Nahodha, Shamuhuna NA SHAHADA ZA MKONONI!!!

OUT ni chuo pekee ambacho kinatoa fursa ktk viwango vya wenzetu, hawa jamaa wana bridging course in case mtu matokeo yake ya sekondari hayampi fursa kujiunga na higher learning Inst, hawa jamaa kila mwanafunzi anapata fursa ya material zote kwa kila kozi na ukiziangalia zile manuals unakubali kuwa hapa they meant education hivyo kuwashutumu waalimu wake ni udhalilishaji. Kwa mwanafunzi makini Open atasoma na atakuwa mwelewa mzuri zaidi ya yule wa Ud na vyuo vingine, jamaa wametoa nafasi kwa wanataaluma kujiajiri kupitia centre maalum dedicated kwa OUT students, hivyo kufauru kwako kutategemea kuifahamu tafsiri ya Open Learning facility na pia malengo yake ktk kile unachosomea. Kama unataka cheti tu Open si mahala pako ila ukisoma vizuri utafauru.

Na sisi wengine tunaitumia fursa hii na imetubidi kupata miongozo toka ktk centres mbalimbali na tunaona mambo yanaenda uzuri.

Nadhani tatizo la wengi ni ile kutaka kujua " Aaah mshikaji ulikuwa pale uki-bookua? Ulikuwa Hall 5/7/? chumba kipi? Kampani yako ilikuwa? vivyo hivyo mzumbe,Sua n.k

Cambridge International College -UK, wao wana ku evaluate mwombaji kwa vigezo vingi mfano
1.Elimu yako ya sekondari na matokeo yake
2.Uzoefu usiopungua miaka miwili ktk field unayotaka kuisomea
3.Certification ya kozi zingine.

Sasa sisi bado tumeng'ang'ania aina moja ya mfumo wa admitting students.

Jamani waungeni mkono OUT ili waendelee kuboresha mazingira ya utoaji taaluma,
 
Given the labour market uncompetitiveness displayed by large numbers of graduates from the Hill, I am frankly flabbergasted by the conceit shown in some of the posts here.

Shavu kubwa FDR.Jr the above post captured everything that came to mind after reading some of the posts in here.
 
ni hivi inabidi tuwe wazi!!!!!ni hivi mi kuna mama yangu mdogo ni naibu waziiri mmoja alikuwa pale ,u know what they use m kumpelekea assignment
pamoja na majibu yake na kuambiwa acopy na kutia saini zake!!!lah ukija swala la mitihani wanadai kwamba wanapelekewa kule lakini mi kuna kiongozi samahani sitoweza kumtaja ilikuwa wakati wa mitihani ananiita ananipa makaratasi ukifungua ndani ni majibu ya mitihani test1&2 na the same ikifika muda wa annual....si wote wanaofanyiwa hivyo ndio maana tunajaribu wkuwaonyesha watanzania viongozi gani tunaowarutubisha
ahsanten
 
Nimefurahishwa na maelezo ya NAHODA lakini cha kuliza hapa kwanini kila mara akitakiwa kueleza elimu yake ameipatia wapi na chuo gani au( UNI)gani alisoma huwa hakupo tayari kutueleza cha kushangaza kwanini afiche shada zake kama anazo nakuombeni kwa wale wenye kumuelewa huyu Nahoda watueleze wapi elimu yake ameipatia na vyeti gani amekuwa navyo

ninavyofahamu nahodha alisoma digrii ya kwanza udsm katika miaka ya 1980s (kati ya 1982 -1987, sina uhakika na muda halisi)
 
kwa mawazo yangu nafikiri tuanze kuthaminisha wasomi wetu kwa mchango wao wa jamii zaidi kuliko vyeti na aina ya chuo alichosoma na inapendeza ikiwa jamii itakuwa ya kwanza kukubali mafanikio yake ndipo ikaangalia mawazo yake.
wengi nadhani mnafahamu tumesoma na watu wengi walikuwa wanapewa mitihani toka zamani na wametoka na vyeti vizuri na bado wameshidwa kutoa mchango wa maana hasa kwa umaskini uliopo na wengine taaluma zao zinagusa jamii moja kwa moja
kwa ni bora tunapo pata bahati ya kusoma tuwe tayari na makini ya nini tumefuata kuliko vyeti
huwa nasikitika sana wasomi wanapo hojiwa hoja za kawaida na watu wakawaida wanaotegemea msaada kutoka kwao wanaposhidwa kuwasaidia
kwa hiyo tubadilike hakuna anayeweza kumkomboa mtazania tena zaidi wasomi kwani wanasiasa wengi wamekuwa wanafki na wachoyo kupitiliza wanaopenda kunyenyekewa na ufalme zaidi
 
Naungana na baadhi ya wachangiaji hapa kuhusu udhaifu wa chuo kikuu huria cha Tanzania, kwa sababu zifuatazo:

1.Wahadhiri wao wengi hawana sifa zinazostahili kuwa wahadhiri wa chuo kikuu. Kama mtakumbuka vizuri, wengi wa wahadhiri wa chuo kikuu huria walikuwa wanafundisha elimu ya sekondari kwa njia ya posta hapo siku za nyuma. Vilevile, nadhani mnakumbuka kuwa chuo kikuu huria kilianzia pale kwenye majengo ya Elimu ya watu wazima, kabla ya kuhamia TIRDO, kisha Biafra. Kwa hiyo, wengi wa wahadhiri wa chuo kikuu huria ni "sub-standard". Msisitizo hapa ni neno wengi, sio wote.

2.Pamoja na udhaifu (1), chuo hakina wahadhiri wa kutosha ukilinganisha na idadi ya wanafunzi waliosajiliwa. Si jambo la kushangaza kuona mhadhiri mmoja anahudumia zaidi ya wanafunzi 200. Matokeo yake ni kwamba wahadhiri wengi pale chuoni wamebuni utaratibu wa "cut and paste" katika kutayarisha assignments, tests and final examinations. Ukiwa mjanja wa kukusanya assignments, tests and final exams za miaka mitatu iliyopita basi ushindi kwako ni tambarare.

3.Kutokana na point namba 2, wanafunzi wengi huwa wanaingia na majibu wakati wa majaribio na mitihani ya kumaliza mwaka. Wanafunzi wanaosomea shahada ya sheria ni vinara katika kuingia na majibu. Kwa ujumla, usimamizi wa mitihani ni dhaifu, huria na holela. Si ajabu kukuta mhadhiri wa Fizikia anasimamia wanafunzi wanaofanya mtihani wa sheria. Kasheshe ni pale wanafunzi wanapofanya mitihani ya "open book".

4. Kwa kuzingatia point 1,2 and 3, haishangazi kuona hawa waheshimiwa, wameweza kujinyakulia hizo shahada zao. wanastahili kabisa kupata hizo shahada. Ningelisikia wamefeli, ningelishangaa kwa mshangao mkubwa!!!
 
Prof.Mbwete, Prof Masenge,+++++++++++ ni waalimu wa sekondari kweli? Big no. of (90) wahadhiri wa OUT ni kutoka UDSM, wasaidizi ni wale waliokuwa Tutorial Asst hapo UDSM na baadhi ya wastaafu wa hapo mlimani.

Narudia tena, aina ya usomaji wa OUT hauwezi kufanana na UDSM kwa sababu nyingi sana, aina ya udahiri wa wanafunzi, mfumo wa digrii zao lakini pia wanafanana sana na Cambridge Inter. College ktk ku groom students wao.
nakupa mfano sasa CIC wanatoa Bachela ktk menejiment/Uchumi/masoko kwa two years lakini wanazingatia nini ktk hilo, ni lazima mfano mtu wa marketing- atatakiwa awe CIC diploma1- Sales Management & Marketing, 2.Global Marketing 3.Advertising &Public Relation, sasa wanakutaka walau uwe umehitimu hizi diploma mbili ili wao waweze ku discount baadhi ya topics ktk degree program yako. Kwa ufupi CIC Degree inapatikana kwa kuzingatia Education and Carrier historical back ground yako, wanachokuongezea ni vile unavyovikosa na automatically umeitia mkononi degree yako. Kwa jinsi wabongo tulivyo wapenda maneno utaona watu wanahoji why 2yrs? wanasahau kuwa hizo diploma hukuziokota msalani na kwamba study, mitihani,mazoezi na time ilitumika mpaka CIC wakakubali kuwa 2yrs is enough for a student.

Out wanaelekea huko na ndiko dunia iliyosonga mbele waliko ila kwa vile mazoea hujenga tabia basi tutang'ang'ania tulipo tu.

KUMBUKENI MUNGAI ALIPOSEMA 2YRS YA DIPLOMA YA ELIMU KWA WALIMU WA SEKONDARI NI SAWA NA MWANAFUNZI ALIYEMALIZA 1ST YEAR YA UNIVERSITY, HIVYO AKIJUNGA NA UNIVERSITY BAADALA YA 3YRS NI TWO YRS , LOOOH IKALETA MANENO SANA NA SIDHANI KAMA IMEANZA KUWA IMPLEMENTED AU LA, IDEA HIYO YA MZEE MUNGAI ILIENDA SAMBAMBA NA KUVIPA NGUVU VYUO VYA KLERUU,MARANGU,KIGURUNYEMBE NA KILE CHA MTWARA KUZALISHA KADA HIYO YA WALIMU BAADALA YA MKWAWA NA CHANG'OMBE AMBAO SASA WANATOA DIGREE YA ELIMU. TANZANIA TUBADILIKE WAKUU, TUSIPONDE KILA FURSA BALI TUZIIMARISHE NA TUHESHIMU MCHANGO WA WALE WANAOJITOLEA KULETA MABADILIKO HAYO MAANA WANADUMU KTK HISTORIA YA NCHI YETU KWA VIZAZI NA VIZAZI.
 
Back
Top Bottom