najutia moyo yangu

mmmh, husyn ndugu.
Kuna wakati maji yanazidi unga, labda upike uji na si ugali.
Kama wataka ugali itabidi tu kugonga kwa jirani na kusema ulilonalo rohoni.

umeona eeh! Bora mtu ufe nalo moyoni kama anashindwa kusoma alama za nyakati.
 
Umesema lililokuwa moyoni mwako hata kama amekutolea nje. Be happy coz at least alikupa nafasi ya kukusikiliza. Amini kuwa si wako japo wampenda. Piga moyo konde na vuta subiri utampata akupendae kwa dhati.
 
Alokwambia mwanaume anatongozwa nani?wanawake kueni na mipaka mna2panda vchwni sasa,kesho c utaanza kuomb upige vidole vya ma......o?zist kamili.
 
Hivi kuna ubaya kwa msichana kumueleza mwanaume hisia zako.Nujutia nafsi yangu kwa kumuonyesha hisia za kweli mwanaum

Hakuna ubaya. Usijute. Tatizo si wewe bali ni mwanaume. Yupo atakekuja kurudisha pendo lako kwa dhati.
 
huyo mwanaume hana kosa kwani ana uhuru wa kukubali au kukataa kama ilivyo kwako,usijutie,,,pole kama amemega kisela.jipange upya shogaa yasikukute tena:confused3:
 
Hivi kuna ubaya kwa msichana kumueleza mwanaume hisia zako.Nujutia nafsi yangu kwa kumuonyesha hisia za kweli mwanaum
kwani ukionyesha unapenda ndo lazima ukubaliwe, mbona ni kawaida kwa wanawake kukataa wanaume ilihali wanaume hao wanawapenda kwa dhati? wewe kama unae mtu wako, wakija wengine kuonyesha hisia nao utawakubalia pia?. kubali matokeo, usilalamike. unavyojisikia kukataliwa , hiyo ndo maisha ya kila siku ya wanaume
 
umeona eeh! Bora mtu ufe nalo moyoni kama anashindwa kusoma alama za nyakati.

We acha tu ndugu yangu, hawa watu wangekuwa wanatuelewa wala kutoswa isingekuwa shida! Ebu fikiria.....unapigwa mtoso na kudharauliwa juu (as if mhuni) kumbe ni moyo kweli umependa!! loh sipati picha aisee!
 
mmmh, husyn ndugu.
Kuna wakati maji yanazidi unga, labda upike uji na si ugali.
Kama wataka ugali itabidi tu kugonga kwa jirani na kusema ulilonalo rohoni.

Ndo hivo sasa mdada anatakiwa ajiandae na majibu yeyote....sio kunung'unisha nafsi na kuapa kutokupenda tena!!
 
Hii nayo ni aina ya stigma wanawake waliyonayo. Haimaanishi ukimwambia mwanamme unampenda naye akubali. Anaweza kuwa na komitimenti na mtu mwingine au hakupendi kiasi cha kuwa na mahusiano.

Ni kawaida kama wanawake wanavyowakataa wanamme ili hali anajua kabida anapendwa, lakini anakataa sababu hampendi.

Tatizo mwanamke anataka akimfuata mwanamme aruke ruke na kukubali straight, haiko realistic hii.

Ndo hivo sasa mdada anatakiwa ajiandae na majibu yeyote....sio kunung'unisha nafsi na kuapa kutokupenda tena!!
 
Ukitongoza jiandae kwa jibu mbili: kuna kukubaliwa na kukataliwa
Hajakosea kukukatalia, sema tu akatae kwa kutumia lugha nzuri.
Pia kuna tofauti kati ya kutongoza na kufunguka kuhusu hisia
Anae toongoza anataka jibu, anae funguka anaongea just FYI
 
Hii nayo ni aina ya stigma wanawake waliyonayo. Haimaanishi ukimwambia mwanamme unampenda naye akubali. Anaweza kuwa na komitimenti na mtu mwingine au hakupendi kiasi cha kuwa na mahusiano.

Ni kawaida kama wanawake wanavyowakataa wanamme ili hali anajua kabida anapendwa, lakini anakataa sababu hampendi.

Tatizo mwanamke anataka akimfuata mwanamme aruke ruke na kukubali straight, haiko realistic hii.

Si ndo hapo sasa!! Kama sisi tunavyowakataaga na wao wana haki hiyo hiyo....sema mbaya ni ile mtu anakudharau na kukuona kama kicheche!!
 
Pole dada.

Lakini hongera kwa kushinda stigma ya mwanamke kumtongoza mwanamme.

Ukiachilia mbali kukataliwa na uliyemtaka, hebu jiulize, wewe umeshakataa wangapi waliokutongoza?

Unadhani mwanamme hana haki ya kukukataa kama hajisikii kukubali?

Na kama akikubali kila anayemtongoza, atakuwa na wangapi?

Haina haja ya kujuta, ni mapito tu. Shida ni kama aligonga mzigo afu akasepa.
Kudagadeki.....

Nyie mnavyotupiga vibuti mnafikiri na sisi hatuumii siyo?

Mkuki kwa nguruwe..........
 
Hivi kuna ubaya kwa msichana kumueleza mwanaume hisia zako.Nujutia nafsi yangu kwa kumuonyesha hisia za kweli mwanaum

Swali;....ubaya kumwambia mwanaume hisia zako,
Jibu; hakuna ubaya.

Maelezo; ...unajutia kumuonyesha mwanaume hisia za kweli...
swali; kwanini?
 
Pole Milcah..

Hukufanya kosa ila huyo baba ndiye wa kulaumu kwa kutothamini jinsi ulivyomuami na kumpa ukweli wako kwake...

Kuna wakati wanaume wanakuwa watu wabaya sana...

...yaani mwanaume amekuwa mbaya kwakuwa yeye hana haki ya kupenda kwingine?
Kwa tafsiri yako ni LAZiMA "umpende" anayekupenda? Utapenda wangapi?
 
Duh! Pole, ni kawaida kama ambavyo wewe uliwatosa wanaume walioonesha hisia za kweli. Usiruhusu mateso ya moyo bidada.

....nice one,....ndio maana sikubaliani na wale wadhaniao ati utayempenda naye lazima akupende
hivyo hivyo....mapenzi sio "fikra" pekee...mapenzi ni vitendo na maisha ya kila siku...incl...kupenda,
kujithamini na kujielewa wewe mwenyewe ambako kunapelekea mazingira ya kupendeka ( sio kutamaniwa)
 
pole sana
namshangaa huyo ulompa moyo wako akakudharau na kukupuuza
mbona wengine hatuna hiyo bahati wajamini?
asie na bahati habahatiki

...hahaha...

Inaonyesha hujali/ hujui hisia zao unapopendwa....maneno yako sounds like a serial "player" (ashakum si matusi)
 
Back
Top Bottom