Naibu Spika: Lugha ya kejeli na kuudhi kwa mtindo wa mafumbo ruksa bungeni

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Kwa maamuzi ya spika kufuatia muongozo alioomba Mh. Tundu Lissu juu ya kauli ya mwanasheria mkuu wa serikali ni wazi na hii ndio tafsri yake kuwa ameruhusu Lugha ya kuudhi na kejeli kwa mtindo wa mafumbo bungeni.

Kwasababu alisema mwanasheria mkuu wa serikali yuko sahihi na hakumtaka afute kauli yake.

Angalizo langu awe teyari kupokea na kuruhusu kauli hizo kutoka kwa wapinzani kwani majibu kwa kauli kama hizo hayaepukiki tena.

Labda kwa wale ambao hamkupata nafasi ya kuangalia bunge kilichotokea ni kama ifuatavyo

Mwanasheria mkuu wa serikali alitoa kauli bungeni ilionekana kumlenga Mh. Tundu Lissu kwa kusema kuwa kuna watu wanatumia kichwa kufuga nywele na si kufikiri.

Baada ya kauli ile Mh. Tundu Lissu alisimama na kuomba muongozo wa naibu spika kuwa mwanasheria mkuu wa serikali afute kauli yake ila cha ajabu naibu spika alisema mwanasheria mkuu wa serikali yuko sahii.

Narudia tena isiwe mkuki kwa nguruwe ila kwa binadamu mchungu na akuanzae mmalize.

ALUTA CONTINUE
 
Pia Naibu spika hakutakiwa kumsemea Mwanasheria wa serikali.

Anyway, yote hayo yana mwisho, wenzio wanajaribu kutumia uwingi wao kulinda uovu. It will take time for Tanzanians to see the reality. Wachache wanaoona watawaeleza wengine, so kutakuwa na tricle down effect.

Hakuna kitu kizuri kama uelewa unaochukua muda mrefu (uelewa wa taratibu), cuz unenda kujikita kwenye akili na mioyo ya watu na haufutiki tena.

LET'S WAIT AND SEE.
 
Huyu mwanasheria mkuu ndie anayetumia kichwa kufuga nywele maana hana lolote la maana. Kutwa kupindisha sheria na kusimamia upande mmoja . Yuko kichama zaidi na si kiserikali.
 
Leo ijumaa bana ni shangwe mapemaaaaaa mabo ya kuchoma nyama mbuzi BUNGENI...
 

Attachments

  • 353698002.jpg
    353698002.jpg
    90.6 KB · Views: 112
Ni swala la muda tu kabla mambo hayajaenda kombo pale bungeni.
Rubani akizembea utarajie nini kama sio ajali.
 
Huyu mwanasheria mkuu ndie anayetumia kichwa kufuga nywele maana hana lolote la maana. Kutwa kupindisha sheria na kusimamia upande mmoja . Yuko kichama zaidi na si kiserikali.
Uko sahihi mkuu,,kaegemea chama zaidi,lkn ndo mambo ya kuteuliwa there's no place utamtegemea awe tofauti na itikadi ya aliyemteua
 
Huyu mwanasheria mkuu ndie anayetumia kichwa kufuga nywele maana hana lolote la maana. Kutwa kupindisha sheria na kusimamia upande mmoja . Yuko kichama zaidi na si kiserikali.

Niliona kweli Mwanasheria amefuga nywele nyingi ( kichwani), ila mh, if that is the style of rejecting important issues, then I am worried with our destination as a Nation. Niliona kwa macho yangu huo mjadala, so niliumia sana. and I think the Man ( Lissu) aliamua kutoka siyo kwa kukataliwa kutoa hoja, but ile hisia za Oppression, In humiliation, Discrimination, Disregard, na majina mengine unayoweza kuyataja, ya wazi kabisa, Nadhani aliumia sana.
 
Niliona kweli Mwanasheria amefuga nywele nyingi ( kichwani), ila mh, if that is the style of rejecting important issues, the I am worried with our destination as a Nation. Niliona kwa macho yangu huo mjadala, so niliumia sana. and I think the Man ( Lissu) aliamua kutoka siyo kwa kukataliwa kutoa hoja, but ile hisia za Oppression, In humiliation, Discrimination, Disregard, na majina mengine unayoweza kuyataja, ya wazi kabisa, Nadhani aliumia sana.

Mtu yeyote mwenye kupenda haki lazima aumie kwa namna kiti cha spika kinavyotumika.
Hata hivyo,nasema yanayoendelea pale bungeni ni mtaji kwa wapinzani, ila tu wasikatishwe tamaa.Hii ni vita ya ukombozi dhidi ya wakoloni weusi.
 
kanuni , ubabe, kukosa hoja , wingi wa wabunge wakupinga makofi, na kupongeza wake zao na familia zao, ndo bunge letu kama tanuru la kula pesa za wapiga kura wetu na walipa kodi.Kimsingi ndugai, madam spika,na mapumba, wako kutetea serikali.watanzania wanawaona, hoja ya vifo vya watanzania wasio na makosa unaosababishwa na uzembe watndaji wabovu halikuwa hoja ya kutetewa na mtu yeyote.ndugai yeye bado usingizini anaona anaposoma vikanuni vyake nafikiri watzania wote ni wajinga.mwache akidodoka kwenye jimbo lake kwa jili ya unazi kama huu anaoonyesha waziwazi , ndo atajua.
 
Yana muda na yataisha soon!sijui watajificha wapi na madhambi yao na uoga wao ,dharau zao,kiburi chao....
 
Ni naibu spika huyu huyu aliyemuita mbunge wa Kawe Mh Halima Mdee 'kituko', na leo tena anaungana na kauli ya mwanasheria mkuu kumtukana mbunge wa Singida. Ni vizuri uongozi wa bunge utambue madhara yatokanayo na tabia zao bungeni kwa jamii ya watanzania. Bunge limekosa ustaarab kabisa kwa sababu kiti cha Spika kinatumika kukashifu wawakilishi wa wananchi. Hivi wakubwa wakizomewa huku mtaani kuna wa kumlaumu?
 
Mbona sijaona cha ajabu alichosema CAG, kuambiwa kazi ya kichwa sio kuotesha nywele, na si kila mwenye nywele ana akili ni tusi?? CDM mnalalamika sana mpaka mnaboa..
 
Kuna wateuliwa wawili ambao binafsi nilishaacha kuwazungumzia hata kama watafanya nini kwa sababu uwezo wao wa kufikiri uko kwenye stage ya ''Menopause'' hawa nai Mwanasheria mkuu na Msajili wa Vyama.
 
Mbona sijaona cha ajabu alichosema CAG, kuambiwa kazi ya kichwa sio kuotesha nywele, na si kila mwenye nywele ana akili ni tusi?? CDM mnalalamika sana mpaka mnaboa..
Unapokuwa na upeo mdogo wa kufikiria na kuchanganua maneno ndo unaweza kuandika kama wewe ulivyo andika hapa hatupo katika ushabiki mambo tunayotakiwa kuyajadili na kuongelea ni utaifa sasa kama tunakuwa na mwanasheria mkuu wa serikali ambaye anatoa maneno kama hayo unategemea taifa linakwenda wapi ndo maana hata Chenge alivyokuwa mwanasheria mkuu madudu yalifanyika na majibu yake unayo na hata aliyefuata alifanya madudu pia na hakudumu.kwa hiyo ndugu usilete ushabiki katika mambo ya muhimu humu JF.
 
Roho mbaya kwa Werema ni y kuzaliwa nayo na haja kulia Tarime ndiyo maana he is behaving like a child we know him well
 
Ndugu wana Jf Kitendo cha mwanasheria mkuu kutoa kauli ya udhalilishaji Bungeni leo kimenisikitisha kwa mara ya kwanza leo nikagundua kuwa nchi yetu ina mwanasheria mkuu Juha, aliyekosa hekima, Adabu na ustaarabu. Haihitaji uwe Profesa kutafsiri maneno haya "Tumepewa vichwa si kwasababu ya kufuga nywele bali kufikiri" na "si kila aliyesoma ana Akili" maneno haya yalitolewa baada ya Mh Tundulisu kutoa hoja ya kuomba Bunge lijadili ajali iliyotokea. Maneno haya machafu ni dhahiri yalimlenga Tundulisu. Nakumbuka kitabu cha Tamthlya nilicho soama miaka iliyo Pita cha "Mfalme Juha". Na kumfananisha Mwanasheria huyu na Juha asiye jua kitu.
 
Analipiza kisasi baada ya Lissu kuwaponda majaji kwamba wanateuliwa kiupendeleo bila kufuata taratibu.
 
Back
Top Bottom