Nakumatt opens USD 1.3 million supermarket in Moshi, Arusha branch forthcoming

@Komandoo umesema ukweli unaouma. Ila watz hata tukiunganisha nguvu uaminifu hamna. Angalia kilichotokea NICO ambapo tulitegemea walau wawe chachu ya kuunganisha nguvu baina yetu. Kwa kweli tutalia hadi siku ya kiama bila mafanikio. Nadhani Nakumatt watakuwa wapangaji pale inapojengwa complex ya AICC kwa kushirikiana na LAPF. Na kama hilo litatolea utakuwa ndio mwisho wa shoprite Arusha kutokana na business location kuwa-favour NAKUMATT. Poor TZ!
 
Ajira ndio hizo tumeshapigwa bao, basi hata tuwe suppliers of fresh produce kama mboga mboga, mayai nk. Pia iwe chachu ya ushindani kwa bidhaa zetu (super brands) kushindana na za wenzetu kwa ku stock bidhaa zetu huko Nakumatt. Bado tuna safari ndefu mpaka tutoke kwenye usingizi wa kibiashara.
 
Wapi Imalaseko?
 
mkuu siunaona machezo wanayopiga wabongo pale mlimani city.. ukitaka receipt 45,000/= bila receipt 32,000/= ... ikitoka nje gari imevunjwa kioo mlinzi yupo pembeni unamuuliza anakujibu sio kazi yangu kulinda magari. Wizi tz umeanza kutoka mlinzi wa getini mpk _________. Tujirekebishe watanzania na haka katabia

Bwana Lameck usemayo ni kweli. Pale Mlimani city kwenye maduka makubwa ni deal kwa kwenda mbele! Unapatana kama unavyopatana na machinga usiogope bei wala nini! Wewe mfuate mhudumu yeyote na onyesha kwamba unataka deal basi kitu cha million 2 utauziwa million 1 na receipt inatolewa na jamaa unampa cha juu kama kilo moja hivi anagawana na jamaa wa ndani.

Mkuu nchi hii ni ya madeal kuanzia mlinzi hadi______________. Kwa hiyo ngoma drooo! Kila mtu ni fisadi tu ila ufisadi unatofautiana kwa kiwango cha kima!
 
naomba wakenya waje tena waanzisha mall yao ishindane na ile ya mlimani city. Pale mlimani city uswahili ,wizi vimezidi sana ,watu hawathamini kazi zao
 
Watanzania tunapenda sana kulalamika, binafsi ninapenda sana Wakenya walivyo firm on issues, very aggressive, with good customer care. Na hawa jamaa wa NAKUMATT nawajua vizuri, wako mbele ya Customer Care, (kuna kitu inaitwa Customer Experience). Nadhani ujio wao utakuwa na Positive Demonstrational Effect kwa wazawa (watanzania) kwani kila wakiambiwa kwa maneno wabadilike wanakuja juu, sasa ni wakati wa kuona na kujifunza kwa vitendo.
Karibuni Tanzania
 
Wapi Imalaseko?

Hapana mkuu namaanisha Nakumatt. Imalaseko asipokubali kubadili corporate strategy kuendana na soko hili la retail market, basi ajue ndio kampuni inaelekea kufa. Akubali kuongeza mtaji, kwa kuongeza wanahisa, management ichaguliwe kwa kuzingatia merits and experience na siyo kuweka family members.
 
Watanzania tunapenda sana kulalamika, binafsi ninapenda sana Wakenya walivyo firm on issues, very aggressive, with good customer care. Na hawa jamaa wa NAKUMATT nawajua vizuri, wako mbele ya Customer Care, (kuna kitu inaitwa Customer Experience). Nadhani ujio wao utakuwa na Positive Demonstrational Effect kwa wazawa (watanzania) kwani kila wakiambiwa kwa maneno wabadilike wanakuja juu, sasa ni wakati wa kuona na kujifunza kwa vitendo.
Karibuni Tanzania

Mkuu Si kwamba hakuna Watanzania wanao weza kuwahudumia wateja vizuri, no wapo tena wengi tu.

- Ukienda baadhi ya Minsupermarket za wabongo kuna customer care nzuri tu ingawa zingine ndo hivyo tena,

- Na tatizo la customer care kwa baadhi ya makampuni ya watanzania linasababishwa na mambo kama vile
1. Kuajiri ndugu- Mtu anaamua awajaze ndugu zake kwenye Hoteli, duka, basi nakazalika na wale ndugu wanakuwa ni full kiburi kwa sababu wanajua mali ni ya ndugu yao na hawatafanywa chochot

2. Kuweka Mke/mme/ Demu/Raifiki- Hawa wa wanachangia kwa kiasi kikubwa sana kuua biashara, Mtu anaamua amuweke mke wake ndo awe meneja kwenye biashara yake, mke hajui chochot zaidi ya kutumia nguvu kuendesha kamuni

3. Kupenda vutu cheap- Watanzania wanaajiri watu ni kweli lakini hakuna hata mmoja anaye wapa orientation ya kazi na hata atafute mtalaamu wa maswala ya masoko aje awapige msasa wafanya kazi wake.

SO WAPO WATANZANIA WENYE CUSTOMER CARE NZURI BUT TATIZO NI MTAJI HAWATAKI KUUNGANISHA MITAJI YAO.
 
@Komandoo umesema ukweli unaouma. Ila watz hata tukiunganisha nguvu uaminifu hamna. Angalia kilichotokea NICO ambapo tulitegemea walau wawe chachu ya kuunganisha nguvu baina yetu. Kwa kweli tutalia hadi siku ya kiama bila mafanikio. Nadhani Nakumatt watakuwa wapangaji pale inapojengwa complex ya AICC kwa kushirikiana na LAPF. Na kama hilo litatolea utakuwa ndio mwisho wa shoprite Arusha kutokana na business location kuwa-favour NAKUMATT. Poor TZ!

MKUU NI KWELI NICO IMEKUWA HIVYO TENA, ILA C KWAMBA NDO IWE SABABU YA WATU KUSHINDWA KUUNGANISHA NGUVU

Na kumbuka kwamba Tatizo la customer care Kwa Watanzania linasababishwa na kuendekeza vitu vifuatavyo
- Undugu kwenye biashara- Mtu anaajiri ndugu zake
- Mke/mme/demu na kazalika- hapa ndo kuna kuwaga na 0% customer care
- Kupenda vya rahisi/ ubahili, kukukosa elimu ya ujasirimali
Watu wanashindwa hata kutenga kiasi fulani cha mapato yao kuwaendeleza wafanya kazi wao kielimu

- ILA MKUU KUNA WATANZANIA WENGI TU WANA BIASHARA ZAO NA WANA CUSTOMER CARE NZURI SANA YA KUWEZA KUSHINDANA NA HAO WATU WA NJE, TATIZO NI NGUVU ZAO

- Tuna kosa nguvu za kimitaji, Hata ukiwa na customer care ya aina gani kama huna nguvu za kustosha you cant compete.

MKUU WA TANZANIA RAZIMA TUBADILIKE NA KUNA NJIA NYINGI TU ZA KUUNGANISHA MITAJI, KAMA

1. Ndugu kwa ndugu kuunganisha mitaji yao
2. Marafuki kuunganisha mitaji yao
3. Wafanya biashara

MFANO:

1. Kuna utitli wa makampuni ya Mabasi Tanzania, na ikija kampuni moja kutoka nje ya nguvu inazika zote hizi
Je makampuni kama 20 ya kijiunga pamoja Si ya tatatoa kampuni kubwa sana?

2. Vipi biashara ya DALADALA?
- Ina takiwa watu wajiunge waje na kampuni ya kueleweka na si kila mtu kutaka amiliki DALADALA LAKE

3. Vipi MAFUSO?
- Wakijiunga watu wa MAFUSO kama 10 hivi wanaweza kuja na kampuni ya kueleweka ya usafirishaji

4. Vipi wafugaji wa kuku? kuliko kila mtu atake kuwa na kuku wake 500 je wakijiunga watu kama watano si watakuja na kampuni ya ufugaji wa kuku iliyo enda shule?

5. Vipi wa MINISUPERMARKET?

6 Vipi wa Migahwa ya msosi?
 
Kama wenzenu wanaweza kuna dhambi gani ya ku-invest popote dunia hii? Mbona wachina wako kila kona hadi wauza mitumba hampigi kelele lakini jirani zenu wamepanua biashara yao hapa bongo basi kelele tu?
Sina kinyongo na Nakumat ama kampuni yoyote inapopanua biashara zake na inapowekeza popote dunia hii as long as they play by the rules.
Imalaseko imekuwa miaka yoooooteee hapa bongo sasa wako wapi? Wao ndio walitakiwa wawe wameshaenea nchi nzima, sasa wameshapigwa bao la kisigino. Kama customer service ya hawa Nakumat itakuwa nzuri basi wenye biashara zingine esp. banks hapa bongo kaeni chonjo na mtakufa kifo cha mende
 
mimi binafsi nafurahia kampuni ya nchi jirani ya kiafrika ikiwekeza hapa tz, ili mtu upate ajira kwenye duka kubwa kama hilo, pamoja mambo mengine kama elimu.mafunzo nk lakini uaminifu ni kigezo kikubwa kinachoangaliwa, na kwa watanzania hilo ndiyo tatizo kubwa,kama generali ulimwengu alivyodokeza tumekuwa wa nigeria wa eastern part of africa,tumekuwa watu wa voda fasta, mission town sitashangaa walinzi, cashiers,head of dept wote wakawa wakenya,kwasababu hakuna anayewekeza fedha zake akubali kufilisiwa na vibaka.
 
WAKUU, MIMI SIONI TATIZO KWA HAWA WAKENYA KUJA KUWEKEZA TANZANIA, TUJIULIZE

1. Kuna kampuni ya Tanzania imejaribu kwenda kuwekeza kenya ikazuiwa?

2. Watanzania Tutaendelea kuwafanyia kazi hao wakenya kwa sababu ya upumbavu wetu wenyewe, NITATOA MFANO WA KWENYE MAHOTELI, KUNA KAMPUNI MOJA INAYO MILIKI HOTELI KADHAA HUSUSANI KWENYE HIFADHI ZA SERENGETI, NA NGORONGORO,
1. Mwanzoni wafanya kazi karibia wote walikuwa Watanzania, kukaibuka vitu vifuatavyo
- WIZI WA VITU VYA HOTELI KAMA VILE GLAS, VIJIKO, MASHUKA, VIKOMBE NA KAZALIKA
- Kampuni ilikuwa inabidi kila mwezi wanunue vitu vya kureplace vilivyo potea katika mazingira ya kutatanisha,
- Kampuni baada ya kufanya uchunguzi na kuweka mitego walibaini kuna chein ya wizi ya kufa mtu, kuanzia kwa wafanya usafi, walinzi, wahudumu kwenye vyumba vya kulaa wageni, Baa na Hoelini
- Walijenga Chaini Huyu wa Baa akivusha glass basi na wewe wa kwenye room jitahidi uvushe mashuka na taulo il baadae wafany buter trade.
HAPA MNATEGEMEA NINI? KWA NINI WASIAJIRI WATU WA NJE?

- WATANZANIA TUTABAKI KULALAMA SANA MPAKA MWISHO WA DUNI

- NAKUMBUKA RAIS MSTAAFU MKAPA ALIWAHI KUSEMA" WATANZANIA BILA YA KUUNGANISHA MITAJI HATUTAWEZA KUSHINDANA NA MAKAMPUNI MAKUBWA YA NJE"

COME TO THE POINT, ALIKUWA ANAMAANISHA HAYA YAFUATAYO

1. Kila mtanzania anataka awe na FUSO lake mwenyewe la kubebea mizigo ya watu,
- Je utaweza kushindana na makampuni makubwa ya usafirishaji yatakayo kuja kuwekeza Tanzania?

2. Kila mtanzania anataka awe na Basi lake, awe Haice zake mwenyewe, awe na Tex zake mwenyewe, Awe na mashine ya kusaga nafaka
- Je yakaja makampunu makubwa na kuivest kwenye mabasi ya kubeba abilia ni nani ataweza kufurukuta?

3 Kila mtanzania anataka kuwa na Duka lake mtaani na kwingineko, kila mmoja

4. Kila mtanzania anawaza kuanzisha Min supermarket
- Hizi min Supermarket tunazo jivunia zitaweza kusimama kwa haya makampuni yenye mitaji ya kufa mtu?
- Tutaweza kushindana na Shoprite?
- Je tutawaweza NAKUMATT
- Tutawaweza UCHUMU SUPERMARKET?

- Watanzania Tutabali kulia, C jajua hapa Serikali ifanye nini, kwani hao wakenya wamepewa fedha na serilkali yao waje kufungua biashara Tanzania?
- Cheki kwenye mabenk, Je serikali inahusika vipi? Kenya comercial Benk walipewa fedha na Serikali yao waje kuwekeza Tanzania?

WATANZANIA KILA MTU AKITAKA AMILIKI, FUSO LAKE, MASHINE YA KUSAGA YA KWAKE, MIN SUPERMAKET YAKE, BASI LAKE NA KAZALIKA TUTAKUJA KULIA KILIO KILICHO KIKUU.

WATU WENGINE WANAAMUA KUUNGANISHA MITAJI YAO NA KUJA NA KAMPUNI MOJA YENYE NGUVU SISI HUKU NI KILA MTU ANATAKA AONEKANE ANAZO PESA HAIJARISHI ANAMILIKI NINI.

-YATAKUJA MAKAMPUNI MENGI SANA KUTOKA NJE WEEZA KWENYE USAFIRI WA MABASI TENA YA LUXURY NA BEI NAFUU SISI TUTABAKI KULAUMU SERIKALI

WATAKUJA WATAWEKEZA KWENYE UBEBAJI WA MIZIGO KWA UFANISI NA KWA BEI YA CHINI, SISI NA USANII WETU TUTABAKIA NA FUSO ZETU TUNAZO MILIKI KILA MTU

WATAFUNGUA SUPERMARKET KUBWA SANA, SISI TUTABAKIA NA MIN ZETU TUTAJIKUTA TUNAGEUKA KUWA WANUNUZI KWENY CAMPUNI ZETU WENYEWE

TUSIPO BADILIKA NA KUUNGANISHA MITAJI YETU HAKIKA TUTAKUJA KUJUTA, TUTAJIKUTA TUNA KUWA THE CONSUMER OF HIS/HER OWN GOODS AND SERVICES

Well written & said.
 
Hata kama tukijenga zetu, umeshashuhudia "customer services" zetu?

Yaani watu wanatka kazi, wakishaipata, maadili na uchapaji kazi unasahaulika mara moja!

Hii ni ktk kila sekta, benki, serikalini na hata walio na biashara zao, tuko tuko tu, mwenye duka, anaweza kuwa ameishia stock za bidhaa fulani, inaweza kumchukua wiki hata mwezi hadi atakapo nunua tena stock, anachekelea na kufurahia kabisa anapokujulisha kuwa kitu ukitakacho hakipo!

Wache wageni waje watufundishe adabu kidogo!

Hahahaa! lakn mkuu mbona Super Market nyingi zina wafanyakai wabongo? Kikubwa ni muajiri kuwa na misingi yake ambayo kila mfanyakazi ni SHARTI AITIMIZE na kuifuata ipasavyo!
 
bado tunasafari kubwa ya kuelimisha wafanyabiashara juu ya soko la hisa ...mi siamini kabisa kwamba sisi hatuna mtaji wa dola mil 1.4 au hata dola mil 10 ....imagine wafanyabiashara kama mohammed ent na bakhresa wakaanzisha supermarkets zao na kuuza bidhaa za kutoka viwandani mwao na tanzania ...sasa hata ukiwa na watu kama 10 tu ka hao industry itabadilika ..ndo maana wakenya wanatupiga bao
 
Watu wengi bado tunapenda kwenye masoko ya kawaida na maduka madogo na hii inatokana na unafuu wa bei.Bidhaa za supermarket ni bado anasa.
 
Jamani tusikimbie ukweli,

Tatizo sio uaminifu wa wafanyakazi kama watu wengi wanavyojaribu kuelezea maana hata hao Nakumatt na Uchumi kama ilivyo Shoprite, Games etc, etc kisheria bado watendelea kuajiri wabongo hao hao ukiondoa labda wafanyakazi wachache senior.

Pia tatizo sio mtaji kwa maana yapo makampuni mengi tu ya kibongo yenye mitaji mikubwa sana mpaka hata kuwekeza kwenye nchi za nje. Mfano angalia Bakhresa group (Kenya, Uganda, Mozambique, Malawi, Rwanda, Zambia), Exim-Tanzania bank (Djibouti, Comoro), TANALEC Ltd, (Nchi zote za EAC na maziwa makuu), Precision Air etc, etc. Pia NICOL si iliweza ku-mobilize nchi nzima na kuuza hisa wakapata mtaji mkubwa lakini wakazitumia vibaya/bad investment decisions?.

Matatizo yetu makubwa:

Kama KOMANDOO na ben van mike walivyonena huko juu bado wafanyabiashara wetu particularly kwenye hili eneo la supermakets wanaendesha kienyeji sana (lack of professionalism and modernity). Hivyo basi elimu zaidi juu ya namna ya kuendehsa biashara kisasa zaidi inahitajika.

Creative minds za vijana zinahitajika sasa, matajiri wengi wakibongo (wengi wao wazee) bado ni waoga ku-take risks, kumbukeni hata Uchumi supermakets ilielekea kufa kufa mwaka mwaka mmoja tu uliopita hivi sasa ndio inarudi tena.

Concept ya Chain stores sio mpya hapa Tanzania, kwa sababu zamani/enzi za mwalimu tulikuwa nazo na tulikuwa tunaziendesha kwa ufanisi mkubwa tu japokuwa hakutuwa na variety kubwa ya bidhaa kwenye shelfs mpaka tulipoanza mambo ya uchumi huria. Mfano ni hayo maduka ya RTC, maduka ya shirika la ugawaji etc, etc. yalikuwa yamesambaa nchi nzima na ndio wananchi walikuwa wakiyategemea.

Tuache tabia ya kulalamika na kuogapa kila kitu, tunatakiwa kubadilika. Nakumatt, Uchumi Shoprite, Games hayo yote ni maduka tu hakuna cha zaidi. Hakuna kisichowezekana.
 
Mkuu unachosema ni kweli, but kumbuka hayo makampuni unayo yataja yanafanya biashara nyingine kabisa, na ni kweli yana mitaji mikubwa sana

- MIMI NINACHO SISITIZA NI SWALA ZIMA LA MITAJI.

1. JE IKAJA KAMPUNI MFANO KUTOKA NJE KUWEKEZA KWENYE USAFIRI WA MABASI NA WAKAJA NA MABASI KAMA 500 KUNA KAMPUNI YA BONGO ITAWEZA SIMAMA?

2. HATA SUPERMARKET KUNA MINSUPERMARKET KIBAO TANZANIA WANA CUSTOMER CARE YA KUFA MTU BUT HAWAWEZI SHINDANA NA KAMPUNI KAMA SHOPRITE AU UCHUMI SUPERMARKET KWA SABABU YA MITAJI.

- C KWAMBA KAMPUNI ZETU HAZIFANYI VIZURI ZINAFANYA VIZURI KABISA TATIZO NI MITAJI YA KUWEZA KUSHINDANA NA MAKAMPUNI KUTOKA NJE,

3. KAMPUNI KAMA DR EXPRESS WANAJITAHIDI SANA NA KUNA NYINGI ZA MABASI ZINAJITAHIDI ILA IKAJA KAMPUNI KUBWA NINA UHAKIKA HAKUNA JIWE LITAKALO SALIA JUU YA JIWE JINGINE.

WATANZANIA KILA MTU ANATAKA AONEKANE YEYE KAMA YEYE, ANATAKA AMILIKI KITU CHAKE MWENYEWE, HUKU TANZANIA MAMBO YA KUUNGANISHA MITAJI HAYAPO KABISA NA HII ITAKUJA KUTO COST SANA, KAMPUNI NYINGI HAZITAWEZA KUSHINDANA.

CHUKULIA MFANO WA BIASHARA YA MABASI, UTAKUTA KUNA MTU ANA MABASI MAWILI, MWINGINE MATATU, MWINGINE MATATANO NA KAZALIKA, HEBU JARIBU KUWAAMBIA HAWA WAUNGANISHE NGUVU KAMA WATAKUELEWA
 
Uzuri ni kwamba dunia huwa haisubiri mtu, kama hawataki kubadilika nguvu ya soko itawabadilisha au kuwaondoa kabisa chaguo ni lao...:lol:

Kuhusu suala la mtaji bado nasisitiza kuwa Tanzania kuna hela nyingi sana kama una nia ya kweli kufanya biashara. Angalia juzi tu Ushirika (TFC) wameweza ku-mobilize Tshs billioni 25 almost $ 16 million kutoka kwenye benki za ndani wa ajili ya ujenzi wa jengo lao pale Mnazi mmoja...

Angalia linki hii hapo chini...

DailyNews Online Edition - Banks provide 25bn/- to TFC
 
Mimi nimoja Kati ya wafanyakazi waliowai kufanya kazi Nakumatt Moshi.
Mwenye swali Lolote lile kuisiana na Nakumatt nitakuwa tayari kuyajibu!!??
 
Back
Top Bottom