Naibu Waziri Adamu Malima aibiwa kila kitu hotelini Morogoro!

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,971
1,650
Habari zilizopatikana sasa hivi zinasema Naibu Waziri Adamu Malima ameibiwa kila kitu ktk hoteli ya Loshera mjini Morogoro. Hadi sasa bado yuko ndani ya chumba cha hiyo hoteli hajatoka nje. Inasemekana hata nguo alizoavaa amesaidiwa tu na wasamaria wema.

Yaleyale ya mawaziri kuendelea kuumbuka ugenini!

Manjagu bado yanafuatilia issue hii nzima!

Source: Radio One, muda 13:14 pm

Hoteli yenyewe ndio hii hapa kama inavyoonekana

View attachment 48953

Hii hapa tena

View attachment 48954

kwa mlinzi getini

View attachment 48955

WAZIRI+MALIMA+KWENYE+KANZU..JPG
mbona dirisha lenyewe,halionekani kuvunjwa au forced entry?? au sio lenyewe??? nimeitoa kwa michuzi loh
 
Radio One inaripoti hivi sasa ya kuwa Naibu Waziri wa Nishati kaibiwa kila kitu katika hoteli aliyolala pale Morogoro mjini..........barabara ya kuelekea kwa Mkuu wa Mkoa................yaelekea kaibiwa na mtu aliyokuwa naye kwa maoni yangu........labda chapa mtu aliyekuwa akimpa maraha..................lol
 
tumesikia anadaiwa kwa mganga mmoja wa kienyeji ndiye aliyechora deal!
 
Ni breaking newz radio one,zimeeleza kuwa naibu waziri Nishati na Madini Adam malima Ameibwa kila kitu Hotelini morogoro.mwenye niuz zaidi atujuze
 
Nimeconfirm na kijana mmoja kwenye hiyo hotel ni kweli alilala hapo tangu juzi kwenye chumba cha exctv suite sh 400000 kwa siku tangu jana alirudi usiku kutoka club na dada mweupe mrefu na asbh kaamka kajikuta hana hata chupi katoka na taulo kiunoni!!hawa dada zetu wa club cjui vp amemkomba kila kitu waziri ni aibu Mkuu wa mkoa alienda kuokoa jahazi
 
Habari nilizozisikia mwenyewe toka Radio One Stereo ni kwamba Naibu Waziri wa Nishati na Madini Ally Malima, ameibiwa kila kitu katika hoteli moja huko Morogoro.
Taarifa zinasema kuwa hata nguo alizovaa sasa amekirimiwa na Wasamaria. Habari hizi zimethibitishwa na Meneja wa Hoteli hiyo Eustace Mutua, ambaye ni Mkenya.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa WanaUsalama wa Morogoro wako, ikiwa ni pamoja na Afisa Upelelezi wa mkoa wameonekana wakitoka na kuingia katika Hoteli aliyofikia Naibu Waziri huyo, huku Ally Malima mwenyewe akiwa hajatokeza nje ya hoteli hiyo tokea alipoingia, na tokea mkasa huo ulipompata.

Naamini tutapata maendeleo zaidi ya tukio hili kwa jinsi muda unavyosogea, na huenda kukawa na menbers kwenye eneo la tukio.

Source: Breaking News saa 7 mchana Redio One Stereo!
 
Adam Malima ni yule anayeongea na kithembe? Anayesemaga kuwa JD yake haina mahali inazungumzia swala la kujiuzulu?

Kama ni huyo, nashindwa kuona huruma
 
Sijui atajiteteaje kwa mkewe akirudi nyumbani kwake. ....anadai kaibiwa, kwani kuna mlango au dirisha la chumba alicholala lililovunjwa?! Hajaibiwa huyo, ni kiburudisho kimeamua kujilipa gharama tu...anyooshe maelezo, utaibiwaje hadi nguo za ndani ulizovaa??
 
Habari zilizopatikana sasa hivi zinasema Naibu Waziri Adamu Malima ameibiwa kila kitu ktk hoteli ya Loshera mjini Morogoro. Hadi sasa bado yuko ndani ya chumba cha hiyo hoteli hajatoka nje. Inasemekana hata nguo alizoavaa amesaidiwa tu na wasamaria wema.

Yaleyale ya mawaziri kuendelea kuumbuka ugenini!

Manjagy bado yanafuatilia issue hii nzima!

Source: Radio One, muda 13:14 pm

Jamaa namuona mjanja wa town kumbe bado hajajua kwamba huwa wanaweka kwenye chakula ya mtoto? Mungu wangu wamekomba kila kitu ili asiweze kutoka nje na nadhani alilala hadi saa za mchana. vichanchide vimeishavuka mpaka tayari huenda vipo Florida 2000 vinasherehekea mafanikio baada ya mawindo yao kunasa! Na kama alikuwa na jiwe ndio amewapa utajiri.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom