Naibu Meya Arusha Ajiuzulu

Hivi wanasheria wa Tanzania vipi? Hakuna kifungu kwenye sheria zetu cha kuwashitaki Mkurugenzi, Meya na naibu meya?
 
kimsingi acha wajiuzulu wote,maana tabu tuipatayo utafikiri tunaishi uhamishoni.hivi kweli JK zinamtosha kukubali damu za watu zimwagike kisa madaraka?mh jamani haya tuyaangalie kwa macho yenye umakini vinginevyo tutaumia.
 
Kujiuzuru sawa, lakini mpaka damu za watu zimwagike jamani? hata hivyo ni kitendo cha kiungwana sana kuliko hawa wakina mwema na nahodha ambao wao hawaoni sababu. Kwao la muhimu na maisha ya ccm si maisha ya raia.
 
Habari za kuaminika muda mchache uliopita aliyekuwa Naibu Meya Arusha AMEJIUZULU. More News to follow na tunasubiri "tetesi" Meya mwenyewe atoe kauli ingawaje yeye ni mbuzi wa kafara labda itachuku siku nyingine tatu mpka tano kutoa tamko..

Then I think RPC, IGP to follow before president.....

Mkubwa kama hii habari ni kweli naondoka sasa hivi naelekea maeneo ya kwa Mromboo kwenda kuchoma mbuzi na bia Bariiiiiiiiidi:peace:
 
Meya pia yuko mbioni,ametengwa na kanisa,familia na umma wa wa arusha na tz kwa ujumla,hakuna kingine zaidi ya kujiuzulu,,mapambano daima
 
uwajibikaji huo.. nashangaa kwa nini waliosababisha umwagaji damu bado madarakani
 
Meya ameliambia Mwananchi kuwa hawezi jiuzulu ng'o! Ila kitaeleweka, atafanya kazi na nani? Ametoswa na wananchi na jumuiya kibao za kiraia! Labda atafanya kazi na UWT na UVCCM na taasisi nyingine za kifisadi. Kujiuzuru naibu Meya is a nice move kuelekea ukombozi.

Meya ana husika na vikao vya manispaa tu! Hii habari ya kutompa ushirikiano ni kutokujua sheria za serikali za mitaa!
 
Meya anasubiri Makamba amwambie,Damu ya waliokufa itampalia mpaka na yeye afe,asipoangalia itamgharimu sana yeye nafamilia maana haya mambo huwa sio mazuri hayamsumbui yeye lakini familia lazima hawana amani mioni mwao,yaani yeye angejuuzulu siku ya tukio,lakini CCM lazima watakuwa wamemkalia kooni hakuna kuachia ngazi huku nafsi ikimsuta.

mungu ibariki Tanganyika na ibariki Arusha.
 
Uamuzi wa busara.....bora hofu ya Mungu imemwingia,bado meya!:playball:
 
uyo ni chambo cha mafisadi.

akijiuzulu bila ridhaa yao lazima watamuuwa.

Kungekuwa na waTZ wengi wenye akili kama wwe nchi hii ingekuwa mbali kwa maana ya maendeleo na mafanikio. Watu hapa wanakimbilia kujiuzulu kwa huyu m***a hawajiulizi mwanzoni ilikuwaje akashiriki kwenye huu uchaguzi. Utasikia wanaitisha uchaguzi wa naibu meya.
 
Meya ana husika na vikao vya manispaa tu! Hii habari ya kutompa ushirikiano ni kutokujua sheria za serikali za mitaa!

Meya asipopata ushirikiano hawezi kufanya chochote. Madiwani wa CCM ni chini ya 50%, hawawezi kupitisha matumizi yeyote bila kuungwa mkono na madiwani wa CHADEMA, na ikumbukwe kuwa CCM wamepoteza diwani wao mmoja aliyejiengua CCM na kijiunga na CHADEMA. Kata hiyo inasubiria uchaguzi mdogo ambao CCM, uwezekano mkubwa watapoteza kata hiyo. CCM inajiondoa yenyewe taratibu hata kabla ya 2015.
 
Habari za kuaminika muda mchache uliopita aliyekuwa Naibu Meya Arusha AMEJIUZULU. More News to follow na tunasubiri "tetesi" Meya mwenyewe atoe kauli ingawaje yeye ni mbuzi wa kafara labda itachuku siku nyingine tatu mpka tano kutoa tamko..

Then I think RPC, IGP to follow before president.....

TEHE UNA HAKIKA WeWE AU BLAAAAAAAAAAAAA BLAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA,,MBONA UNASEMA ATATOA TAMKO BAADA YA SIKU TANO AU??
 
Kitaeleweka tu tayari kuna watu wamepoteza maisha kwa ajili yao, hiyo dhambi haiwezi kuondoka mikononi mwao.

Mkuu ona huyu mnywa damu anavyosema!!

Wakati huo huo, Meya anayelalamikiwa Gaudence Lyimo amesema hafikirii kujiuzulu katika nafasi hiyo kwani amechaguliwa kihalali na kwa kufuata taratibu.


"Mimi kwa nini nijiuzulu? Nimechaguliwa na madiwani kwa kufuata sheria na hao waliandamana mimi siwezi kuwazungumzia kuwa waliandamana kwa ajili yangu," alisema Lyimo.

Source Mwananchi, 07 January 2011
 
Back
Top Bottom