Najuta Kuipigia CCM Kura

Status
Not open for further replies.

Muke Ya Muzungu

JF-Expert Member
Jun 17, 2009
3,444
264
Source: Mange Kimambi Blog: [mods tafadhali msiondoe kama mnawatendea watanzania haki hizi ni picha zao wenyewe]

Baada ya tusi la binti mfalme kuturingishia hekalu lake [hisani ya mwandishi wake wa habari] nimeumia sana moyoni kwani nafanya kazi kwa bidii licha ya elimu yangu kubwa ambayo hainisaidii kuwalisha wanangu vizuri. napokea mshahara wa Tsh. 800,000 kwa mwezi. Nina shahada ya uzamili nimeajiriwa na taasisi ya umma, nyumba ninayoishi ni ya kupanga na malipo kwa mwezi ni Tsh 400,000 hapo makato kazini bado hela za chakula bado nauli bado. Sasa nashangaa mtoto wa kiongozi ambaye ameanza kazi nyuma yangu anakuja na jumba la billioni 3 najiuliza ni nini alichokifanya zaidi ya kujianika kwenye viombo vya habari na mablogs ambacho mimi nimeshindwa kukifanya. Mods naomba msitoe post yangu kwa maana ni la kisiasa na sijataja jina la mtu. Waache wana jukwaa walijadili mada yangu. Naomba kujua ni kitu gani wanachokidanya watoto wa viongozi wa CCM ili kupata utajiri wa haraka hivi? Naombeni mchangie mada kwa umakini na pia TAFAKARINI tunakoelekea. Tunawapigia kura alafu wanaturingia mali walizochuma . Mtakaosema wivu poleni siyo wivu. Ni usawa kwa wote. kumbukeni maisha bora kwa kila mtanzania na siyo kwa baadhi
View attachment 46432View attachment 46433View attachment 46434View attachment 46435View attachment 46436View attachment 46437View attachment 46438View attachment 46439
 
kwani wewe uko peke yako hapa Tanzania? kwani ilishinda kwa moja? acha kujidanganya.
 
Unafanana sana na wale madada wanaokumbuka dawa ya penzi wakati 'kisu' kipo kwenye ALA ya 'kuazima'
 
jaman mtoa mada yupo sahihi,.kalitambua kosa na amekir sidhan kama ni sahih kumnanga hvyo ila tumshukuru Mungu kwa kumfumbua macho na tumuombe afumbue wengi ili 2015 wafanye machaguo sahihi
 
na bado hamjajuta vizuri. Bila shaka hii mada ni ya mwanamke. hIVI NYI SI NDO MLISEMA MNATAKA RAIS MUUZA SURA? I wish......!!!!!!

Paaambaffff!
 
chukuru churulu si ndondondo! BIla shaka kura yake na yangu na ya yule ndo zilileta ushindi nakushindwa kwa wengine
kwani wewe uko peke yako hapa Tanzania? kwani ilishinda kwa moja? acha kujidanganya.
 
Tunajuta wakati kama huu tunapoona mambo yanakwenda ndivyo sivyo. Lakini ukifika wakati wa Kampeni bado kila kona watu tumevaa T-shirt, kofia, na khanga tunatangaza sura za watu.

HUKU TUNASEMA "KIDUMU CHAMA CHA MAFISADI"

Tukienda kwenye sanduku la kura kwa sababu tulipokea Tsh. 1,000/= basi hapo tunasema

"WAJINGA WOTE TUTIE, TUTIE, TUTIE TUTIE KWA MOYO MMOJA, NAMBARI WANI EEEEE, NAMBARI WANI NI CCM"

LEo tusilalamike ndio malipo ya Ths. 1,000/= haya!!!!!!!!!!!!

MIZAMBWA
IANIUMA SANA!!!!
 
Huo ni mwaka mmoja na mwezi mmoja! baado miaka mingine mitatu! kha.
POPOBAWA.
 
Ujinga uloufanya uwe fundisho mwaka 2015, waelemishe na wajinga wenzako wa mwaka 2010, msifanye tena hilo kosa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom