Nakufa mwenzenu usharauri tafadhali!

kazuramimba

Senior Member
Jun 14, 2011
126
57
Nimekuwa nikiumwa tumbo sana sielewi tatizo ninini.Nimetumia tiba mbalimbali kama dawa za minyoo na za typhoid lakini sijapona hapa mwananyamala naona wananisumbua au wanabahatisha tu.Nimekuwa nikiharisha mara chache sana ila tumbo limekuwa likiunguruma.Naombeni ushauri wakuu maana naona nakufa.
 
hao mwananyamala wanataka kitu kidogo, tafuta hospitali nzuri utakayolipia ili upate matyibabu ya uhakika
 
nenda hospitali nzuri kapime ujue tatizo ni nini hlf jitahd kutumia dawa za asili mf. Ukwaju ni dawa nzuri sn ya kusafisha tumbo na kutoa sumu.
 
nenda ospitali ya maana sio mw'ala. Usibanie pesa utakufa. Pole lakini. Kunywa maji mengi hasa asubui kabla hujala chochote. Google watertherapy utapata info. Kama unakunywa vya jioni acha kwa sasa
 
see the dr. kwenye hospital ya uhakika ndugu yangu. hutakufa, kuteseka kupo sana na kutaendelea kama hautajijali kwa kumuona dr.
 
Unahitaji kumuona daktari wa upasuaji (surgeon)...afya yako kwanza, halafu pesa baadae! Sidharau madaktari wa M'mala, lakini kila daktari ana upeo wake wa ujuzi, na ndio maana kuna madaktari bingwa.
 
Kaka inaweza kuwa h-pyroli namaanisha ni bacteria wanaopelekea vidonda vya tumbo.ukipimwa wakaonekana mapema unapewa dozi ya mwezi mmoja.ukimaliza unakuwa umepona kaka kama umeiwahi.
 
inawezekana una amoeba. Nenda hospitali nyingine kubwa, utapona tu. Kufa hutakufa ila maumivu utayaona.
 
pole sana ndugu nenda hosp. kama vipi chemshwa mwarobaini ongeza na majani fulani yanapandwa kama maua ila hayachanui, ukipata hiyo dozi kwa siku tatu wewe mzima kama zamani - samahani dr. riwa hii nayo ni tiba mbadala.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom