cheusimangala
JF-Expert Member
- Feb 27, 2010
- 2,585
- 497
As salam aleykum wapendwa wangu.
Natumai pasaka imekua yenye furaha kwenu.
Wapendwa kwa asili mim ni mtu mwenye kupenda utani na mtu ambaye ni vigumu saaana kukasirika.Hakuna binadamu asiyekasirika lakini kwa kweli mimi Cheusie nikikasirika lazima hilo jambo litakuwa kubwa mara nyingi mim ni mtu wakufurahi na mwingi wa tabasamu usoni mwangu.
Lakini wapendwa sijui ni nini kimenipata siku za hivi karibuni,yaani ninaweza kuamka nikiwa nimejawa na hasira bila hata kuudhiwa na mtu yeyote.Yaani siku hiyo shemeji yenu nimpendae kupita maelezo kila atakaloongea nitaona linanitibua,akijaribu kujitetea kuwa hajamaanisha kitu kibaya ndio anakua kaharibu kila kitu.Yaani siku za kuamka na hasira na kuwa sijisikii kuongea na mtu yeyote.Siku kama hizi hata JF siingii sababu nikiingia naweza kujibizana na mtu vibaya nikaishia kuwa banned.
Ajabu ni kwamba kuna siku nyingine tena naamka moyo wangu unakua umejaa furaha ya ajabu,furaha ambayo sijui hata inatokea wapi.
Kuna siku naweza nikaamka nikiwa nina huzuni ya ajabu,huzuni ambayo siwezi kuelezea imesababishwa na nini.Siku hiyo naweza kujikuta najisikia kulia,kama niko nyumbani nitajitupa zangu kitandan machozi yatanitoka nitalia wee huku nikisikia huzuni kubwa moyoni mwangu.
Shemeji yenu,marafiki,wanafunzi na wafanyakazi wenzangu nahisi wamegundua kuwa siku hizi siko normal,naona wanakua kama wananisoma kwanza kuona kama leo Cheusie kaamka na mood gani,nikiwa na mood ya furaha basi wataongea na mim kama tulivyozoea siku zote,nikiwa na mood ya hasira au huzuni naona wanakua makini wakati wakuongea na mimi.
Kiukweli nahisi something is not right with me,sijui ni nini kinanisumbua,lakini najijua mimi hii sio kawaida yangu.
Je hii ndio Depression au ndio dalili za stress? Au hii ni nini jamani..
Niko serious,naombeni kama kuna mpendwa yeyote humu ndani ameshawahi kutokewa na kitu kama hiki aniambie au kama kuna wataalam mnaojua hii inasababishwa na nini mnisaidie.
Natanguliza shukrani zangu kwa mtakaonichukulia serious na kujaribu kunisaidia.
Asante.
Cheusie.