Nakumbuka...

Mentor

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
20,328
23,879
...NAKUMBUKA...

Psalm 37:25 “I was young and now I am old, yet I have never seen the righteous forsaken or their children begging bread.”​

…IDM Mzumbe…

Nakumbuka enzi za Mwalimu! Wakati huo tukisoma ADCA (Advanced Diploma in Certified Accounting). Elimu ilikuwa nzuri, chuo kilikuwa kikiheshimika. Tulikuwa tukila vyakula vizuri sana; chai ya maziwa, mayai, siagi, jam, mikate, karanga, chakula mboga saba na kikikosekana kimoja tu, tunagoma.

Ghafla vikaanza kupungua kimoja kimoja. Zilianza jam, siagi, karanga, maziwa. Hayati baba wa taifa, Mwalimu J. K. Nyerere akasimama akalihutubia taifa akasema, “Tufunge mikanda” adui alikuwa ametuvamia na hatukuwa na budi kuhamisha rasilimali nyingine kwenda kwenye vita. Mpaka leo, na bahati mbaya amefariki, hatujaambiwa tufungue mikanda.

Nilimfahamu binti mmoja, maji ya kunde, mfupi, mwenye uzuri wa asili. Nikisema uzuri wa asili namaamisha kuwa hata nywele, kucha, na kujipamba kwake kulikuwa kwa kawaida kabisa hivyo ni rahisi kuuona urembo wake wa asili.

Tulimaliza chuo na yeye kwenda kufanya kazi Morogoro, kwenye kiwanda cha ngozi, Morogoro Tanneries kama mhasibu.

Viwanda vilikuwa vingi kipindi hiki. Viwanda hivi vya ngozi kwa wakati huo vilikuwa vitatu tu; Morogoro, Mwanza na Kilimanjaro. Hiki cha Kilimanjaro kilikuwa ndicho kiwanda cha kwanza kabisa cha ngozi nandiyo maana kiliitwa Tanzania Tanneries.

Kulikuwa na kiwanda binafsi cha ngozi pia mkoani Kilimanjaro, Himo Tanneries. Sikumbuki kilikuwa ni cha nani, na hadi leo bado kipo ingawa hivi vingine vyote – vya serikali – vilikwisha kufa.

Kazi ilikuwa nzuri na alikuwa mwaminifu sana kazini hata ilipotokea nafasi ya kwenda IFM kusoma Post Graduate Diploma ya Uhasibu kwa mwaka mmoja, yeye alichaguliwa kwenda. Ilikuwa ni kawaida ofisini kusikia tukiambiwa, “mbona hamjitumi kama huyu dada jamani?

Akiwa huko ilikuwa ni jambo la kawaida sana wanafunzi kuchanga na kununua mitihani. Alikuwa na hofu ya Mungu. Hakutaka kushiriki katika hilo. Wenzake walimcheka na kumdhikahi na kumuambia, “Utafeli wewe!” Alijiwazia moyoni mwake, “Sina cha kupoteza. Cha maana sana hapa nasoma ili nipate notes za kufanya mitihani ya bodi ya NBAA.

Mwaka mmoja si mrefu, hatimaye muda wa mitihani ukafika.

Alikuwa anafahamu sana somo la Financial Management. Ila somo la Accounting lilikuwa likimpiga chenga. Wakati tunasoma Mzumbe, tulifundishwa kwa kutumia mfumo wa Muingereza ilhali masomo ya huko IFM yalikuwa kwa mfumo wa Mmarekani.

Nakumbukua mfano mmoja. Alikuwa akichanganywa na maneno haya, “accounts receivable and accounts payable”. Hakujua yalikuwa sawa tu na kusema “debtors and creditors.”

Siku kadhaa kabla ya mtihani wa mwisho walimletea maswali ya Financial Management awasaidie na aliwasaidia kuyafanya. Alikasirika sana alipoingia kwenye mtihani na kukuta maswali yaleyale. Aliamini kweli walinunua mitihani.

Kwa bahati mbaya, hakupata mtu wa kumfundisha Accounting maana kila mtu alikuwa na majibu tayari, hakukuwa na haja ya kusoma tena. Waliendelea kumkejeli kuwa atafeli. Alirudi chumbani kwake akamkuta mwenzake akifanya maswali yao ya kununua, alikuwa ni mja mzito. Mwenzake akamwambia, “toa hela wewe upewe mtihani, utafeli!” Akamjibu, “tena ninaomba nifeli ili niwaoneshe Mungu wangu ninayemtegemea ni wa namna gani.

Matokeo yalipotoka alifeli mtihani ule wa Accounting hivyo alirudi kazini Morogoro bila cheti.

Kazini kwake walimsimanga na baadhi waliopata kusikia alichofanya huko walimkejeli kuwa amekataa kununua mtihani akakosa cheti.

Baada ya miaka michache, binti yule aliolewa na kuhamia mkoani Kilimanjaro kumfuata mumewe. Alitoka kuishi kwenye nyumba ya hadhi ya juu huko Kingalu, Morogoro hadi kwenye nyumba ya kupanga Moshi. Nyumba isiyo na hata ceiling board, choo cha nje cha shimo. Kwa bahati nzuri, Moshi nako kulikuwa na kiwanda cha ngozi hivyo aliendelea na kazi kwenye kiwanda hicho hicho.

Wakati wote huu aliendelea kushikilia msimamo wake wa uaminifu na hofu kwa Mungu. Wengi walimcheka kwani wakati ule ilikuwa rahisi kwa wahasibu kuiba bila kugundulika kirahisi. Walimkuta na kumuacha - kiuchumi. Lakini yeye hilo halikumghasi usingizi.

Huku nyumbani hali ya maisha ilikuwa ya kawaida sana. Kwa nyakati zile familia zetu hizi, ukienda shule unakuwa ndiyo tegemeo la ukoo mzima. Ndugu wa mume na wa kwako wote watakuja kwako kuomba msaada. Kwa hofu ya Mungu waliyokuwa nayo, hawakuweza kumfukuza mtu. Hii ndiyo iliyofanya, pamoja na kupata mishahara ‘nafuu’ haikuwa ikiwatosha. Iliwalazimu kuwalisha watoto mchicha kila siku na maziwa nusu lita kwa watoto wawili. Nakumbuka kuna kipindi watoto walifikia hadi kuharisha.

Siku moja mhasibu mkuu alimwita ofisini kwake akamwambia, “Wewe binti nataka nikupe dili! Hapa nimepiga milioni 20 kutoka kwenye OC sasa wewe kwa kuwa hutaki rushwa na ulokole wako hata nikikupa pesa utakataa, basi nenda shule mimi nitakulipia.

Yule binti aliuliza maswali mengi juu ya fedha zile na kwamba atagundulika lakini mhasibu mkuu alimthibitishia kuwa hilo halimhusu, yeye aende shule na kwamba atalipiwa na ofisi. Wakati ule sehemu pekee kwa kanda hii iliyokuwa inatoa masomo ya kujiandaa na mitihani ya CPA kilikuwa ni chuo kipya cha IAA, Arusha. Alikubali akaenda.

Wakati huo binti huyu ni mama wa watoto wawili. Alisoma kwa bidii masomo yake yale ya kujiandaa. Kipindi kile CPA ilikua ikitolewa kwa awamu mbili; CPA 1 na CPA 2. Binti huyu alifanya mitihani minne kati ya sita ya CPA 1 na kufaulu yote. Hata hivyo hakuruhusiwa kuendelea na sehemu ya pili bila kufanya kwanza mitihani ile miwili na kupita, enzi hizo walisema ‘ku-clear’.

Alienda hadi ofisini kwa mwenyekiti wa bodi ya wahasibu (NBAA) na kumuomba aruhusiwe kufanya mitihani yote kwa wakati mmoja. Mwenyekiti alimkatalia ila baada ya kumsumbua sana alikubali ila akamtaka aandike barua ya kujifunga kuwa kama atafeli mtihani wa sehemu ya kwanza kati ya ile miwili aliyobakiza, hata kama atapita ile ya sehemu ya pili basi hataruhusiwa kuhesabika amefaulu, akakubali.

Alirudi kusoma tena kujiandaa na mtanange wa pili. Wakati huo huo alikuwa na uja uzito wa mtoto wa tatu. Alidhamiria kusoma hivyo hivyo na kumaliza kwa wakati.

Alienda tena kuripoti chuoni Arusha na mkuu wa chuo alipomwona na jinsi alivyodhamiria, alimwonea huruma na kumwambia atafute tu dada wa kumsaidia kazi. Hivyo aliendelea kusoma hadi akajifungua. Alikula yeye na dada wa kazi kwa ada ile ile moja hadi anamaliza chuo.

Wakati anasoma, aliona masomo marahisi maana alikuwa bado na notes za kipindi kile akiwa IFM kwenye kozi aliyofeli kwa kuwa alikataa kununua mtihani. Wakati huo alielewa tayari kilichokuwa kikimtatiza kwenye Accounting. Alikuwa vizuri zaidi kwenye Finance maana ndiyo kazi hasa aliyokuwa akiifanya kazini kwake.

Wakati anakaribia kujiandikisha kufanya mtihani, mwanaye alikuwa mgonjwa. Mkuu wa chuo alimshauri asijiandikishe kufanya mtihani kwani aliona jinsi alivyojituma asingependa kumuona akifeli wakati yeye alifahamu ana uwezo mkubwa. Hakumsikiliza, alijiandikisha hivyohivyo.

Mkuu wa chuo bado hakukata tamaa, alijua akimzuia kufanya mitihani hatajaziwa matokeo yoyote walau atakuja kufanya mitihani wakati mwingine. Binti yule alikuwa na mawazo mengine tofauti kabisa, “Mungu wangu nimekutegemea wewe tangu utoto wangu, ninakutegemea wewe hata sasa!” aliomba.

Wakati wa mitihani, mkuu wa chuo alikuwa akiingia chumba cha mitihani na kukagua ambapo alijiridhisha hayupo. Kumbe! Binti alikuwa amejificha na pindi tu mkuu wa chuo anapotoka ukumbini yeye alikimbia na kuingia ndani ya chumba cha mtihani na kuendelea. Alijitahidi kuingia kabla nusu saa hazijaisha baada ya mtihani kuanza. Mitihani sita, mkuu wa chuo alikuwa akiingia na kukagua. Mitihani sita alikuwa akijificha na kuingia baada ya mkuu wa chuo kutoka. Hatimaye alimaliza mitihani yake.

Baada ya mitihani alirudi nyumbani na kazini kuendelea kulea watoto na kulitumikia taifa. Hakujua linaloendela hadi siku mtoto wake wa tatu alipoamka anaumwa. Ametokwa na jasho kali na ana joto mwili mzima. Aliharakisha kwenda hospitali ambapo mtoto alilazwa.

Asubuhi ya siku iliyofuata, alichanganyikiwa alipomuona mumewe anakuja na tabasamu kisha anamuambia, “hongera D”. Hakuelewa hadi alipomuambia kuwa amepigiwa simu na rafiki zake na kumuambia kuwa ame ‘clear’. Hakuamini!

Alilia huku akiwaza kwa nini rafiki zake walimfanyia vile. Hawakujua yuko hospitali na mtoto halafu wanamtania na kumdanganya tena kupitia kwa mumewe kuwa amefaulu masomo yote? Haiwezekani! Watu huwa hawafaulu CPA kirahisi hivyo. Alijua lazima kuna somo atakuwa alishindwa ku-clear. Hakuhitaji kusumbuka sana ili kuthibitisha hilo kwani mumewe alimuahidi kwenda hadi Dar es salaam kwenye bodi ya NBAA kumuangalizia matokeo.

Mumewe alipofika alilakiwa na msururu na kelele za watu kila mmoja akisema la kwake. Wengine wakilia, wengine wakilia na kucheka maana wamefaulu baadhi na kufeli baadhi. Wengine walikuwa wakiulizana, ‘huyu mwanamke ni nani?’

Alisogea hadi kwenye mbao ya matangazo na kuanza kutafuta jina la mkewe. He he he, ni kama ulijua, alianza kutafuta chini kuelekea juu. Baadaye akagundua yamepangwa kwa alfabeti. Alipeleka macho mahali alipojua jina la mkewe litakuwepo. Hakuliona, haikuwa kazi rahisi kuamini, kwani mahali ambapo palikuwa – au palipotakiwa kuwa – na jina la mkewe palikuwa na alama za michoro ya kalamu mpaka jina hilo halikuonekana.

Alijongea hadi ofisini na baada ya kujieleza alishangaa anapewa hongera na kuulizwa huyo binti yuko wapi? Aliwaeleza yupo hospitali Moshi. Alirudi na furaha kuliko ile ya mwanzo na kumueleza kuwa alikuwa amefaulu masomo yote aliyokuwa amefanya.

Na kama hiyo haitoshi, kati ya watahiniwa 77, ni watahiniwa 3 TU waliopita masomo yote bila kurudia na kati ya hao watatu basi wa kike ni yeye pekee. Aliyemaliza chuo miaka 10 kabla ya kufanya mitihani hiyo. Mumewe alitembea kifua mbele kama vile yeye ndiye aliyepata hiyo CPA (T)!

Baada ya wiki moja binti yule alirudi kazini na kuendelea na majukumu yake kama kawaida.

Nakumbuka siku moja asubuhi na mapema, akiwa nyumbani kwake bado kwenda ofisini, alishtushwa na mlio mkali wa honi ambapo alipotoka nje alikuta gari aina ya land cruiser nyeupe na mbaba mfupi, mweupe akiwa ameliegemea.

Hujambo binti?” alimsalimia. Na binti aliitikia salamu ile na kuijibu kwa heshima aliyostahili. “Wewe ndiye mrs. **** mwenye CPA?” aliendelea kuongea mzee yule. “Je, unajua kufundisha?

Bila kujijua alichokuwa akikijibu, alikubali. Binti aliambiwa aandike barua ya kuomba kazi na mwezi mmoja tu baadaye alipata kazi katika chuo kimoja hapo Moshi akiwa mmoja kati ya walimu wanne tu - kwa wakati huo - wenye CPA.

Walihama kutoka kwenye nyumba isiyokuwa na ceiling board kwenda kwenye nyumba yenye vyumba vitatu vya kulala na mengine mengi.

Nakumbuka akiulizwa, “Unajiona ukifika wapi?” naye akajibu, “Mungu anajua…

Nakumbuka…

Nakumbuka…

Wasalaam wapendwa,

Mentor.
 
Nashindwa hata niandike nini ila nimeelewa somo, gud job Brother
 
Mmmh hujui tu ulivyonitia nguvu.... "Sijawahi ona mwenye haki ameachwa".

Utapitia magumu mengi, unaweza kupoteza vingi, but Mungu hatokuacha kamwe. Na baada ya yote hayo kwisha, Mungu atakurejeshea enzi yako, na mamlaka yako, na kila kitu chako ambacho mwovu alikuibia kitarudishwa maradufu . Kuwa mwaminifu kwa Mungu katika hali zote si kazi ndogo (mfano kwa Ayubu), but thawabu yake ni kubwa mnooo

" Nami Nitawarejeshea hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu na tunutu". Yoeli 2: 25
 
Mzeee wa kuzingua
 
Back
Top Bottom