Naishi na mke ambaye sina mapenzi nae nifanyeje?

ushauri ni kwamba kama kweli unahisi hutaweza tena maisha yako yote kumpenda kwa dhati muite na kisha mwambie ukweli ulivyo na mpe uhuru wa kumake comment then fanyeni maamuzi ya kishujaa kama vile kutengana kijasiri bila kuona jamii inayowazunguka itawonaje maana wakati mwingine ukiogopa sana wanadamu utabaki wewe ndo unaye sumbuka kila leo angali wao wakilala na kuamka na mapenzi moto moto ili hali yakwako yamepoa kama barafu.
 
mi napenda kujta MAPUNGUFU ALIYONAYO kabla sijashauri lolote mana isijeikawa mapungufu yenyewe ni hajui kupika,anakojoa kitandani nk.
 
Mkuu, au ww ndo ulimwachisha shule? Kama kweli, dhambi itakukaa maisha. Kama sivyo, fanya tu namna ya kuachana naye lest akakuzalia tena. By the way, tunda mwala??

kama hawapendani haliwezi kuwa tunda tena. Sema kijitunda.
 
Wanaume bana! Kipindi mpo wote kijijini ulikua unamuona mrembo wa kijiji baada ya kuja mjini ukakutana na wasomi+warembo zaidi yake unamuona hafai, shame on you!
 
LOVE IS ALL ABOUT KIND ACTIONS.................... USIISIKILIZE SAUTI HASI NDANI YA MOYO WAKO. MFANYIE MATENDO MEMA TARATIIIIBU, NAYE ATAANZA KUJIFUNZA.Kumbuka Love is how you create it. Umempita kwa kiwango kikubwa sana cha elimu. Hii ni advantage kwakoo ya kuweza kumsaidia. Una exposure kubwa, ku interact na watu, kusoma love articles, internet etc. Tumia mwanya huu. Na kikubwa uwezo wako wa ku-manage stress ni mkubwa.Think of your baby.............. na kikubwa all smart women you see on the streets, offices etc si kwamba wote wanafurahia maisha ya ndoa as you see their outlook. Is all about emotional marturity........... Be one of them. Show kind actions to you parter and at last utaanza kumpenda tena kama ulivyokuwa mwanzoni.
 
baada ya kuja udsm ukasoma soma ukaona visista du uliporudi kijijin ndo ukaanza kumuona hafai na ukaanza force moyo wako ukubariane na tamaa zako kuwa ana mapungufu ili mradi upate sababu ya kumwacha. Ina maana wakati unampanda mpaka akapata mimba hukuona kuwa ana mapungufu mpaka baada ya wewe kuja dar? Na umeongelea kuhusu eti mmepishana elimu sana so hiyo ndiyo sababu au?
Mnapenda sana ngono lakini kuzaa hamtaki jaribu basi kutumia hata kinga sio mnawamimba watoto wa watu halafu mnaanza ooh ilikuwa bahati mbaya siyo chaguo langu mnawaacha hawana thamani wanaangaika wakitafta wakuwaoa.
Ukweli ni kwamba mwanamke akishapata mtoto anapoteza asilimia 90% ya kupata mume wa kumuoa so ukimimba umuoe.
Ndo hayo tu
 
Mkuu hiyo ni kawaida na nilitegemea.

Status yako ya Elimu na maisha imebadilika sana toka ulipoachana naye na sasa unajikuta uko katika level tofauti ya maisha wakati yeye akiwa level ile ile.

Bado unayo nafasi ya kutengeneza mambo kabla hujafanya maamuzi ya kuachana naye.

1. Kila mtu anao uwezo wa kupenda. Kupanga ni kuchagua. Dhamiria kumpenda no matter what na jitahidi kumfanyia matendo mema huku ukimrekebisha mapungufu yake.

2. Mpeleke shule hata za ufundi stadi au chuo na ikiwezekana mfungulie mradi ili scope yake ya maisha iendane na yako.

3. Mpendezeshe na kumbadilisha awe mwanamke wa ndoto zako.

4. Ongea naye juu ya mapungufu yake na vipi unapenda awe.

5. Kumbukaa bado unaweza mwanamke unayedhani unampenda lakini ukija ishi naye bado ukaona ana mapungufu. Binadamu ndivyo tulivyo. Tujifunze kuwapenda hata wale ambao mioyo yetu inadhani haiwapendi. In fact vitabu vya dini vinakwenda mabli zaidi kuwa wapendeni adui wenu na muwaombee. Itakuwa mke?
 
wanaume wengi wanaona mapungufu ya mwanamke hasa pale wanapowazalisha but kabla ya kumbebesha ujauzito ulikuwa unamuona queen, huna lolote umewaona vimodo wa UDSM ni wazuri sana na wakijijini amechoka hata mafuta mazuri hapaki unamuona ana mapungufu yake sasa basi tuweke wazi huyo msichana ana mapungufu gani?
 
kazi kweli kweli.............

Anyway mapenzi hayalazimishwi....

Mkataa pema pabaya panamuita....


Fuata ushauri wa The Boss, bila kusahau umpe mtaji na pesa ya matumizi kwa mtoto.........

Ila baadae akipendeza usimtamani.......
 
Last edited by a moderator:
umeishakutana na wamjini wamekuchanganya,ila kumbuka ipo siku utamkumbuka uyo unaomuana ana mapungufu,what goes around,comes around,baada ya kuchakachua sana ndio umeona ana mapungufu
 
  • Thanks
Reactions: LD
Pole kaka. Uzuri bado hamjafunga ndoa lakini kuna mtoto hapo anayewaunganisha. Bora kutengana naye ingali mapema kuliko kuendelea naye huku huna raha katika ndoa. Itakuwa kosa kubwa sana kufanya hivyo. Mkalishe chini umueleze yanayokusibu na amini atakuelewa hata kama si sasa huko badae ataelewa. Usipoteze muda.
 
Ah bora hata kuna watu kama Platozom.Kama hupendi waambie marafiki zako wa karibu wamchukue then utafarijika.Hakuna malaika mrekebishe utachukua wangapi na maradh haya?
 
Watenda dhambi kwan hata biblia inasema kuish na mwanamke usiyempenda ni dhambi kwani hutomjari kama inavyopaswa
 
Watu huwa tunakimbilia kusema mapungufu ya wenzetu.. Ina wezekana wewe ndio mwenye tatizo baada ya kuona umepata hako ka elimu ka chuo ndio unaanza kumuona mwenzio ana mapungufu... Si ajabu dada wa watu anakuvumilia, wewe kwa nini ushindwe kumvumilia??? Nway, ukishindwa usijilazimishe kaka, fata ushauri wa The Boss.
 
  • Thanks
Reactions: LD
yani katika posts nizosoma umu,hii ni kiboko mana nimeshindwa shangaa,kuamini,kustaajabu,kusikitika ata sina lugha ya kueleza navojisikia
 
Duh! nimechoka kabisa kwa hili swala lako mkuu ila ngoja nikwambie kitu wewe hukuwa na upendo wa kweli kwa huyu binti its like mechi ya mchangani ikazaa bao ukaona mchezaji anakiwango kumbe bao laweza hata kubahatishwa pia skills and tekniks zina matter sana tu.

ngoja nikwambie kuna mtu mmoja ambaye aliwah kufunga mechi za mchangani ila alikuwa shule kama wewe na kama kawaida shule kwa binti ikaishia hapo. baadae alipokuja chuo na kusoma akapata kazi alioa mtu tofauti ila akamwambia ukweli kwamba anaye kid wa mashtuzi. Uzuri huyu mkew alikubaliana na lile na kwakua fair kabisa huyu mama alilazimisha mtoto aletwe toka kijijini ili amlee yeye kisha mke wa huyu jamaa akatafuta hela akampa yule mama mzazi wa mtoto wa mashtuzi kama mtaji.

yaani huyu mama mashtuzi na mke halis wa huyu jamaa wanapatana na mtoto analelewa vizuri kuliko kawaida kwa huyu baba. so ungekuja mapema ningekushaur hivi ila kwa sasa mshape hadi awe kama utakavyo wewe uish naye.
 
mleta mada,icho kipenggele cha elimu,kiondoe mapenzi ayana kiwango cha elimu,cha msingi maelewano na upendo
 
mimi naona wewe ndo unamapungufu kwani hadi ukapata huyo mtoto ulimpata kwa barua ulikula usichojua kama kina chumvi na sukari pambana umeshampotezea mwenzako ramani na je huyo mtoto ataishi maisha ya namna gani kama vile hana umuhimu anabebwa na mahisia ya wazazi utajuta mwanao atakulia na tabia hizo za mama yake ambazo dawa si kukimbia ni kurekebisha very sn mwanao ataletwa hapa na mchumba wake kwa lawama hizihizi
 
Back
Top Bottom