Mimibaba
JF-Expert Member
- Jul 1, 2009
- 4,557
- 1,291
Job Yustino Ndugai, Naibu Spika na Mbunge wa Kongwa.
Ikumbukwe kwamba hizi anazodai ni siri za serikali ni pamoja na;
- Ahoji uadilifu wa baadhi ya watendaji serikalini, kutokana na tabia yao ya kuvujisha siri za Serikali kwa wabunge wa upinzani.
- Awaomba wabunge wa CCM kuisaidia Serikali kupitisha bajeti kwani kutofanya hivyo ni kuwaongezea nguvu wapinzani bungeni.
Hii ina maana kama Job Yustino Ndugai angekuwa na uwezo katika kipindi kilichopita 2005 - 2010, kashfa kama za EPA, Kagoda, Kiwira, Dowans, Meremeta, Rada angewawajibisha waliovujisha hizo anazoita siri za serikali. Halafu bila aibu ni huyu huyu Ndugai aliyeongoza ujumbe wa Wabunge nchini Uingereza eti kwenda kufuatilia aliyoita chenji ya rada huku akidai nchi hii inaheshimika kwa uadilifu na matumizi bora !
- Nyaraka zinaoonesha wizara zikitoa hongo kwa Wabunge wa CCM ili bajeti zao zipite.
- Nyaraka zinazoonesha pesa zikilipwa kwenye akaunti binafsi kununua Shirika la Umma.
- Ushahidi kuonesha Wabunge wa CCM wakipewa hongo ili halmashauri mbali mbali zisiwajibishwe.
- .............................. na kashfa nyingi tu zinazolikumba Taifa kila leo.
Job Yustino Ndugai anadai ni heri kashfa zikafagiliwa chini ya kitanda kuliko Upinzani kupata nguvu kwa kutetea maslahi ya Taifa. Je tumweleweje huyu Naibu Spika na Mbunge wa Kongwa, kwa nini alitaka awe mwakilishi wa watu wa Kongwa ? Job Yustino Ndugai hawaonei hata huruma wananchi wa Kongwa wanavyoendelea kuteseka kwa umaskini na maradhi kwa sababu ya huu mfumo fisadi ?
Hajachaguliwa na watu wa Kongwa hata kwa kura moja. Pesa za sakata Loliondo zilitumika kumpitisha bila kupingwa. Muulize lini ametembelea jimboni hususan wakati wa mafuriko Mtanana na Kibaigwa? Jibu HAKANYAGI hana anaemtambua. Ni majonzi tunayopewa na CCM.