Najuta Kuifahamau M-PESA

Nilidhani watu wa kipato cha chini tumepatiwa mkombozi na voda com,
kumbe sio mkombozi ila ni malaika izraele mtoa roho aliye kuja kwa sura ya upole, upendo na tabasamu huku nyuma yake akiwa na silaha kali yenye kukuua kifo cha taratibu chenye makali na machungu yasiyomithilika.
Nimetumiwa vijisenti kama laki nne hivi , nilipoenda kuvidroo nimekatwa shilingi elfu saba,
jamani....
Hivi ni benki gani ya biashara yenye bank charges za juu kiasi hiki?
Je mamlaka zinazosimamia maswala ya fedha zimeshindwa kabisa kumshauri rostam azizi arekebishe tariff zake??
Kweli rostam kwa sasa ndiye baba wa taifa.

Hebu cheki vizuri mkuu, sina la kuzungumza kuhusu gharama za M-PESA kv sijawahi kutuma wala kutumiwa pesa kwa njia hiyo! Hata hivyo, nina idea ya kutosha kuhusu money transfer fee ktk benki zetu; hususani Benki ya Makabwela. Kama unamwingizia/unamtumia mtu pesa kwenye a/c ya NMB, basi ni FREE-Lakini assume upo kijijini kwetu ambako mathalani hamna CRDB na wewe unataka kumtumia mtu Sh. 400,000/= kutokea NMB kwenda CRDB, or any other bank( and the reverse hold true); then transfer fee hapo ni Sh. 20,000/= (then compare with sh. 7,000/=). The best option, is to have the bank account, though the question remain "which bank and for which reason!"
 
Kwa mteja asiyesajiliwa hakatwi kitu chochote anayekatwa ni mtumaji, ila kama wote mmesajiliwa sender na rreceiver unakatwa 200, ni huduma nafuu sana labda wewe hukuelewa
 
nadhani ukiwa umejisajili na mpesa unakwatwa hela ndogo sana.jaribu kuchat na watu wa vodacom uone imekaaje
 
Back
Top Bottom