Elections 2010 Nakaaya arudisha kadi ya CHADEMA

Nakaaya Sumari ameamua kujitosa katika kinyang"anyiro cha kuwania ubunge wa viti maalumu mkoani Arusha kupitia chama cha demokarisia na maendeleo (Chadema) kwa kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo mjini Arusha.
nakaayasiasa.jpg

VIPI UBUNGE ALIKWAMA? Pole sana mama....... Rudi ukale hela za kodi yetu na migodi. Ila angalia usije ukawa umekosea.
wabunge wa viti maalum maamuzi yatatolewa baada ya uchaguzi mkuu, wote waliambiwa waende majimboni wakahamasishe ili kuzoa viti vingi. kwa hiyo mchango wa mgombea viti maalumu ndiyo utakao judge nani awe na nani asiwe, hiyo ni katika kutekeleza falsafa ya siyefanya kazi na asile, huenda Nakaaya ameshindwa kufanya kazi hiyo na ameona kuwa hatapata viti maalum. kwa hisani ya watu wa marekani.
 
Nakaaya Sumari amerudisha kadi ya Chadema jioni ya leo na kumkabidhi JK kwenye mkutano wake ulio fanyika leo mkoani Arusha, JK amempongeza sana kwa kitendo hicho na kumwambia karibu mama CCM ndicho chama pekee Tanzania.

kalogwa???????????????????????????????????????????????????????????????????????????/
 
Ningekufa kama ningesikia Prof. Baregu au Chacha Wangwe au Mzee Mtei karudisha kadi ya Chadema ......................

Huyo choko tu. Nakaaya ni sawa na simu ya kichina tu. Garantii wiki moja. Hawezi zuia mawimbi ya bahari kufika ufukweni...................

Kwanza nilikuwa sijui hata kama naye yuko Chadema.

Tunakuja na haturudi nyuma.......................

Kama vyama vingi ni vita (kama tulivyokuwa tunapumbazwa zamani), basi CCM watavianzisha hivyo vita.................

Anguko la CCM lipo karibu sana .......................

Soma alama za nyakati .................................

CCM ni nafsi. Na kila nafsi itaonja mauti

I hear you mkuu, ile lugha ilikuwa kali na ingeleta atention za mods bila sababu
 
Nakaaya Sumari ameamua kujitosa katika kinyang"anyiro cha kuwania ubunge wa viti maalumu mkoani Arusha kupitia chama cha demokarisia na maendeleo (Chadema) kwa kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo mjini Arusha.
nakaayasiasa.jpg
Nakaaya ambaye ni katibu mhamasishaji wa baraza la vijana la Chadema wilayani Arusha alichukua fomu ya kuwania kiti hicho juzi katika ofisi za chama hicho zilizopo maneeo ya Esso jengo la Meru Plaza mjini Arusha.
Akiwa ameongozana na mwenyekiti wa vijana wa Chadema wilaya ya Arsuha. Exaud Mamuya sanjari na katibu wa vijana, Arnold Kamnde, mgombea huyo alichukua fomu ya kuwania kiti hicho majira ya saa 3:30 asubuhi katika ofisi hizo.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fomu ya kuwania kiti hicho Nakaaya alisema ya kuwa binafsi anahisi ya kuwa nafasi ya yeye kuwa mwakilishi wa wanawake wa mkoa wa Arusha katika bunge la jamhuri nchini kupitia chadema mkoani Arusha umewadia.
Nakaaya alisema ya kuwa lengo kubwa lililomsukuma kuwania nafasi hiyo ni kutokana na uchungu alionao hususani mateso wanayopata wakinamama katika masusla ya afya ya uzazi katika huku akihaidi kusimamia masula ya afya ya uzazi kwa wakianamama nchini.
"Nahisi muda umefika wa kutenda ninayoyahubiri siku zote,nataka nikasimamie matatizo ya uzazi kwa wakinamama hili linanipa uchungu katika maisha yangu siku zote.Nataka nikawawakilishe wanawake wa mkoa wa Arusha kupitia chama changu nina imani nitashinda nafasi hii kwasababu ninajiamini, hivyo naomba mniunge mkono wanawake'alisema Nakaaya.
Awali akimkabidhi fomu ya kuwania nafsi hiyo katibu wa Chadema wilayani Arusha,Bakari Kasembe aliwataka wanawake wote wa mkoa wa Arusha kupitia chama hicho kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi hiyo.
Kasembe alisistiza ya kuwa awali chama chao hakikuwa na uwakilishi wa kiti hicho mkoani Arusha katika bunge la jamhuri nchini lakini wakati huu wamejipanga kutoa viti vitatu na kiti cha ubunge wa Arusha mjini.
Tayari joto la kuwania nafasi ya ubunge wa viti maalumu mkoani Arusha kupitia chama hicho limeanza kushika kasi ambapo hadi sasa tayari wagombea wawili wameshajitokeza kuwania kiti hicho ambao ni Magreth Olotu na Joyce Muya.

From: Wahapahapa

VIPI UBUNGE ALIKWAMA? Pole sana mama....... Rudi ukale hela za kodi yetu na migodi. Ila angalia usije ukawa umekosea.

Akikua ataacha, mi namshangaa pamoja na kuwa ni haki yake kuchagua ila vipi juzi tuu alikua mstari wa mbele kuwaponda viongozi wa siasa walioko madarakani kwa wimbo wake na leo ghafla anajiunga nao? well kama nilivyosema akikua ataacha, kwenye blog yake nilisoma jinsi alivyokua na mapambano na maisha yake kwa ujumla na mahusiano yake ila najaribu kumwelewa huyu mwananchi mwenzangu na kumwachia nafasi ya kujisoma na kujitambua, All the best with the turn you took and we will accept u if u decide to come back as u went. U said it all before in your blog so we need not ask u nothing now what with the confusion. Siasa sio Bongo fleva yahitaji moyo na uzalendo.
 
Akikua ataacha, mi namshangaa pamoja na kuwa ni haki yake kuchagua ila vipi juzi tuu alikua mstari wa mbele kuwaponda viongozi wa siasa walioko madarakani kwa wimbo wake na leo ghafla anajiunga nao? well kama nilivyosema akikua ataacha, kwenye blog yake nilisoma jinsi alivyokua na mapambano na maisha yake kwa ujumla na mahusiano yake ila najaribu kumwelewa huyu mwananchi mwenzangu na kumwachia nafasi ya kujisoma na kujitambua, All the best with the turn you took and we will accept u if u decide to come back as u went. U said it all before in your blog so we need not ask u nothing now what with the confusion. Siasa sio Bongo fleva yahitaji moyo na uzalendo.

Kuna kazi kweli mkuu ... redio, tv, promoters zote wako kwenye kampeni.
Inatia huruma akikumbushwa haya yote lakini ndio hivyo tena, dawa imetoka kwenye chupa ya mswaki.
 
Hii kuhama chama inaweza hata kumnyang'anya washabiki wa muziki wake. Labda awe ameamua kufanya siasa kazi na ahadi ya uDC

Inaweza kumsaidia kutembea na JK kwenye kampeni zake mikoa ilosalia kama Flora Mbasha, Marlow na TOT, atapata mshiko wa kutosha kwa night zilizobakia.
 
[video]http://www.weloveafricans.com/video_player/videoid/14284/nakaaya-feat-m1---mr-politician[/video]


Anaimba very logical song lakini hamaanishi kumbe ni njaaa jamani! lakini si cha ajabu, maana CCM ndo wenyewe kwa zile milion 60. Lazima dau limepanda saaana. Ila watanzania hatudanganyiki! Natamani sana nione watu kama hawa baadae wawepo wakati Tanzania ikipiga hatua kubwa kiuchumi chini ya serikali tofauti na ccm.
 
MSANII wa kizazi kipya, Nakaaya Sumari ambaye mapema mwaka huu alijiunga na
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amejiondoa katika chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Nakaaya jana alijiengua Chadema na kujiunga na CCM muda mfupi, kabla ya mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho, Rais Jakaya Kikwete hajahutubia mkutano mkubwa wa kampeni kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid hapa.

Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda, ndiye aliyeweka wazi kuhamia kwa Nakaaya katika chama hicho wakati alipokuwa akitangaza utaratibu wa mkutano huo kabla
ya Kikwete kuhutubia.

"Mheshimiwa mgombea wa urais na Mwenyekiti wa CCM Taifa, nitamkaribisha Mwenyekiti
wa Mkoa akukaribishe ili kabla ya kuhutubia, uje umkabidhi kadi mmoja wa vijana wetu maarufu, msanii Nakaaya Sumari ambaye alikuwa amepotea na sasa ameamua
kurejea katika chama chetu," alisema Chatanda.

Kwa upande wake, Nakaaya aliyejipatia umaarufu kwa kibao chake cha ‘Mr Politician', alisema amerejea CCM na kushukuru kwa kupokelewa tena.

Kuonesha umahiri wake katika sanaa, msanii huyo aliimba mashairi machache ya kuisifu
CCM, akitumia falsafa ya mwaka huu ya Rais Kikwete ya ‘Ari Zaidi, Nguvu Zaidi na Kasi Zaidi.' Baada ya kumaliza hotuba yake, Rais Kikwete alimpongeza Nakaaya kwa kujiunga na CCM na kumkaribisha katika chama hicho, na kueleza kuwa atajiunga na kundi la wasanii wenzake kuhamasisha wananchi waichague CCM.

NB: Bila shaka kaahidiwa kitu na JK, sijui tunaenda wapi?

Source: HabariLEO
 
Hana Jipya alikuwa natafuta umaarufu wa kukutana na JK na leo hii wapo Hoteli Moja sasa Huko anaimba wimbo au........................Anapewa nini??? Taarifa baadaye
 
Dau lake kuhama ilikuwa kiasi gani? Nadhani kuna wafuatiliaji tayari wanalijua hili..
Nimesikia msimu huu wameambiwa nyota yao #6..hivyo inawezakana dau likawa mil 6 au 60..sijui! hebu mtujuze
 
Dau lake kuhama ilikuwa kiasi gani? Nadhani kuna wafuatiliaji tayari wanalijua hili..
Nimesikia msimu huu wameambiwa nyota yao #6..hivyo inawezakana dau likawa mil 6 au 60..sijui! hebu mtujuze

kuna mtu kaniambia kuwa katanguliziwa milioni 30 na atapewa milioni 30 baada ya kampeni. Sitaki kuamini hili ila hata kama ni kweli, Nakaaya amefanya maamuzi yake na mimi binafsi namtakia kila la heri huko ccm
 
Nakaaya amefanya uamuzi ambao ni mzuri kwake. Ndiyo uzuri wa demokrasia. Vyovyote vile ilivyokuwa pressure ilikuwa kubwa sana kwake. Somebody had to give.
 
Wanaojiunga na CCM kipindi hiki, poleni sana, CCM iko mwishoni sana kuanguka hata kama hamna vyama vya upinzani, ni lazima CCM kuanguka, muda unaruhusu CCM kuanguka. CCM haina muda mrefu wa kuanguka.

Dalili ya CCM kuanguka ni pamoja kubeba watu kwenye magari tayari kupelekwa kwenye kampeni kama magunia, kukakataa kushiriki kwenye midahalo, kukataa kuumlizwa maswali wakati wa kampeni, rushwa kuongezeka sana.

Narudia kusema CCM imebakiza muda mfupi sana. Tusubiri, mimi ninaipigania nchi yangu.
 
Back
Top Bottom