Naibu Waziri Tizeba atishia kumuua Kaka yake, Kisa tofauti za Kisiasa

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,564
7,970
UGOMVI wa kisiasa kati ya ndugu wawili wa familia moja, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba(ccm) na kaka yake Adrian Tizeba(Chadema) umechukua sura mpya baada ya kutishiana kifo.

Akizungumza na gazeti hili jana, Adrian alisema kuwa tangu ahame CCM na kujiunga na CHADEMA, mdogo wake huyo amekuwa akimbambikizia maneno mabaya yaliyoleta uhusiano mbaya katika familia yao.

Alidai kuwa naibu waziri huyo aliwahi kumwambia mama yao mzazi aseme kwamba Adrian aliwahi kumbaka.

Alisema kuwa hayo yote yanasemwa ili afunguliwe mashtaka na kufungwa.

Adrian aliongeza kuwa baada ya uchaguzi mdogo wa madiwani katika ya kata ya Lugata ambapo naibu waziri huyo alimtumia mama yake kuendesha propaganda chafu dhidi yake, sasa amebambikiziwa tuhuma mpya.

Alisema baada ya uchaguzi huo alibakia katika kata hiyo iliyo kisiwani kwa lengo la kuendelea na kazi za kisiasa, lakini naibu waziri amembambikizia kesi kuwa anazuia mgambo kufanyika katika eneo hilo.

Hali hiyo imesababisha polisi na wanajeshi kumsaka kwa nguvu ikiwemo kumtengenezea shtaka la wizi wa kutumia silaha.

Alifafanua kuwa siku za karibuni kwenye kata hiyo kumekuwa na kitendo cha kulazimisha vijana kushiriki mgambo bila hiari yao.

Alisema kuwa katika kutengeneza sababu ya kuwabana, polisi walitumia vurugu za tukio la kijana Emanuel Joseph kunyang'anywa baiskeli yake na wakufunzi wa mgambo wakidai kuwa vijana walimpiga mkufunzi na kuchaniwa sare za jeshi.

Alipotafutwa Naibu Waziri Tizeba kujibu tuhuma hizo za kutishia kumuua kaka yake alisema hayo ni masuala ya familia ambayo hayana nafasi ya kuandikwa katika vyombo vya habari.

"Ninashangaa kila kunapotokea kutoelewana kati yetu huyu kaka yangu anakimbilia kwenye vyombo vya habari wala sio kwenye familia wakati bado tunaye mama yetu mzazi ambaye anaujua vema mgogoro wetu.

"Mimi naona anafanya hayo akidhani kuwa angeweza kuniua mimi kisiasa lakini suala hilo halitawezekana," alisema Tizeba.

Source: Tz Daima.

MY TAKE:
Inaonekana sasa viongozi na wanachama wa ccm wamechagua njia ya kuua tu dhidi ya wapinzani wao kisiasa. Ni wiki iliyopita tu meya wa manispaa ya Ilemela amemtishia kumuua mbunge wa Ilemela mbele ya mkuu wa wilaya na mkuu wa polisi wilaya ya Ilemela lakini hakuchukuliwa hatua yoyote. Hali hii isipodhibitiwa haraka basi watanzania tujiandae kuingia vitani muda si mrefu.
 
Hii ni hatari,

Naomba Watanzania wenzangu msipuuze hili lililojitokeza ili mpime kiwango kibaya kisiasa tulipofikia.Kama kwasababu tu ya CDM na CCM ndugu wanataka kuuana vipi wewe wa pembeni?

Wanasiasa muogopeni Mungu na jueni maisha ya kisiasa ni mafupi kuliko maisha ya kiumbe chochote duniani,mliona ilichukua dakika ngapi Lowasa kuanguka tena akiwa waziri mkuu! Acheni tamaa za kisiasa hadi hamuoni dhamani ya utu.

Tulipofika hakuna atakayekuwa salama uwe CDM au CCM hata kama wana dola.Turudi kwenye kuheshimiana na kuwajibishana bila kuangaliana usoni ili wananchi waone haki inavyofanya kazi.
 
.....

......ndugu yako wa Damu kisa yuko Chadema sembuse mimi....Naunga mkono Red brigade!!!!!

Hili bilaa sasa maana akimtishia ndugu yake au kama anauwezo wa kumfanyia hivyo ndugu yake wa damu itakuwaje wewe mtu baki? Sasa naanza pata picha kwanini watu wananunua sana manati ya mzungu
 
Ee Mungu tujalie roho ya Imani, Matumaini and Mapendo baina yetu. Zishindwe roho chafu katika nchi yetu. Amen

Ni kuwa wapole na kupambana na hali iliyopo sasa .....Ila naamini Mungu atakuwa upande wetu na kuwaondoa wabaya wote
 
Du mi kaka yangu ni askar, nina mashejej 2 askar, wananitonya kila siku kuwa ccm imeoza na inatumia jesh kwa maslah yake.kashaur mabadiliko kwenye katiba yaguse vyombo vya dola, hapo mbivu na mbovu zitaonekana.na wamechoka kutumiwa tatizo ni mfumo,ukiacha jesh wanakufatilia kwa kila kitu.wameamua kubaki tu jeshin kishingo upande.
 
...Tundu Lisu jana alisema - Hizi zote ni dalili za mfumo unaomong'onyoka. Tutauliwa sana, tutapigwa mabomu sana, tutashitakiwa sana,.........
 
Maccm ni majinga kweli ni majizi tupu.Yaliyosoma na yasiyosoma,yaliyofaulu na yaliyofeli elimu za darasanani yote yanaamini siasa ndio maisha na pumzi ya binadamu,na hakuna life nje ya siasa.Ndio maana upinzani wowote wa kuwatoa ktk siasa wao wanachukulia ni kutangaza vita na mauaji ni sehemu ya survival.

Mentality km hizi haziwezi komboa nchi masikini kam yetu.HUyo si wa kwanza ktk CCM kutumia vitisho, mauaji kwa wana familia kwa sababu za kijinga kabisa za kisiasa.Kwani hajui kuwa kuna viti maalumu na km JK anamuona kuwa anafaa si anaweza mteua km mbatia na kumpa uwaziri bado.Kwanini hayaoni nafasi ya kugombea kupitia maeneo mengine au kukubali kushindwa au hata kuhama chama mapema ili wakajenge CV miaka ijayo wawe ktk nafasi ya kugombea ktk chama kinachouzika.


Pia si lazima washinde au hata kuhsindwa pia ni ushindi kw amtu aliyeshindana na kushindwa kwa haki.Je wakija watu wababe wasioweza uwawa kijinga nao wana uwezo wa kumuua yeye angefanya nini?
 
Mama mzazi naye anakubali kusema kwamba mwanae amembaka wakati si kweli?

Katika mambo ambayo imeniwia vigumu kuyaamini ni hilo la mama kukubali kumpakazia mwanae kuwa amembaka! Lakini kama alivyosema hapo juu Kongosho inawezekana naibu waziri ndiye bread winner kwahiyo mama mtu amelazimika kumsikiliza na kufanya analotaka hata kama anajidhalilisha yeye mwenyewe.
 
Last edited by a moderator:
Katika mambo ambayo imeniwia vigumu kuyaamini ni hilo la mama kukubali kumpakazia mwanae kuwa amembaka! Lakini kama alivyosema hapo juu Kongosho inawezekana naibu waziri ndiye bread winner kwahiyo mama mtu amelazimika kumsikiliza na kufanya analotaka hata kama anajidhalilisha yeye mwenyewe.

heshima kwako kamanda.........ki ukweli hili tatizo ni la wengi....(mimi mwenyewe nikiwa muhanga).....lakini kwa sababu nina jazba ya mageuzi....nitaenda nalo mdo mdo........ki ukweli ni tabu kuu.......
 
Na ndio Wasomi walioaminiwa na Watanzania wawaongoze,Huyo jamaa una udokta wa nini?Wasomi wa Kibongo bana tabu kweli kweli.
 
  • Thanks
Reactions: kui
heshima kwako kamanda.........ki ukweli hili tatizo ni la wengi....(mimi mwenyewe nikiwa muhanga).....lakini kwa sababu nina jazba ya mageuzi....nitaenda nalo mdo mdo........ki ukweli ni tabu kuu.......

Pole sana kamanda wangu mimi nipende tu kuku-encourage kwamba kwa sisi tuliochagua kuwa mstari wa mbele kupigania mageuzi lazima tunakumbana na changamoto mbalimbali nyingine kutoka katika familia zetu lakini tukiendelea kuwa imara hatimaye mafanikio yatapatikana kwakuwa hapa tulipofikia ni laana kwetu na vizazi vyetu kama tutaamua kuwa wasaliti wa nafsi zetu.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom