Najichukia kwa hili tatizo langu la ngozi, nimekosa mwenza

Mamboz,jamani kama mnakumbuka nilikua natafuta mchumba na hali yangu niliyonayo,wengi walijitokeza wakidhani natania labda,walihisi mimi ni mzuri sana ila natania.

Kusema ukweli nipo kama nilivyosema,na nimerudi tena kuomba msaada kwa anaejua dawa ya makovu tafadhali,sio ya ajali yani yanatokea tu hata nikijikuna kovu linabaki,pia nikiumwa na mdudu lazima kovu libaki,nikijikwaruza kidogo bas kovu hilo.

Wanaume pia hawaniangalii hata mara mbili,niko mpweke,sina hata mwenza.

Nachukia sana ngozi yangu na sijui shida ni nini,naomba tafadhali kwa anaejua dawa ambayo itanifaa...

Wanawake wenzangu nisaidieni,kina baba,kina kaka naombeni mnitajie dawa itakayoondoa makovu haya jamani.

Bio oil nimejaribu haifanyi kazi,aloevera hua napaka sioni matokei,limao pia hakuna kitu.

Najisikia vibaya sana,mda mwingine hua nikijiangalia nalia tu,why me?
Msaada wenu ndugu zangu tafadhali.
Nenda kanisani kaombewe rafiki yangu, usimkufuru mungu kwa kuchukua hali yako, wangapi ambao ni walemavu wa viungo vyote!!! Wewe ni ngozi tuu dadaa
 
not guaranteed!
FACT IS AKATAE KUOLEWA KWA HURUMA!
atateseka maisha!
ANADESERVE KUPATA MUME ANAYEMSTAHILI!SIO WA KUMUOA OUT OF SYMPATHY AU KUKOSA CHAGUO YYE AWE SECOND AU LAST OPTION!
BIG NEHIIIII!
dada snowhite, huyu anaonyesha kukata tamaa hata post yake ya kutafuta mchumba ameonyedha kasoro nyingi ambazo sidhani kama zinawavutia wengi ushauri wangu ni mzuri tu akiufua5a akajishikize kwa jamaa yake mmojawapo akisema asubiri mpya anaweza kubahati ndio ila mara nyingi ni bora mwanamke aolewe mspema
 
Nenda hospital wangu wakupime mwanza unaweza Tunis dawa ukizingatia ushauri wa watu Kumbe unazidisha tatzo ,cha msingi Nenda ukapimwe ngozi yako mpka damu ,kwasababu huenda unamchafuko kwenye damu yako ndo mana ngozi inakua dhaifu
 
U are beautiful keep that in mind. Ngozi si kielelezo tosha. The beauty is & will always be inside you. Thats one. Pia kuhusu dawa utapata tu. Just be patient.
 
Nenda hospital wangu wakupime mwanza unaweza Tunis dawa ukizingatia ushauri wa watu Kumbe unazidisha tatzo ,cha msingi Nenda ukapimwe ngozi yako mpka damu ,kwasababu huenda unamchafuko kwenye damu yako ndo mana ngozi inakua dhaifu
Asante,nitafanya hivyo
 
meshibajeee!
Sa skia!
ACHANA NA KUJITAZAMA UNAANGUKA KATIKA NINI ,TAZAMA U BORA KATIKA NINI!
ITAKUSAIDI KUONA ULIVYO WA THAMANI NA KUUVAA UTHAMANI HUO!
LAKINI ITAKUSAIDIA PIA HATA KUTAFUTA MATIBABU WITH A POSITIVE MIND,KWA IMANI KUWA HIYO SIO LAANA!

kwa kuanzia
hebu badili mfumo wako wa ulaji
kula zaidi mboga za majani maji kwa wingi,amtunda
punguza au acha kabisa matumizi ya nyama nyekundu hususan ya ng'ombe.
pumzika muda mrefu
lala mapema
fanya mazoezi
achana na kutafuta kimbilio la kula kila unachokiona kufidia upweke wako!
halaaaafu kingine hebu tafuta hobbies na uziishi
angalia movie
ongea umbea wa insta(enh story za ally kiba na jet yake na zenyewe zinasogeza siku)
jifunze mapishi mapya
anzisha kajiproject hapo home,maua,fuga kuku,paka (UKIONA VIUMBE WENGINE WANAKUA NA KUFURAHI KWA AJILI YAKO IT WILL GIVE UR LIFE A TOTAL MEANING OF EXISTENCE NA KUTEGEMEANA )
furahia marafiki ulio nao,tumia vipawa vyao kuwa na furaha!
nenda uangalie movies(mlimani city kuna kichupa cha hatar Dec 02 ,yani ijumaa hii!)kama upo dar nenda asee
saidia wengine kufurahi,utaona kuwa maisha yako yana thamani kwa wengine kwa vile watakavokuthamini!

HIVI UKIMIX NA MSAADA WA KITABIBU KAMA KUCHECK DAMU,NA KUPATA DAWA NA KUZITUMIA!
aseeeeee utaona maisha yalivyo jambo jema na a kheri WITH OR WITHOUT NGOZI YA KUTELEZA KAMA UNAOGEA MAYONAISE!
sawa?
HEBU FANYA HII uje unipe feedback by pasaka mwakani!
Asante nitajaribu
 
Hangaika kwanza na uzima wako. Mambo ya kukosa mwenza hayo ni majaliwa. Kumbuka wapo mabinti warembo mpk wanakera, ila hawana furaha na wapenzi wao.
 
Kama wewe ni mkristo au hata kma sio mkristo ila unaamini katika maombi, tafuta watumishi wanaotoa huduma za kuombea watu, naamini ukiwa na imani watakusaidia. Kinachofanya tushindwe kupona matatizo yetu muda mwingine ni kwmb tunakosa imani tu. Ukimpata mmoja mwelezee vizuri shida yko. Binafsi naamini kma utapona. Fanya maamuzi tu wewe mwenyewe.
 
Back
Top Bottom