Naisikitikia tanzania

Chona

JF-Expert Member
Mar 8, 2010
523
360
Naisikitikia nchi yangu Tanzania kwa kile kilichokilichotangazwa na Prof. Magembe kuwa serikali itafuta mitihani ya Darasa la saba ili kuwawezesha wanafunzi wote kuingia kidato cha kwanza. Najiuliza swali, Je tatizo ni mitihani au tatizo ni ufahuru wao. Na kama tatizo ni ufahuru wao jibu ni kuondoa mitihani au kutafuta njia ya kuwezesha ufahuru wao uongezeke.

Kwanini ninasikitika badala ya kufurahi kwa tamko ilo!

1. Kufuta mitihani kutapunguza hamasa ya wanafunzi kujisomea, kwasababu wanafunzi wengi wanasoma ili waweze kujibu mitihani na kwa kufanya hivyo wanajikuta upeo wao wa kuelewa umeongezeka ingawa wao walitaka wajibu mitihani tu.
2. Utafiti uliofanywa na taasisi ya Twaweza unaonyesha kuwa wanafunzi 2 kati ya 10 waliomaliza darasa la 7 hawawezi kusoma kiswahili cha darasa la 2 na nusu ya wanafunzi wanaomaliza darasa la 7 hawawezi kusoma kiingereza cha darasa la 2.
Source:Twaweza.org
(Labda mtanisaidia kuiweka vizuri hii link ili mtu aki click imdirect kufungua)
Hii ni hatari kwa taifa kuendelea kuwa na mbumbu wengi hasa kwa wakati huu wa soko huria.
MTAZAMO WANGU
Kuna uwezekano kunataka kuandaliwa kizazi cha wenye nacho na wasionacho, napengine kizazi cha watawala na watawaliwa.

Kwanini basi nafikiria hivyo
Katika hali ya kawaida mwajili yoyote yule anaajili mtu si kwasababu ya vyeti tu lakini pia uwezo wa mtu. Sasa kama vijana wetu hawawezi kuwa wanajaribiwa kwa mitihani ya kitaifa sio tu darasani, kata au wilaya tu watawezaje kujipima na kuangalia position yao kitaifa. Kwamba yeye na wanafunzi wengine wa mahali pengine wanazidianaje kwasababu kwenye ajira mwanafunzi wa Mbeya atakutana na wa Kagera na Mtwara na Mara na Arusha na Mahali pengine nchini na duniani kote. Kwahiyo lazima uangalie uwezo wako na watu wengine wa mahali pengine pia.
Lakini kama hilo halifanyiki matokeo yake vijana wengi watakuwa wanasonga mbele tu kumbe uwezo wao upo chini sana. Na matokeo yake wakifanya mtihani wa form 4 wanafeli na baadaye kungundua kuwa kumbe wangeweza kujiandaa upya na wakati huo watakuwa wamesha chelewa sana kwani waswahili husema 'Samaki mkunje angali mbichi'.
Lakini wale watakao kuwa shule nzuri za private(kwasababu hazitakubali kudahili watu bila kuwapima) hawataweza kupanda vidato au kuingia form1 bila kufanya mitihani na kwasababu hiyo ni wale waliofanya vizuri tu ndo wataweza kuendelea. Kwa hiyo katika hali ya kawaida ni vigumu kumpambanisha mwanafunzi aliyezoea kufanya mitihani ya mara kwa mara ya kujieleza na mahesabu ili aweze kupanda kidato kwa kufikia passmark na yule ambaye kwake kupanda kidato si kwasababu ya kufanya vizuri darasani bali kwasababu muda wake wa kuwa kidato hicho umeisha hivyo inamlazimu apande kidato tu kwasababu ni mwaka mwingine.

Nadhani huu ni mkakakti unaoandaliwa kuwapatia elimu mbovu watoto wa kitanzania hasa wale wa kipato cha chini maana wenye uwezo hawatakubali kuona watoto wao wakipotezwa hivihivi.

Mkakati huo ulianza kwa kuondoa mitihani hii ya kitaifa
-Waliondoa mitihani ya darasa la 4 iliyokuwa inamwezesha mwanafunzi kufanya vizuri ili aende darasa la 5
-Waliondoa mitihani ya kidato cha 2 iliyokuwa inamwezesha mwanafunzi kufanya vizuri ili aende kidato cha 3

Nashawishika kuamini kwamba mkakati huo unalenga kuwanufahisha watoto wa wenye hela maana wao watasoma shule nzuri na hata watakapo kutana na wenzao wa familia za kimaskini maana hao ndo watalazimika kufuata huo mfumo kwenye empoyment lazima watawazidi kwenye vigezo vya ajira maana wamepikwa vizuri zaidi kwa kila nyanja. Wataweza kujieleza na kufanya vizuri assignment watakazopewa wakati wa interviews vizuri zaidi. Maana yake ni kwamba nafasi zote nzuri zitashikiliwa na wale ambao walipata elimu bora na sio bora elimu. Na wale wengine watabaki kuwapigia mogoti, makofi barabarani na kuwasafishia ofisi na magari yao.
Mwl. Nyerere aliwahi kusema hivi 'lengo la elimu yetu si kupata watu kwenda chuo kikuu' kwamba kitu cha msingi si kufika ngazi flani ya elimu lakini elimu hiyo inakusaidiaje wewe na jamii yako. Lazima Magembe atambue hilo. Lengo sio kuwa na watu wengi waliohitimu form 4 lakini je uelewa wao na utendaji wao unaendana na kidato chao? Vinginevyo tuwapatie basi wanao maliza darasa la 7 certificate za form 4. Si tunataka wengi wafike form 4!
Kama kweli Magembe anataka kuwasaidia watanzani kwa kutengeneza shortcut hiyo tumlazimishe yeye na watendaji wengine kwenye wizara yake wawapeleke watoto wao kwenye shule za serikali mahali popote nchini ila sio private na tulisimamie hilo.
Hatuwezi kuwaacha watu wanaharibu elimu ya watoto wetu wakati watoto wao wako salama.
Nadhani ni wakati muuafaka wa kutunga sera itakayowalazimisha viongozi wetu wa ngazi zote na familia zao kutumia huduma zinazotolewa serikali ndani ya nchi kama elimu na afya ili waweze kuzisimamia vizuri na kwa umakini kwasababu zitawagusa na wao pia.

MAGEMBE KWAHILO UMEAHIBISHA ELIMU YAKO.
 
Back
Top Bottom