Naibu Waziri Jafo, huu ni mtihani kwako...

structuralist

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
1,231
905
Wakati serikali ilipopeleka hoja (muswaada) bungeni kuhusu kuzuia fao la kujitoa wabunge wengi walikuwa wakali kupinga hoja hiyo.

Muasisi wa upingaji hoja alikuwa Mh Suleimani Jafo mbunge wa Kisarawe. Alitetea hoja yake na ukweli serikali nadhani ililegeza kamba kwenye hilo na watu wakafanikiwa kuendelea kupata withdraw benefits zao.

Leo hii serikali inaonekana kutaka kurejesha (kama bado haijafanya hivyo rasmi) utaratibu wa kuzuia fao hilo.

Kwa bahati nzuri aliyekuwa akilipinga wakati ule leo hii ni Naibu Waziri TAMISEMI mh Suleiman Jafo. Swali kwa Jafo ni kama kweli alikuwa na nia wakati ule ya kuwatetea watanzania je uko wapi msimamo wake leo hii?

Inawezekana jana alikuwa na msimamo lakini leo akageuka?

Kwa utaratibu wowote ule (najua unalinda pia kitumbua chako) ni ipi kauli yako na unafanya nini kupigania kile ulichokiamini kuwa hakikuwa sahihi toka mwaka jana?

Na kwa wale wabunge wengine walokuwawakipinga katazo lile ni nini kimetokea hatusikii tena wakiwa na misimamo ile?
 
Huyu hakuandaliwa kuwa waziri, huwa anajibu maswali kwa spidi kubwa huku akiongeza mambo yasiyo na muhimu katika kujibu swali husika. Leo NS amemwambia ajibu kwa ufupi akapoa sana kwani hajazoea. Hakika uongozi ni kipaji.
Hilo fao lakujitoa hawezi kulitetea tena.
 
Kweli mkuu kashakula shavu sasa hivi hawezi ona tena kuwa hili ni tatizo@mkambarani
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom