Waziri Mulugo: Tanzania ilitokana na muungano wa visiwa vya Pemba na Zimbabwe

Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,143
3,196


Duh, Mulugo analiaibisha Taifa, Tanzania ilitokana na muungano wa visiwa vya Pemba na Zimbabwe.... nani amemuandalia huyu hii hotuba? Mungu wangu, anakuwaje waziri wa Elimu huyu ilihali yeye mwenyewe Elimu yake ina walakini? Hawezi hata kulocate Zimbabwe katika ramani ya dunia?


Update: Kuna makosa mengi ukiachilia mbali hilo la Zimbabwe. Katika speech yake anaanza na Tanzania ilizaliwa mwaka one nineteen sixty four. Wewe unaifahamu hiyo 1-1964? lakini cha ziada anasema NACTE inaoffer master na PhD. Wewe unaifahamu NACTE ni nini? NACTE inatolea wapi hizi degree? Yaani at the level of waziri wa elimu huwezi kutofautisha NACTE, TCU na vyuo vikuu? What are you doing katika wizara ya elimu kama vitu vidogo kama hivi kwako ni shida?

Kwa level ya waziri wa wizara ya elimu alitakiwa awe na uwezo wa kufafanua vizuri nini ni nini katika elimu ya Tanzania. Kwa watu ambao hawajui NACTE ni nini wanaweza kudhani ni chuo kikuu. Na wengi watakuwa wanashangaa sana kwamba ni chuo kikuu gani hicho kinachopigiwa chapuo kiasi hicho na Naibu waziri ilihali kuna vyuo vikuu vingine vingi nchini vinavyo award hiyo master na PhD. Ulikuwa ni wajibu wake ku-define NACTE na kueleza Institution zinazounda NACTE na namna ambavyo NACTE inafanya kazi ya kuassure quality ya hizo institutions, na si ku award Master na PhD.


======
Media yaandika:

Waziri aiaibisha serikali

-Asema Tanzania ni Muungano wa Zimbabwe, Pemba na Tanganyika

na George Maziku|Tanzania Daima

NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, amemwaibisha Rais Jakaya Kikwete na taifa kwa ujumla mbele ya jamii ya kimataifa, baada ya kuitangazia dunia kuwa Tanzania imetokana na muungano wa visiwa vya Zimbabwe na Pemba vilivyoungana na Tanganyika.

Mbali na hilo, aliwaambia mamia ya wajumbe kutoka mataifa mbalimbali katika Bara la Afrika kuwa, Tanzania ilizaliwa mwaka 11964.

"Wasilisho langu litakuwa na sehemu saba; Utangulizi, Tanzania iliundwa mwaka 11964 kwakuunganisha visiwa vya Bahari ya Hindi vya Zimbabwe na Pemba vilivyoungana na nchi ya Bara iliyokuwa ikiitwa Tanganyika" alisema Naibu Waziri Mulugo kwa kujiamini na bila kuonyesha dalili yoyote kuwa alikuwa amekosea.

Naibu waziri huyo alikuwa akiwasilisha mada katika mkutano wa viongozi na wataalamu wa elimu katika Bara la Afrika, ambao ulifanyika Afrika Kusini kuanzia Oktoba 5-7, mwaka huu.

Kuboronga huko kwa Naibu Waziri huyo kumeibua mjadala mkubwa na mzito miongoni mwa Watanzania wa kada na rika mbalimbali, huku wengi wakianza kupata wasiwasi juu ya uwezo wa watu wanaoteuliwa na Rais Kikwete kushika nyadhifa mbalimbali serikalini.

Watu wengi waliotoa maoni yao juu ya suala hili kupitia mitandao ya kijamii ya Jamii Forums, Facebook na Twiter wameonyesha wasiwasi mkubwa na kiwango cha elimu na weledi wa Mulugo na kuuliza swali; "Elimu ya Waziri huyu inatosheleza kumudu majukumu yake ya Naibu Waziri wa Elimu?"

Wasifu wa Naibu Waziri Mulugo uliopatikana kupitia mtandao wa Google, unaonyesha kuwa ana elimu ya shahada ya kwanza aliyoipata kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, kati ya mwaka 2002 na 2008.

Anadai katika wasifu huo kuwa kabla ya kuingia chuo kikuu, amesoma katika shule za sekondari za Songea Boys High School kwa masomo ya kidato cha tano na sita kuanzia mwaka 1994 mpaka 1996, na Sekondari ya Mbeya kwa masomo ya kidato cha kwanza mpaka cha nne kuanzia mwaka 1990 mpaka 1993.

Mulugo amejieleza kuwa kati ya mwaka 2000 na 2004 alifanya kazi ya ualimu katika Shule ya Sekondari Southern Highland, huku akiwa hajapata mafunzo yoyote ya taaluma ya ualimu.

Alipotafutwa kwa njia ya simu kufafanua alivyojieleza, Waziri Mulugo alisema alikuwa mjini Dodoma kuhudhuria kikao cha Baraza la Mawaziri, hivyo hakuwa na muda wa kuzungumza na gazeti hili.


mulugo.jpg

Picha kwa hisani ya global publishers
 
Last edited by a moderator:
Nimeisikiliza nimecheka sana. Utafikiria ni Zekomedi!!!!!
Haha, jamaa hata English yake tu kichekesho. Full comedy yaani. Kwa kweli nina wasi wasi sana na uwezo wa huyu jamaa, kuna siku niliwahi kualikwa kwenye ufunguzi wa kituo fulani hapa Dar, jamaa hakuongea chochote cha maana zaidi ya kutulazimisha tumpigie makofi. Nilikuwa namshangaa sana, how on earth unaweza kuwaambia wasikilizaji wakupigie makofi badala ya wewe mwenyewe uongee kitu cha kukufanya upigiwe makofi. Ningekuwa JK, huyu angeshaondoka kwenye uwaziri tangu siku aliyotoa speech hii!
 
Zecomedy
Hao ndio maprofessor wetu wa bongo. Ndio maana na Dhaifu hawezi kuongea chochote cha maana alifundishwa na akina Mulugo. Natamani niwepo kwenye mikutano yao ya baraza la mawaziri. Unatarajia nini kwenye elimu kama wazirii ndio huyo?? Sishangahi kuona wanamweka tena Dr Katunzi kwenye elimu yeye na Mungai walitoa vipindi vya science katika ssule zote za sekondari
 
Naaaaaaaah.... Naibu waziri (wa elimu)? Zimbabwe imetoka wapi Tanzania? Huo mkutano umefanyika South Africa, kuna ulazima gani wa Naibu waziri kuanza kusema Tanzania inapakana na nchi gani, anahutubia watoto wa darasa la kwanza?

Hii clip inabidi CABINET nzima ione, jamnani hakuna mtu aliyeipitia hiyo presentation kabla mheshimiwa hajapanda ndege?
 
Hii ndiyo bongo bwana, usishangae wakati mwingine ndo atakuwa waziri mkuu wetu. Nimewahi pia kumsikia kama mara mbili hivi, nikajiuliza sana kuhusu uwezo wake.
 
Ni kumshikia kidedea aondoke kwenye ofisi nyeti kama hiyo, JK ampangie kazi nyingine anatuaibisha sana. Hafai kwenye hiyo nafasi. Hope UWT wanaiona hiyo aibu, na watasaidia kufikisha ujumbe!!
 
hadi nimehisi kichefuchefu, ni kilaza mkuu kati ya mawaziri wote
yaani hata introduction anasoma hawezi kutaja muungano umetokana na nchi zipi
fun enough hata pronunciation yake ni ya utata nadhani amefaulu kwa kudesa.
a minister yewomi shame upon him kaliabisha taifa kajiabisha yeye na familia yake
kamwaibisha pia aliemteuwa,
 
Back
Top Bottom