida na hata hatoi msaada kwa ndugu zake kuwasaidia.
 
Mkuu si unajua wabongo? Ana hiari atoe mamilioni kwenye harusi ili aonekane ila mtu huyo huyo mfuate kumuomba msaada kimya kimya kama ata kupa.
 
Kazi kweli kweli,sasa tunafanyaje kwenye hili swala maana kidogo huwa napata shida unaimbwa ili? Na wakati huna mchango wowote kwenye jamii tena mtu huyu utakuta hana msaada hata kwenye jamii inayomzunguka,nakumbuka miaka ya nyuma niliwahi kusikia wakimtaja kwenye hizo nyimba zao jamaa mmoja kwa jina MKARABATI,hivi huyu nae alikuwa na mchango gani kwenye jamii?
 
Lakini WOS cha kukumbusha Jack Pemba hivi sasa amefulia totaly mpaka anaona aibu kutoka alikuwa anamzalau mdogo wake sasa yupo TBT pale aibu kafulia.
 
Kazi kweli kweli,sasa tunafanyaje kwenye hili swala maana kidogo huwa napata shida unaimbwa ili? Na wakati huna mchango wowote kwenye jamii tena mtu huyu utakuta hana msaada hata kwenye jamii inayomzunguka,nakumbuka miaka ya nyuma niliwahi kusikia wakimtaja kwenye hizo nyimba zao jamaa mmoja kwa jina MKARABATI,hivi huyu nae alikuwa na mchango gani kwenye jamii?

Ni kweli mkuu yani hamna maana yoyote. Si hata baadhi ya vipindi vya radio haswa radio kama clouds uta sikia kipindi kizima mtu ana taja majina tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom