Naibu Waziri Elimu katika kashfa vyeti

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Philipo Mulugo anadaiwa kutumia ujanja katika wasifu na elimu yake ambapo katika maisha yake ya kielimu ametumia majina manne tofauti.Uchunguzi uliofanywa na gazeti la mwananchi umegundua kuwa mwaka 1988 alihitimu darasa la saba na alijulikana kwa jina la Philipo Augustine Mulugo na hakufaulu.Mwaka 1989 alirudia kwa jina la Hamimu Hassani katika shule ya msingi Rukwa mkoani Mbeya.Tena akabadili jina na kuitwa Hamimu Augustino wakati yupo Sekondari ya Mbeya Day mwaka 1990.Mwaka 1998 akaitwa Dickson Mulungo,jina la mwanafunzi mwenzie waliomaliza wote Sekondari yaSongea Boys ambaye alipata division two.
SASA HIVI HUYU MTU NI NAIBU WIZARA YA ELIMU WAKATI YEYE MWENYEWE NI BINGWA WA KUBADILI MAJINA NDIO MAANA WATOTO WANACHORA MAZOMBI.

source;gazeti la mwananchi la leo tarehe 25/03/2013.

ELIAS MSUYA wa gazeti la mwananchi ndiye mwandishi wa habari hiyo na amelipwa fedha na watu kadhaa kumchafua mbunge wetu tutapambana naye
 
Kwa kuwa mwandishi hakuficha jina "na mwandishi watu" basi hii habari ya kweli tena wapo wengi kama msako ufanye kwa wote ukienda bandari utalia
 
ELIAS MSUYA wa gazeti la mwananchi ndiye mwandishi wa habari hiyo na amelipwa fedha na watu kadhaa kumchafua mbunge wetu tutapambana naye
Mpelekeni mahakamani huko zitajulikana mbivu na mbichi. Mbona yule mzee Msemakweli na kitabu chake cha "Mafisadi wa Elimu" bado anadunda tu? #haibiwimtung'o
 
Watu sampuli ya naibu waziri Mulugo wako wengi sana ndani ya ccm kwakuwa huko ndiko usalama wao ulipo.

Lakini kwakuwa sasa mambo yake yamewekwa hadharani hana budi kujiengua mwenyewe, hana sababu ya kusubiri aenguliwe kwakuwa hii kashfa ni nzito sana kwake na kwa wizara ya elimu pamoja na serikali nzima.

Suala la yeye kurudia shule ya msingi si hoja sana lakini watetezi wake watambue kuwa hoja ya msingi ni yeye kutumia cheti cha mtu (Dick Mulungu) kujipatia ajira baada ya kufeli kidato cha sita na hivyo kuwanyima fursa waliostahili ajira hiyo.

Hivi huyo Dick Mulungu nae hana hatia katika sakata hili? Kwa kufacilitate kufanyika kwa makosa ya udanganyifu katika ajira ya Mulugo?



Mkuu acha kutuchekesha kihivyo. Yaani huyu ajiengue mwenyewe ili iweje...atakula wapi? Chukua hako Mapema ndiyo mmiliki wa maovu Tanzania. Mwanachi ukija kulalamika unatafutwa kumwagiwa tindi kali, huu si umafia jamani? Yaani manabii hawataki kuambiwa ukweli kisa wanataka kula na kufirisi nchi tu bila kujali watu wao.
 
Kila kukicha waovu wanazidi kujulilkana,hadi uchaguzi 2015 upite mtasiikia mengi sana.
 
Mpelekeni mahakamani huko zitajulikana mbivu na mbichi. Mbona yule mzee Msemakweli na kitabu chake cha "Mafisadi wa Elimu" bado anadunda tu? #haibiwimtung'o

ni msela wake fast jet mbaya.....
wanapiga wote madilli ya kumiliki maskuli.hakuna jipya hapo mbona magambani wapo wengi tu.....!
 
Hii ni kashfa kubwa inayopelekea kusimaishwa kazi,na kufunguliwa mashtaka.Angekuwa mstaarabu angejiuzulu kupisha uchunguzi au aliye mteua angefanya mabadiliko ya nafasi yake.
Kuendelea kuwepo madarakani ni Kuidhalilisha wizara.
 
Kama ni kweli, imethibitka basi watu wa dizaini hii mh! ni wengi sana katika hi siri kali. jamani wapeni nafasi za uongozi watu waliosoma na waadilifu sio kupeana vyeo kwa kujuana. WAPENI WATAALAM NA WAAMINIFU ILI TUPIGE HATUA.
watu wa namna hii hata nchi ibarikiwe mvua ya mafuta kila mkoa basi haiwezi kuendelea coz watakuwa hawana mipango thabiti na ya kisomi, kifikra na kimaadili katika uongozi.
Vihiyo mnaong'ang'ania ondokeni!!!!!
 
Waziri hana uhalali wa kuwa wizara ya elimu, N/Waziri hana uhalali...... Je, tutegemee nini?
Eh Mola tunsuru maana haya mashikaji mawili hayana hata huruma na taifa, ni full vilaza meeeeen
 
Mulugo namfahamu sana baba yangu alimfundisha shule ya msingi Rukwa kabla hajahamishiwa kapalala. Huyo mwalimu Nyoni aliyetajwa hapo alifundisha na baba yangu hapo Kapalala kabla hajahamishiwa huko Rukwa, mkitaka namba ya huyo mwalimu nyoni nitawapa namfahamu kwani alikuwa mcheza soccer mzuri sana wa namba tano na baba yangu alikuwa namba sita
 
Mbona ndani ya ccm wapo wengi?

Mmmh! ila serikali ikisema iunde task force kuchunguza vyeti vya watumishi wote wa serikali, mbona itakua kizungumkuti!issue ya vyeti ni ngumu sana na inaonekana wengi wametumia vyeti vya watu! kuna wakati jamaa chuo kikuu alipishana na mtumizi wa vyeti vyake, yeye kaja kuanza mwaka wa kwanza, mtumizi ndio anahitimu!balaaaaa!
 
Back
Top Bottom