Naibu Spika Job Ndugai amtoa nje Mbunge wa CCM kwa siku tatu

Wadau, mi naomba kujuzwa. Hivi, Halima Mdee kasema nini kustahili maneno ya kuundi jinsi hii? Je, Spika anapotoa maneno ya kuudhi kuna kanuni zinazo tumika kumuadibisha au yeye youko juu ya kanunu? Naomba nijuzwe wadau kuuliza si ujinga!
Wala usijiumize mkuu,
Bunge la Magamba,
Serikali ya Magamba,
Mahakama ya Magamba,
Magamba yote yako juu ya Kanuni/sheria.
 
Sina shaka kabisa ipo siku Ndugai ama atapigwa au kutukanwa live Bungeni.

Ndugai na Wenyeviti wa Bunge wanapwaya mno, wana maneno ya kuudhi kwa Wabunge tuliowachagua.

Ndugai, kama kweli ametoa kauli kuwa Wana Kawe wamechagua kituko ni tusi kwa wananchi na Bunge linapelekwa kusiko kabisa na Naibu Spika na Wenyeviti wa Bunge hasa Mabumba.
 
Ndugai alitaka kujiosha kwa makosa ya nyuma sasa amekosea tena!
 
nyinyiem hawana jipya,wanajikosha kwa wananchi,mwenendo mzima wa uendeshaj wa vikao vya bunge umejaa upendeleo mkubwa,hata kaul za waendeshaji zinatia shaka,huwez kumdhalilisha MP mwenzako kwamba anatafuta umaarufu!hata kwny hoja za msingi tunaweka siasa ndani yake..,.
 
ebaeban. Nilikutegemea wewe uandike vizuri hiyo habari ya ndugu yako Ndugai na mambo yako kumtetea. Mtu anaharibu upepo bungeni, anafoka ovyo na kuunga statment kama WENYE UCHUNGU WAENDE WAKAZAE je hizo ni kauli za mtu wa hadhi kama yake?
 
Last edited by a moderator:
Baada ya kushindwa kutoa uthibitisho kuhusu serikali kuhonga madiwani wa Kigamboni! Wakati naibu spika akitoa hukumu ndipo Halima Mdee (waziri kivuli wa ardhi) akataka kutoa taarifa, Job Ndugai akamzuia kisheria! Ndipo akawaambia wana Kawe kuwa wamechagua kituko! Eti anataka amtoe nje apate umaarufu na aandikwe kwenye magazeti!
My take: Job Ndugai hongera kwa kuua CCM! Janga la taifa

Lakini Haujasema kwanini Dr. Ndugulile kwanini ametolewa Nje???
 
Na nyie wana JF wengine mpimwe akili kwa kuandika habari hazina nyama, utafikiri siyo great thnkers, napata usumbufu sana kusoma thread hizi ambazo zinamwacha msomaji in suspence, sisi huku kwetu SOLYA karibu na Manyoni hatuoni TV live mpaka jioni Taarifa ya habari tunawasha generetor
Tatizo watu wanakimbilia kupost utadhani wanalipwa na utafikiri wote tuko kwenye hilo tukio
 
Hivi huwa mna haraka gani? sasa angalia hata kiswahili ulichoandika hakieleweki, rudia tena Ndungulile katolewa inje kwa sababu gani? Tumia kiswahili fasaha.

welu=waluwalu=wehu. Angalia user ID yake utajua kwanini kakosea.
 
Ni Faustine Ndugulie mbunge wa Kigamboni. Tulizoea kuona wa CHADEMA tu lakini leo tunamuona na wa CCM.

Nimewahi kuwalletea thread maana nimekikuta hicho kitendo ignawa mwanzo wake sikuwepo kwenye TV.

Ndugai katumia kanuni 73{3}:{ Endapo Mbunge yeyote atatakiwa kuthibitisha ukweli wa maneno aliyoyasema na hadi kufikia mwisho wa muda aliopewa, amekataa au ameshindwa kutoa uthibitisho huo, Spika anaweza kumsimamisha Mbunge huyo asihudhurie vikao vya Bunge visivyozidi vitano}
Hii ni timing tu walijua wakija kwenye kupitisha mafungu Dr. Ngugulile angewasumbua sana kwa swala la kigamboni ndio maana Ndugai akaanza kutokwa mapovu!!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom