Nakumbuka: Part II

Mentor nitajitahidi kuja kesho kuchangia hii maana inanigusa maana nalea vijana ambao wamechipukia na namshukuru Mungu pamoja na kuwa mama yao mdogo wanakuja kunieleza juu ya mahusiano yao. Kifupi ni kwamba hakuna jibu la moja kwa moja au jibu sahihi. Na mara nyingi haliwezi fanya kazi kwa watu wote wakati wote. Na hata mshauri wa mambo ya ndoa mkubwa unayemfahamu naye ana matatizo ktk ndoa yake. Hivyo hakuna jibu kamala hesabu. Maisha hayako fair, na mahusiano hayako fair zaidi. Binadamu hawezi kuwa mkamilifu, hivyo kama hakuna kuchukuliana mizigo hakuna mahusiano kamwe. Be content, jiamini na muamini Mungu na mpende mwenzio. Amini Mungu kuruhusu chochote kutokea ktk maisha yako, anajua you can handle it na amekupa enough grace to take uou through. Majaribu LAZIMA YAJE. Tafuta wimbo wa The Martins ...This is the promise.
hayo ya Mentor tuweke pembeni!
hili la kukumiss hakiiiii naumwaaaaaaa!
 
hayo ya Mentor tuweke pembeni!
hili la kukumiss hakiiiii naumwaaaaaaa!

Unajua mwalimu uache utani..niko bize hapa nasubiria busara from you!!

Imbombo ngafu, kuna wanaoichukulia kiimani zaidi na kuna wanaoitetea kimwili zaidi.

either way mtazamo wangu ni lazima kuwe na mfuatano wa mambo katika kuangalia compatibility. Na kwa njia yoyote ile (kiimani au kimwili) physiological compatibility ni muhimu and foremost kuliko physical compatibility.

Lazima ujue kuwa hiyo sexual compatibility (ni ya muhimu sawa) lakini inatumika zaidi kwa miaka michache ya ndoa kuliko kuwa na mwenza ambaye mna nia mamoja, ni rafiki yako, you can be happy with, etc etc...maana sex 'the act' is a moment of a few minutes...than life itself!!!!
 
Unajua mwalimu uache utani..niko bize hapa nasubiria busara from you!!



either way mtazamo wangu ni lazima kuwe na mfuatano wa mambo katika kuangalia compatibility. Na kwa njia yoyote ile (kiimani au kimwili) physiological compatibility ni muhimu and foremost kuliko physical compatibility.

Lazima ujue kuwa hiyo sexual compatibility (ni ya muhimu sawa) lakini inatumika zaidi kwa miaka michache ya ndoa kuliko kuwa na mwenza ambaye mna nia mamoja, ni rafiki yako, you can be happy with, etc etc...maana sex 'the act' is a moment of a few minutes...than life itself!!!!
Hii kitu hii!!!
 
hayo ya Mentor tuweke pembeni!
hili la kukumiss hakiiiii naumwaaaaaaa!
yaani I don't see any seriousness in you my, you know where to get me. I guess utakuwa unaumwa nywele. Jokes aside, what are cooking maana umekua adimu kuliko pesa za rushwa.
 
NAKUMBUKA



Genesis 2:24 “Therefore a man leaves his father and his mother and cleaves to his wife, and they become one flesh.

Kijijini...1961


Nakumbuka enzi za mwalimu! Ndiyo kwanza tulikuwa tumepata uhuru nami ndiyo nilikuwa najiunga na darasa la kwanza. Hayakuwa maisha marahisi kwani pamoja na kubahatika kwenda shule bado kulikuwa na majukumu mengi nyumbani.



Kabla ya kutoka nyumbani ni lazima ukamue ng’ombe, utoe samadi na kuwalisha ng’ombe na mifugo yote mliyonayo kisha uondoke nusu saa kabla ili kufika shule.

Shule ilikuwa mbali na nyumbani kiasi kwamba nyakati za mvua mara nyingi tulishawishika kutoroka shule. Kwa bahati mbaya tangu nikiwa darasa la nne nilikuwa mtunza stoo ya shule hivyo kunifanya nishindwe kutega au kutoroka shule.

Sitosahau siku madaftari yangu yalipodumbukia mtoni wakati nikienda shule. Mvua ilikuwa ikinyesha hivyo njia ilikuwa ikiteleza hasa ukizingatia hatukuwa tukivaa viatu. Nilifika kwenye daraja ambalo lilikuwa ni mbao moja ndefu nyembamba. Kutokana na waliopita awali kutolea matope kwenye mbao ile sikujua hasa upana wake hivyo kujikuta nimekanyaga sehemu yenye tope na kuteleza. Nilibahatika kujishika mwenyewe na bahati mbaya kuyaachia madaftari yangu na yakaangukia mtoni. Sijawahi kulia maishani mwangu kama siku ile.

Ukitoka shule unafikia kukata kuni kwa ajili ya kupikia ikiwa ni pamoja na kupika chakula cha jioni kama ni zamu yako au kwenda kukata majani au kukamua na kulisha ng’ombe kutegemea na zamu yako. Ulikuwa na bahati kama mlizaliwa wengi.

Nakumbuka tulikuwa tukibeba mahindi ya kukaanga tunayafunga vyema kwenye jani la mgomba kisha tunaenda kuyaweka pembeni ya mto ambapo maji hayapiti mengi. Basi saa nne – muda wa mapumziko – utaona kila mtoto akikimbia kuelekea kunako mto. Mahindi yale yanakuwa yamekwisha kulainika na yanakuwa matamu sana.

Safari moja ikaanzisha nyingine nami nikachaguliwa kwenda shule ya upili. Maisha yalikuwa ya dhiki ingawa kwa kipindi kile tuliona sawa tu. Ni bahati kuchaguliwa kujiunga na shule ya upili maana watu walichaguliwa kulingana na idadi ya shule zilizokuwepo kwani waliofaulu walikuwa wengi kuliko shule zilizokuwepo.

Tulijitahidi kusoma sana tuwapo shule maana wakati wa likizo tulikwenda nyumbani kwetu na wazazi hawakuelewa wakikuona unashika kitabu. Ungeweza kusoma usiku kama kuna mbalamwezi kwani wasingeruhusu umalize mafuta ya taa kusoma magazeti (baba yangu alikuwa akiita madaftari yangu magazeti).

Nilibahatika kufaulu vizuri na kuchaguliwa kwenda kusoma shule ya upili ya Azania kwa ajili ya kidato cha tano na sita.

Azania Sekondari, Dar es salaam


Kutoka kijiji nilichozaliwa, ni vijana watatu tu ambao tulibahatika kufikia ngazi hii na kutoka shule niliyotoka ni vijana 10 tu tulioweza kuchagulia kuendelea na masomo. Nilijiapiza kutokuipoteza nafasi ile. Ndiyo nilikuwa na akili lakini pia nilitambua kuwa wengi wa waliobaki walikuwa sawa na mimi ila uhaba wa shule ndio uliofanya wao wabaki na mimi niendelee.

Ni wakati wa vipindi vya UKWATA ambapo tuliungana na shule ya jirani ya Jangwani.

Nilimuona binti!

Alikuwa ni wale wadada viongozi wa UKWATA na kwaya na hakuna jinsi ungeweza kumweleza lolote kuhusu mahusiano akakukisiliza, lakini alikuwa mzuri, ukweli na usemwe.

Nilijitahidi tukazoeana na ilibidi niridhike na cheo nilichopewa cha ‘kaka’. Kwa kuwa pia tulikuwa tumetokea mkoa mmoja mimi ndiye nilikuwa nikiwasindikiza kwenda mjini au sehemu nyingine nje ya shule ili wasipate shida. Kwa kipindi kile niliridhika na kufanya yote hayo ili tu niwe karibu na dada huyu. Sikuwahi kuwa na mahusiano yoyote na binti wa kike hasa ukizingatia malezi yetu nyumbani na kanisani.

Nilikuwa na suruali moja tu – ukiacha sare ya shule – ambayo ndiyo nilikuwa nikiivaa tunapoenda mjini au kwenye matukio yoyote nje ya shule, na shati langu lekundu lakini nilijitahidi sana kuwa msafi. Nilikuwa nikizifua kila ninapotoka kwenye mizunguko kisha kuzikunja vyema na kuziweka chini ya godoro langu hadi wakati mwingine wa mtoko.

Maisha yalienda haraka na miaka miwili iliisha na kumaliza elimu yangu ya sekondari.

Kipindi hiki ulitakiwa kwenda JKT kwa mwaka mmoja kisha mwaka mwingine ufanye kazi ndipo uende chuo kikuu. Nilipangiwa Kambi ya Makutupora, Dodoma.

Kutokana na kufanya kazi nyingi nilipokuwa nyumbani, kijijini, nilipata wakati mwepesi sana nilipokuwa kambini hapo kwani walipotaka fundi waashi nilikuwepo, wajenzi, kazi zote za mikono na hata Sanaa nilikuwepo. Hivyo mara nyingi watu wawapo kwenye gwaride au kazi za ‘mahovyohovyo’ mimi nilikuwa bize napaka rangi Ikulu ya Chamwino.

Tulikuwa pia tukifanya kazi binafsi kwenye nyumba za maafande hivyo kuweza kupata kipato cha ziada ingawa nakumbuka bado tulikuwa tukipewa fedha tulipokuwa kambini.

Nilimuona binti!

Huyu alikuwa binti wa ‘saa-meja’ yaani RSM wa kambi yetu ya Makutopora. Alikuwa kidato cha tano kipindi kile ila alikuwa mrembo sana. Alikuwa akisoma shule ya kutwa.

Tulionana siku ambayo nilikuwa nikirekebisha mfumo wa umeme nyumbani kwao ambapo alitoka shuleni na kunikuta sebuleni peke yangu. Tulisalimiana kwa aibu – yeye kwa kuwa ni binti wa kike na mimi kwa sababu ya uzuri wake, aisee kalikuwa karembo kweli kweli na kalikuwa kameanza kujipodoa basi kalikuwa kanang’aa kweli kweli. Ingawa alikuwa ndiyo ametoka shule lakini alikuwa msafi utadhani alikuwa ndiyo anaenda, na sketi yake ya marinda, daah nakumbuka vyema.

Tuliendelea kuonana mara kwa mara kwa kuwa mara nyingi kama tulikuwa tunaenda kufanya kazi kambini ni lazima tukapige ripoti kwa RSM kisha atupeleke. Jambo moja nililompendea RSM ni hakuwa akichukua pesa zetu, alitupa fedha zote kama tulivyopatana na afande tuliyemsaidia kazi yake – alikuwa mzee mmoja mwaminifu sana.

Nakumbuka RSM alikuwa akitamka maneno ambayo yalikuwa yakituchekesha sana, “Kila mtu avae green vesti ya kijani!” mara nyingi alikuwa akitumarisha kabla hatujaenda kambini.

Maisha yalienda haraka na tulikaribia kumaliza mafunzo yetu na kurudi kijijini kwetu. Ni wazo hili ovu lililonifanya kuruka hatua kwani nilihisi baada ya mimi kuondoka sitokuja tena kukutana na binti yule mtoto wa RSM. Nilijisemea moyoni, japo tu ‘nimuonje’ walau hata nikiondoka basi nisiwe nimekosa vyote.

Hivyo wiki za mwisho za mafunzo nilijitahidi kuongeza ukaribu na yeye na kumuonesha nilikuwa nikimpenda kweli. Ilikuwa muhimu kwangu kumuonesha nampenda kwani ingerahisisha uongo/ushawishi wangu kuwa ili kuonesha kuwa naye ananipenda basi anipe ‘salome’ wake.

Sitaelezea kwa kina lakini ilikuwa ni siku ya passing-out na kwa kuwa mimi nilikuwa mtu wa kukaba chaka – ingawa nilikuwa vyema kwenye vitengo vyote vya kijeshi - sikuwepo kwenye gwaride la kufunga mafunzo ambapo baba yake alikuwa ndiye RSM wa gwaride…

Baada ya mwaka mmoja wa JKT nilichaguliwa kuendelea na kozi ya JKT. Hivyo nilibaki kambini pale na kuendeleza mahusiano yangu na binti huyu ambapo tuliahidiana mengi sana hasa atakapomaliza shule. Tulipanga akimaliza shule tukajitambulishe kwa wazazi wetu na kwamba wakiridhia basi nimuoe kabisa.

Tuliingia kwenye uhusiano wetu kwa kupitia mlango usio lakini kwa kulazimisha tulifunga –nilifunga – macho na kuendelea. Kumbe mwenzangu hakufurahishwa na jinsi tulivyoanza uhusiano wetu. Hivyo wakati mimi namaliza mwaka mmoja wa kuwa JKT nikiwa sasa Lance Koplo, alihitimisha mahusiano yetu.

Ingawa niliumia sana kwani nilikuwa nikimpenda alinirahisishia maamuzi yangu juu ya maisha yangu. Tulikuwa tumeahidiwa kuwa tutapelekwa shule na Jeshi kama tukiridhia kubaki. Kutokana na maumivu niliyokuwa nayo niliamua kutokuendelea na Jeshi na kwenda Chuo Kikuu.

Chuo Kikuu cha Dar es salaam

Nilifika chuoni nikiwa fedha za kutosha hivyo ukiongezea na kwamba tulikuwa tukipewa kila kitu maisha yangu yalikuwa nafuu kuliko wenzetu wengi.

Sasa nilikuwa na suruali na mashati ya kutosha kubadilisha na nilikuwa sasa kijana barobaro kweli kweli.

Kwa muda nilisahau nilikotoka na kuendekeza anasa za mjini. Ingawa nilikuwa nikienda bado kwenye vipindi vya dini lakini dhamira yangu haikuwa kamili. Room mate wangu hasa alichangia mimi kwenda kwenye vipindi hivyo ingawa yeye alikwenda kwa nia moja tu. Watu walikuwa wakituita mapacha watuonapo ingawa mioyoni tulijua jinsi ambavyo tabia zetu zilikuwa kama Kaskazi na kusi…nakumbuka sana nikimpiga ‘exile’.

Ukitukuta kwenye vipindi utasema hawa ndio vijana wa Bwana. Tulikuwa tukikaa mbele wakati wote. Kuna kipindi wadada ilibidi watuulize, “Jamani nyie kina kaka, ina maana hamtuoni?” Tulipowauliza kwanini walisema hivyo walijibu, “Yani nyie mkija mnakaa mbele tu na mkipiga makofi mnaangalia juu tu.

Itoshe kusema nilifanya mengi yasiyopendeza. Kwa kipindi kile nilisingizia kuumizwa na mtoto wa RSM hivyo sikuona umuhimu wa kuwa na mahusiano ya kudumu. Sikuwa na hofu ya kuchelewa kuoa au kukosa mtu wa kumuoa kwani nyumbani wazazi walikuwa wamenichagulia binti wa kumuoa.

Ingawa sikuwa nikimpenda lakini nilijua yupo tu. Kwa bahati mbaya alikuwa ni kati ya wale watatu tuliofaulu kwenye sekondari na baada ya hapo alikwenda shule ya ualimu na kurudi kufundisha shule ya msingi pale kijijini.

Nakumbuka nikiwa mwaka wa mwisho nilikutana na binti mmoja aliyekuwa ndiyo kwanza anaanza mwaka wake wa kwanza wa masomo. Huyu alinivutia kwanza kwa umbo lake matata lakini kadri nilivyozidi kumfahamu niligundua hata tabia yake ya ndani ilikuwa ya kuridhisha japo kwa kuanzia.

Sikumlazia damu nikaona japo nijaribu huenda akawa ndiye. Kama kawaida yangu ya kutokuwa na uvumilivu, naye pia nilitumia mlango usio sahihi kuanza naye mahusiano.

Mahusiano yetu yalikuwa na kwa kiasi room mate wangu alipumua maana alikuwa amezoea kukutana na wadada tofauti tofauti chumbani.

Ni hadi wakati nilipokaribia kumaliza masomo yangu ndipo binti huyu alipoanza mikasa yake naye. Sikujua shida hasa ni nini lakini kidogo kidogo alianza kubadilika. Sikugundua hili mapema nikajitahidi kuvumilia.

Siku moja, Jumapili moja.

Baada ya kutoka kanisani nilirudi chumbani kwangu na baada ya kufanya usafi na maandalizi madogo madogo nlielekea chumbani cha rafiki yangu huyu. Mwenzake wanayeishi naye chumbani alikuwa amekwenda kuwasalimia wazazi wake maana yeye kwa bahati nzuri alikuwa mwenyeji wa jijini hapa.

Baada ya kuandaa chai tulikaa tukinywa huku tukiongea haya na yale kuhusu maisha na masomo. Baadaye tulikubaliana tutoke tukatembee na kupata chakula cha mchana nje kisha ndipo turudi.

Kabla ya kutoka nakumbuka alikuja rafiki yake kipenzi ambaye walitoka naye kijiji kimoja. Baada ya salamu alimwambia kuwa kaka yake alikuwa amekuja kumtembelea na alitaka aje kumuona. Tulimjulisha kuwa kwa kuwa tunashuka chini basi tutapitia chumbani kwake kumsalimia.

Tulitoka kwenda kutembea na kisha kurudi baadaye jioni. Ilikuwa ni siku njema ambayo haikustahili kuisha jinsi ilivyoisha.

Nakumbuka akitoa nguo zake ambazo alipanga kuzivaa kesho yake darasani huku akilalamika gauni lake alipendalo lilikuwa limefumuka kwa pembeni. Wakati akinieleza hayo, rafiki yake yule alirudi tena na kumuita nje.

Baada ya maongezi yao mafupi alirudi ndani na kuniambia kuwa kaka yake amelalamika kuwa tumemchomesha mahindi kutusubiri (kumsubiri) na hakwenda.

Nikamuuliza kama alimwambia kuwa tulipitia kwake wakati tunakwenda na hata wakati tunarudi na hawakuwepo. Akanijibu ‘ndiyo’. Hivyo nikamwambia akae atulie maana si makosa yake.

Baada ya dakika chache tena mlango wake uligongwa na akatoka nje kuongea na mgeni mpya ambaye sikumjua kwa kipindi hicho.

Kwa kuwa nilibaki ndani peke yangu nilijihisi mpweke hivyo kutaka kujiweka busy nilichukua uzi na sindano na kuanza kurudishia sehmu ile iliyofumuka ya gauni lake. Haikuwa kazi rahisi maana lilikuwa gauni lile la utelezi lenye layer nyingine kama mbili ndani.

Ni hadi aliporudi ndani ndipo nilipogundua kuwa alikuwa ametoka kwa zaidi ya dakika 50. Sikuwa nimewaza lolote baya hadi nilipomtazama machoni. Sikuhitaji kuuliza sana ili kugundua alikotoka hakukuwa na jema lolote. Hata hivyo nlikuwa mpole kijana wa kiume wa Kimachame mimi na kumsikiliza.

Ningelikuwa sijasoma, au Mkurya (sina maana mbaya) basi ile siku ingekuwa mbaya sana kwake.

Mwaka mmoja baadaye…

Nikiwa sina hili wala lile nikuwa nikisoma kitabu cha I Married You – Walter Trobisch.

***nanukuu***


SEX IS NO TEST OF LOVE



If a couple want to use the sex act in order to know whether they love each other, one has to ask them:


“Do you love each other so little?”




If both of them think: “Tonight we must have sex - otherwise my partner will think that I don't love him or that he does not love me,” the fear of a possible failure is sufficient to prevent the success of the experiment. Sex is no test of love, for it is precisely the very thing that one wants to test which is destroyed by the testing.


Try to observe yourself when you go to sleep. Either you observe yourself, then you don't fall asleep. Or you fall asleep, and then you haven't observed yourself. The same is true about sex as a test of love. Either you test, then you don't love. Or you love, then you don't test. For its own sake, love needs to wait with its physical expression until it can be included in the dynamism of the triangle.


This waiting is usually harder for the young man than for the girl. Therefore, the girl has to help the young man here, who, because of his natural impetuousness, is more tempted to aim short of the goal. The first help she can give him is to learn how to say 'no' without wounding, how to refuse without breaking off. This is an art.



***mwisho wa kunukuu***



Kwa majonzi nilijiona mimi. Jinsi nilivyojitahidi kuingia kwenye mahusiano mengi kwa kupitia mlango usio sahihi. Nikaelewa kuwa kumbe si makosa yao yaliyofanya tuachane au makosa yangu...lakini ni kwa kuwa tulikosea msingi wa kuingilia.



Nakumbuka nikimfuata pacha wangu ambaye kwa bahati tulikuwa wote tukifanya kazi sehemu moja na kumueleza nilichokisoma na kwamba nilikuwa na nia ya kubadilika.

Alikuwa na furaha kuliko maelezo na sikujua sababu hadi aliponyanyuka na kuingia chumbani ambapo alitoka na bahasha ambayo ilikwisha kufunguliwa.

Ilikuwa imeandikwa majina yetu mawili.

Niliifungua na kuanza kuisoma kimya kimya;




S.L. P. **,

Morogoro.




Kaka Mentor,


Nakusalimu kwa jina la Bwana wetu mpendwa Yesu Kristo.

Ni matumaini yangu kuwa unaendelea vyema na kumtumikia Bwana katika maisha yako.

Nimefurahi kupata barua yako ambayo uliniandikia ingawa nilichelewa kuipata kwani nilihama kazi. Kwa sasa nipo mjini Morogoro. Ingawa ni zaidi ya mwaka tangu uniandikie nitajitahidi kukujibu kama Roho atakavyoniongoza.


*


*


*


*

Pamoja na kukujibu barua yako nilipenda kukufahamisha kuwa mwezi wa tisa tutakuja Dar es salaam kwa ajili ya semina fupi. Nitafurahi kama tutapata nafasi ya kuonana.

Wako katika Upendo,


Yule wa Jangwani Sec.


1 Wakorintho 6:20


Ingawa barua ile haikuwa na maneno yoyote ya mapenzi lakini ilinifanya nimkasirikie sana rafiki yangu kwa nini hakuinipa barua ile awali kwani ilionesha yeye aliipata miezi miwili kabla na ule ulikuwa mwezi wa nane, yaani mwezi mmoja tu kabla hawajaja.

Alinisihi nikae chini anielezee na aliniambia ni kutokana na tabia yangu mbaya aliyokuwa akiifahamu iliyomfanya asinipe barua ile na kama si kuja kumueleza mabadiliko yangu alipanga kutonipa kabisa barua ile.

Alinieleza aliumia alipowaza kuwa nitamharibia maisha binti yule (maana alimfahamu pia tangu tukiwa sekondari) akaona njia pekee ni kutokunipa barua ile.

Ilinibidi niwe mpole kwa maelezo yale na kugundua kumbe nilikuwa najinyima fursa mwenyewe.


Septemba 21, 2016

Itoshe kusema kuwa sasa mimi ni baba wa watoto watatu na leo imenikumbusha siku ile Ijumaa ya Septemba 21, 1984 nilipokaa na shemeji yenu na kuongea kwa kina kuhusu mustakabali wa maisha yetu na mwaka mmoja baadaye kufunga pingu za maisha.

Bado nakumbuka…





Wasalaam wapendwa,


Mentor.

MKUU SAMAHANI UNA UMRI GANI?
 
Unajua mwalimu uache utani..niko bize hapa nasubiria busara from yo

either way mtazamo wangu ni lazima kuwe na mfuatano wa mambo katika kuangalia compatibility. Na kwa njia yoyote ile (kiimani au kimwili) physiological compatibility ni muhimu and foremost kuliko physical compatibility.

Lazima ujue kuwa hiyo sexual compatibility (ni ya muhimu sawa) lakini inatumika zaidi kwa miaka michache ya ndoa kuliko kuwa na mwenza ambaye mna nia mamoja, ni rafiki yako, you can be happy with, etc etc...maana sex 'the act' is a moment of a few minutes...than life itself!!!!
hujaacha kuwa na akili nyingi Mentor ,hakiiii hujaaacha!
na hii tu unajua ndo sababu nakupenda.
 
yaani I don't see any seriousness in you my, you know where to get me. I guess utakuwa unaumwa nywele. Jokes aside, what are cooking maana umekua adimu kuliko pesa za rushwa.
nionee huruma!
A lot had happen hakiii,nionee huruma tu kuhusu pa kukupata!
hakyamama nakumiss mpk dah!
na huku JF sijui walinitangazia NOTE OF POPOTE ALIPO AKIONEKANA MKAMATENI!
PLS usiniwie mkali!
 
Back
Top Bottom