Nakerwa na tabia ya serikali kuingilia bunge na mahakama - angalia hii

salosalo

JF-Expert Member
Jun 7, 2012
596
278
Mapema hapo jana Mh. spika wa bunge la jamhuri ya muungano alikuwa akizuia wambunge kuzungumzia swala la mgomo wa madaktari eti sababu swala hilo liko mahakamani. Ni mangapi yanakuwa mahakamani na yanazungumziwa katika ukawaida wake bila kuhukumu? kama wabunge ambao ndio wasemaji wetu walizuiwa kutusemea majanga yanayotusibu(janga la kupoteza maisha) nani tena atatusemea?

kiukweli hali ile imenikera sana na imeonyesha dhahiri kuwa spika alipewa maelezo ya kufanya hivyo na upande wa serikali yaani Mawaziri. mbaya zaidi iko kama hata TV ya taifa TBC imekatazwa kuripoti chochote kuhusu mgomo wa madaktari maana taarifa ya habari ya saa 2 usiku hawajasema chochote kuhusu hali ya wagonjwa hospitalini. sitaki kamini kuwa habari hii wameona haina mvuto mvuto kiasi cha kutorushwa. lazima ni serikali imewaamuru wasifanye hivyo Na sasa naamini zile sababu za nyuma ya pazia zinazosemekana ndio zilizo muondoa bwana Tido Mhando kwenye kiti cha Mkurugenzi wa TBC. Kweli tutafika?

Mahakama nayo si huru, inafanya kazi kwa kuongozwa na serikali. Hapakuwa na haja ya kusitisha Mgomo wa Madaktari huku ikijua serikali imeshindwa kutekeleza makubaliano ya awali. yaani sijui nisemeje mnielewe hiki kitu nnachotaka niwaeleweshe
 
mkuu mimi nafikiri tatizo ni wabunge kutojua mjukumu yao. Maana sijawai kumsikia mbunge akiomba kura kwa wananchi huku akiwaaidi kuitete serikali. Mara nyingi utasikia niataibana serikali kwa hili na lile, lakini wakisha kula kiapo utafikiri mbwa mbele ya chatu yaani wanabweka kwa kushangilia.inaonekana wabunge wengi wanaenda bungeni kama wametumwa na serikali na sio wananchi, kubwa zaidi ni katiba inayompa rais mamlaka ya kuvunja bunge kabla ya wabunge kupiga kura ya kutokua na imani na rais, hii inawejengea hofu wabunge hadi wanajihisi wamewekwa pale na rais.!!
 
Watanzania mnajiponza wenyewe!! Mnapiga kura kama vipofu, kisha mnalalama kama vichaa!! Hiyo ndiyo serikali mliyoiweka madarakani ninyi wenyewe. Mliendekeza ushabiki wa Yanga na Simba kwenye siasa bila kuangalia uhalisia wa mambo!! Sasa tulieni mnyooshwe vizuri hadi hapo mtakapopata mang'amuzi mwaka 2015.
 
Sawa sawa kabisa mkubwa. Pia mimi nilitegemea spika angeruhusu hilo swala lijadiliwe ili kupata mawazo ya wenge ya namna nzuri ya kuondokana na tatizo. sasa wataenda kujifungia hao wanaojiita cabinet na kutoka na mawazo yao. Wangewasikiliza wabunge mawazo yao mbalimbali kisha tokea hapo wangeenda kufanya majumuisho. Nahisi uchumi wetu utashuka sana tusipoangalia maana tutatumia muda mwingi kwenye mazishi na kuzikana badala ya kuzalisha ndani ya siku zijazo. Kweli hii ni siasa ya Tz zaidi ya tuijuavyo
 
Watanzania mnajiponza wenyewe!! Mnapiga kura kama vipofu, kisha mnalalama kama vichaa!! Hiyo ndiyo serikali mliyoiweka madarakani ninyi wenyewe. Mliendekeza ushabiki wa Yanga na Simba kwenye siasa bila kuangalia uhalisia wa mambo!! Sasa tulieni mnyooshwe vizuri hadi hapo mtakapopata mang'amuzi mwaka 2015.

Duh! hivi kumbe ndio matokeo ya 2010?
 
Ttz ni udhaifu wa Bunge na sbb kubwa ni kutokana na wingi wa wabunge wa CCM. Hakuna zaidi
 
unafahamu maana ya jambo kuwa muahakamani? Au
Ndio nafahamu lakini hiyo sio sababu inayozuia jambo lisijadiliwe. tana kwa kulijadili jambo kama hili bila kutoa maamuzi ya kwanini Madaktari wamegoma wakati Mahakama imewazuia kufanya hivyo. Pale ilikuwa ijadiliwe tufanyeje ili kuokoa maisha ya wa TZ wanaoangamia bila sababu kwa sababu ya uzembe wa pande moja kati ya Serikali au Madaktari au wote kwa pamoja.

Kumbumbuka Mahakama lao ni Uhalali wa kuwepo kwa mgomo na Utii wa amri ya mahakama. Sisi raia letu ni tunasaidiwaje kufuatia kuwepo kwa mgomoo? hilo haliwahusu mahakama hata kidogo.
 
ckatai lakini lijadiliwe sehemu ingine cyo bungeni maana huo ni mhimili mwingine, nadhani unatambua.
 
unafahamu maana ya jambo kuwa muahakamani? Au
Haya sema sasa swala liko mahakamani, Raisi kazungumzia swala lililo mahakamani kwenye hotuba yake. yote kwa yote Wabunge wa chama tawala wamejadili swala lililo mahakamani hapo jana tena. Bado unalakusema? Hii ndio Tz zaidi ya uijuavyo
 
Back
Top Bottom