Naishi na virusi vya ukimwi natafuta kama mimi

Amalia

Member
Feb 9, 2012
6
10
habari zenu wana jamvi la "great thinkers". mimi ni mgeni kabisa katika jamvi hili na ni mara yangu ya kwanza kuweka post yangu hapa, japo ni msomaji sana wa JF lakini kama mgeni.
kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu, mimi ni mama 40+ naishi na virusi ya ukimwi. ningependa kupata mwenzangu wa kuanza maisha pamoja kama si kumalizia pamoja. lakini ambaye atakua tayari kutumia zana wakati wote wa mahusiano yetu ili kuzuia uambukizo mpya. nina maisha yangu na ninajiweza. ninajua wako wengi wenye hali kama mimi na ni wapweke na wangetamani kupata wenzao, ila sababu ya kuepuka maneno, kunyanyapaliwa na kunyooshewa vidole unaamua kujificha na kuishia kujifungia ndani wakati sio mwisho wa maisha. hali yangu hakuna anayeijua zaidi ya mimi na daktari wangu. naomba yoyote ambaye atakua interested ani PM kisha tufahamiane zaidi. Mimi makazi niko MOrogoro. Nisingependa malumbano maana hata wewe utakayelumbana na mimi afya yako huijui, ni bora mimi najijua na nafahamu jinsi ya kuishi.
mwenye maswali, yanakaribishwa, ni PM nitajibu. Jioni njema na Ijumaa njema wote wana JF.
 
kwakuongezea, naomba mtu ambaye yuko very serious. sio tuwasiliane for sometimes halafu utake tuonane only kutaka kujua nafananaje. muonekano wangu, huwezi kunijua kabisa. nina muonekano mzuri ambao unaweza kudhani natania kua ni muathirika, lakini ukweli ndio huo. naomba maswali mengi yatumwe kwenye inbox yangu maana najua hapa wengi mnachojua ni kudhalilishana.
 
na mie nataka ndoa, ndio maana nimekuja jamvini. inshallah wote wana JF lazima niwaalike kama atapatikana hapa.
 
Kila la heri katika uteuzi wa mweza wako.Nimependa sana mawazo yako umeonyesha ubinadamu wa hali ya juu sana
 
na mie nataka ndoa, ndio maana nimekuja jamvini. inshallah wote wana JF lazima niwaalike kama atapatikana hapa.
Kwakuwa nipo Moro najua nitashiriki kwenye maandalizi ya harusi hiyo shaka ondoa
 
Kil la kheri dada, maana kwa hali jinsi ilivyo ni wachache kama wewe wenye moyo kama wako.
 
Hongera sana kwa kutambua hali yako ni kweli wengi hatujui afya zetu,nakutakia maendeleo mema ya kutafuta mwenza!!!
 
Dada hongera sana, ni kweli kwa halli ya sasa huo ni ugonjwa wa kawaida kabisa na unadhibitika na unaweza kuishi tu maisha kama kawaida....tu.
Kila la kheri..mdada, nakukubali vibaya!
 
hongera dada. Mungu akujalie na kusikia ombi lako. Hakika utapata mwenza usihofu. Ubarikiwe sana.
 
Shariti la Jf mpaka ufikishe 5 post ndo um- pm mtu. So mimi sijafikisha hizo post,hivyo inakuwa ngumu kuku pm,na am so interested with You!
Tuwasiliane basi kupitia sweetrwabu@gmail.com
am serious!
 
Pole sana mama..sikunyanyapai ila ushauri wangu ni kuwa ungetakiwa kutafuta mtu ambaye naye ameathirika hapo ndio mtaishi kwa usalama zaidi.ila ambaye hajaathirika na kusema kuwa mtatumia mipira for the whole of your life sina uhakika.ningependa uwe na maisha mazuri na wanaokuzunguka wasikubague kabisa ,thats my wish to you
 
Back
Top Bottom