Naihurumia CHADEMA kwa malumbano.....

Timueni tu.
Hapakosi watu wa kuokota mbao za vipande vya CHADEMA iliyovunjika vunjikia baharini

Hapo nilipoweka red sijapaelewa. Je! Unamaanisha mwili wa CDM kuvunjika na kutupwa baharini au unamaanisha mwili wa kiongozi aliye hovyo kuvunjwa na masalia yake wakang'aniana vyama vingine?
 
CHADEMA will soon go six feet under. Series of events show that this NGO is completely debilitated and suffers from political hypoglycaemia. However, CCM is sincerely thanking you for showing, at least a modicum of opposition during your life time. RIP in advance Mr. CHADEMA
 
CHADEMA will soon go six feet under. Series of events show that this NGO is completely debilitated and suffers from political hypoglycaemia. However, CCM is sincerely thanking you for showing, at least a modicum of opposition during your life time. RIP in advance Mr. CHADEMA

Only if wishes were horses................................!
 
Kama Shibuda ana misimamo bnafs ni bora akazane katba iruhusu mgombea bnafs.CCM wamemshindwa CHADEMA watamweza?????. CDM TIMUA HUYO MNAFIKI>
 
Hakuna haja ya kuwa na vyama vya siasa au mfumo wa vyama vingi kama chama hakitachora mistari. Kama chama hakitajipambanua kinasimamia nini. Jukumu la kulinda mistari na kuwawajibisha wanaovuka mistari ni la wanachama na viongozi. Mistari sio kuviza demokrasia, ina lengo la kutengeneza mipaka ili demokrasia ifanyike vizuri.

Kwanini tuwe na vyama vingi kama kila mtu ktk chama fulani anaweza kujisemea lolote? Kwanini tusiwe na chama kimoja cha siasa nchini halafu tukaruhusu kila mtu aseme lake-huyu ubepari na yule ukomunisti? Kitu gani kinakitofautisha chama kimoja na kingine? Tusilee ghasia ktk vyama kwa kisingizio cha demokrasia. Demokrasia sio domokasi.

Watu wanadhani demokrasia ya nchi kama USA imekuwa kiasi kwamba unaweza ukasema na kufanya lolote na chama kikakuacha tu. Hii si kweli. Kuna congressman kajiuzulu kwa kuwatumia picha zake za utupu vijana wa chuo(sexting), chama kilimshurutisha ajiuzulu. Hivi kweli unaweza ukaanza kupiga kelele za kutaka kuwepo haki za mashoga na wasagaji ukiwa republican? Democrats na republicans wana vitu vya msingi vinavyowatofautisha, kiasi kwamba pamoja na demokrasia, huwezi ukafanya tofauti na msimamo wa wazi.

Wanomtetea Shibuda bado hawajaweza kuonyesha hoja za msingi ili asiwajibishwe kwa alichokifanya. Mbaya zaidi, Shibuda anaongea kwa jeuri, tena bungeni-sio kwenye chama au party caucus. Kama Shibuda hawajibishwi, sioni kama chama kitakuwa na mamlaka ya kimaadili ya kumwajibisha yeyote iwe mwizi wa mali za chama, msaliti wa chama n.k. Hivi tunajua ni kwanini CCM imefika hapo ilipo? Au tunadhani CCM ni bi mkubwa na CDM ni bi mdogo na ndio maana anapendwa zaidi na wananchi kuliko CCM?
 
Malumbano ya hoja yasiyo na uvumilivu na yaliyojikita katika kuenguana hayawezi kukisaidia CDM.

Watakao iua CHADEMA ni wanachadema wenyewe kwa kuwashinikiza viongozi wetu kujenga moyo wa kufukuzana na kusemana hovyo hovyo. Leo utasikia Shibuda, kesho Zitto, baada ya muda Mh Godbless hatumwelewi!!

Mara zote hauwezi kujenga amani na umoja eti kwa msingi wa kufukuzana na kusemama hovyo.

Kwa mfano, issue ya Shibuda: Kwanza lazima tuelewe mtu mnayesema ni mamruki, Shibuda. Huyu ndg move yake ya kuhamia CDM imetokana na kuenguliwa ktk kura za maoni za CCM 2010. Na sababu kubwa ni kwamba alikuwa ni mtu wa kwanza kabisa kujitokeza hadharani kutangaza nia ya kumpatia JK changamoto ktk kura za maoni ndani ya CCM kwa post ya URAIS . Ndiye aliyeonekana katika TV ya Mlimani akihojiwa na ndg Damu-Mbaya kwa lengo la kutangaza nia. Baada ya kufanya hivyo, Makamba aliweka wazi kwamba CCM itamsimamisha JK, anayetaka kugombea urais atafute chama kingine lkn kwa CCM NO!

Kwa hiyo, si kweli kwamba huyu ndg ni mamluki. Wana CCM nao walimng'oa baada ya kuona kwamba anataka kuleta mvutano usiokuwa wa lazima ndani ya chama kwa habari ya mtu wa kumsimamisha kugombea kiti cha URAIS. CCM nayo haimtaki!

Nini kifanyike kwa Shibuda: Ninachokiona kwa shibuda ni dalili za frustrations, ambazo zinatokana na kushindwa kuelewa hatima yake iko wapi kisiasa! Ikiwa CDM mtamfukuza mjue atahamia chama kingine cha upinzani na wala si kurudi CCM. Hata ikiwa atarejea CCM hana jipya zaidi ya kukalia benchi. All in ALL kuna mambo mengi mazuri ambayo CDM inaweza kujipatia kutoka kwa Shibuda, moja kubwa likiwa ni moyo wa ujasiri wa kudiriki kufanya au kusema kile anachokiamini. Pengine, anahitaji msaada wa kisaikolojia tu kuweza kumfanya kuwa na mfumo wa ku-consult wakubwa wake kabla hajatoa contradicting statements,
hasusani msimamo wa chama unapohitajika. Nadhani kumfukuza si jambo la kujenga.

Mkuu mimi najua sakata la Shibuda ni kuhusu posho. CHADEMA hawana msimamo wowote kuhusu posho kwa hiyo Shibuda alikuwa sahihi tu kusema ukweli ambao ni ukweli walionao wabunge wengine wa CHADEMA lakini wanaogopa kuusema. Hapa Shibuda alionyesha tu kwamba si mnafiki na kweli huyu jamaa huwa si mnafiki ila ndani ya CHADEMA kumejaa wanafiki hasa linapokuja suala la posho ambalo kwalo wanataka kumsulubu Shibuda. Kama wana msimamo thabiti na wanavutwa na dhamira ya kuzikataa posho mbona hawajawasilisha barua kwa watendaji wa Bunge ili kuzikataa hizo posho?
 
Back
Top Bottom