Naibu Mwanasheria Mkuu wa SMT na Waziri Ghasia Live Channel Ten Kuhusu Muswada wa Katiba

Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,941
9,947
Wadau, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bwana Masaju na Waziri wa Utumishi Mh. Hawa Ghasia wako live Channel Ten wakitoa ufafanuzi juu ya Muswada wa Katiba. Ukiwa na wasaa wasikilize
 
Mwanasheria anasema watoto wanahaki ya kujadili mswada. Na Zanzibar kuchoma mswada haisaidii chochote
 
wanalazimisha sana hawa nao............ndio mpango mzima nini? waende zanzibar kwanza wakaweke mambo sawa sio kila saa kwenye ma tv ilihali wanajua kuwa wananchi wanataka nini
 
Mwanasheria anasema watoto wanahaki ya kujadili mswada. Na Zanzibar kuchoma mswada haisaidii chochote
hajui anachoongea huyu, mpaka sasa hivi hii ngoma hawataweza kuicheza , i swear to God , wasipomaliza na kuwaridhisha watu wa Zanzibar hakuna kitu kitakachoeleweka
 
Wamesema tayari muswada umeisha tafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili, na wamekuja nao tayari hapo studio.
 
hajui anachoongea huyu, mpaka sasa hivi hii ngoma hawataweza kuicheza , i swear to God , wasipomaliza na kuwaridhisha watu wa Zanzibar hakuna kitu kitakachoeleweka

mkuu ... mimi siangalii runinga .... kwani werema ni sawasawa na Bileku ya Mpasi au Kabasele ya Mpanya
 
Mwanasheria kasahau kuwa hao watoto hawajausoma muswada na wasingeweza kusoma huo ili wachangie. Wangejali haki yao ya kushiriki wangetafsiri kiswahili. Hapa anaongea bla bla tu-hivi hawaoni wanajichora?.
 
hajui anachoongea huyu, mpaka sasa hivi hii ngoma hawataweza kuicheza , i swear to God , wasipomaliza na kuwaridhisha watu wa Zanzibar hakuna kitu kitakachoeleweka

Mkuu nashangaa wanasema ati Wazanzibar wameshirikishwa ilihali leo mchana nimemsikia Mwanasheria mkuu wa Zanzibar ndani ya Radio Ujerumani akiponda sana Muswada. Hapa kuna kizungumkuti!!
 
CCM wanatakiwa wawe extremely careful wakati wanaongea mambo ya katiba ya Jamhuri kwa upande wa Zanzibar. Wakubwa hawa wanaweza kubeza kitendo cha kuchoma muswada na statements za kuutakataa muswaada huo and that will be a dreaful mistake hasa baada ya kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa. Kwa kifupi ni hivi; Ungujans have something to say about Pembans, and Pembans have something to say about Ungujans, but they both have lot say about Tanganyikans!
 
Mwanasheria kasahau kuwa hao watoto hawajausoma muswada na wasingeweza kusoma huo ili wachangie. Wangejali haki yao ya kushiriki wangetafsiri kiswahili. Hapa anaongea bla bla tu-hivi hawaoni wanajichora?.

Huwezi jua, huenda waliwakusanya watoto wao wanaosoma English Academy ndio wakaenda kukusanyika ili wachangie na wala si watoto wetu wanaoenda shule na fagio pamoja na makopo ya maji huku wakisukumwa kwenye daladala!
 
CCM wanatakiwa wawe extremely careful wakati wanaongea mambo ya katiba ya Jamhuri kwa upande wa Zanzibar. Wakubwa hawa wanaweza kubeza kitendo cha kuchoma muswada na statements za kuutakataa muswaada huo and that will be a dreaful mistake hasa baada ya kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa. Kwa kifupi ni hivi; Ungujans have something to say about Pembans, and Pembans have something to say about Ungujans, but they both have lot say about Tanganyikans!

Wamejiunga ili waitenge Tanganyika!!?
 
Mbona wanachakachua? Wanasoma vifungu tofauti na vile vilivyo kwenye nakala zilizotolewa kwa umma. Eti hakuna katazo la kujadili rais na muungano.

Wanadai kila mara kwamba mswada umepotoshwa lakini hawasemi nini kimepotoshwa. Eti ulikuwa ni mswada wa kuunda tume siyo katiba mpya. Sikumbuki kama kuna mtu aliwahi kusema ni mswada wa katiba mpya!

Wanadai wanafunzi wa UDOM walikuwa wamebeba mawe mifukoni! Walijuaje?

Wanadai tume zote Za awali zimefanya kazi kwa uhuru na haki kwa sababu hakuna mwananchi aliwahi kuzipinga mahakamani
 
Mkuu Werema hayupo amemtuma Naibu wake bwana Masaju

Nime muona huyo Mzee Masaju anajidhalilisha kwa kusema wale (watoto) waliokuwa Karimjee si watoto, na hakuona kabisa watoto pale. Pia amesema, wanasiasa wameupotosha katika kutafsiri muswada. Kwa kweli nimemdharau pamoja na mvi zake-Ni mtu wa hovyo sana!
 
Akiwa kwenye kipindi cha channel ten on monday Hawa Ghasia kasema kuna wanasiasa walifuata wanafunzi na kuwambia wabebe mawe mifukoni
George Masaja naibu mwanasheria mkuu kasau kwamba anatakiwa asiwe partisan kaegemea CCM kuwatuhumu wanasiasa
Hawa ghasia na George wanasema watoto kupelekwa Karimjee ilikuwa na haki yao ya kikaba na hawakufanya fujo yeyote

Mytake hivi hawa CCM wanadhani wananchi hawaoni jinsi walivyorikoroga kwenye mswaada nani watakubaliana na propaganda zao,manake wananchi wanapiga simu wanawaeleza ukweli wanabaki kuuma uma maneno kwa aibu
 
Back
Top Bottom