Elections 2010 Naikumbuka kauli hii ya KIKWETE

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,720
155,326
View attachment 11955RAIS Jakaya Kikwete ameushangaza umma wa Watanzania baada ya kuanza kukiuka misingi iliyokiunda Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kuwaheshimu Wakulima na Wafanyakazi pale alipokutana na wazee wa MSkoa wa Dar es Salaam na kutoa hotuba kali akiwashutumu viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafabnyakazi Nchini (Tucta) kuwa ni wanafiki kwa kuendelea kushinikiza mgomo wa wafanyakazi licha ya mazungumzo yanayoendelea kati yao na Serikali.

“Hawa viongozi wa Tucta walisema sisi serikali ni watu wasioambilika… hawa viongozi wa Tucta ni waongo,” alisema Rais Kikwete akisisitiza kuwa hii ni moja ya sababu iliyomfanya jana awajibike kujibu.

“Sasa iweje tunakubaliana hili, kesho yake asubuhi unazungumza kama hatujakubaliana,” alisema Rais na kusisitiza: “Ninayo kila sababu kuhoji dhamira zao iwapo kweli wana nia thabiti ya kuwabeba wafanyakazi ama wana lao jambo.”
 
Nadhani wafanyakazi wa Tanzania wako katika lile kundi la 70% ambao ni mbumbumbu na hufuata mkumbo, ndo maana JK alisema hivyo with confidence!

Ukweli wote tutauona mara tu baada ya Oktoba 31.
 
Back
Top Bottom