Nahodha Shadrack Nsajigwa(FUSO)

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,039
2,199
Kwa maoni yangu mchezaji huyu wa yanga na timu ya Taifa anaweza kuwa nahodha bora kabisa kati ya waliowahi kutokea katika soka la Tanzania.
Mwenye wasifu wa mchezaji huyu atuwekee hapa ikiwa ni pamoja na makombe(TROPHIES) aliyowahi kuchukua.
 
Mwenye nao jamani pls.Ninachojua alichezea Prisons na Moro Utd kabla hajajiunga Yanga na majuzi kapata jiko.
 
Kwa maoni yangu mchezaji huyu wa yanga na timu ya Taifa anaweza kuwa nahodha bora kabisa kati ya waliowahi kutokea katika soka la Tanzania.Mwenye wasifu wa mchezaji huyu atuwekee hapa ikiwa ni pamoja na makombe(TROPHIES) aliyowahi kuchukua.
Be right back
 
Kwa maoni yangu mchezaji huyu wa yanga na timu ya Taifa anaweza kuwa nahodha bora kabisa kati ya waliowahi kutokea katika soka la Tanzania.
Mwenye wasifu wa mchezaji huyu atuwekee hapa ikiwa ni pamoja na makombe(TROPHIES) aliyowahi kuchukua.

Umri unamtupa mkono sasa! Nguvu zaidi uwanjani akili kidogo....Siwezi mlinganisha na Ahmad Amasha, David Mwakalebela, Ken Mkapa, Yusuf Bana enzi zao
 
Kama sikosei Nsajigwa Shadrack alizaliwa mwaka 1981,Rungwe Mbeya...

Elimu ya Sekondari alisoma Sangu Secondary Mbeya...

Mpira alianza kucheza tangu akiwa mdogo(chandimu)....

Alianza kuwika zaidi akiwa na timu ya Mount Rungwe ya Tukuyu,Mbeya ambayo ilikuwa ikishiriki ligi daraja la 3 mkoa wa Mbeya enzi hizo...

Aliichezea Mount Rungwe mpaka mwaka 1999 ambapo mwaka huohuo alijiunga na timu ya Kyela United ya Kyela,Mbeya iliyokuwa ikishiriki ligi daraja la 3 ngazi ya mkoa wa Mbeya.....Nakumbuka alihamia Kyela United akiwa na mchezaji aitwaye KAISI ambaye ni rafiki yake na alikuwa na kipaji cha hali ya juu(sijui yuko wapi Kaisi)....Akiwa Mount Rungwe na Kyela United alikuwa akijulikana zaidi kwa jina la Nsaji ama Jigwa...

Baada ya kutoka Kyela United alijiunga na Prisons ya Mbeya ambako hakukaa muda mrefu sana akahamia(yeye na swahiba wake Ivo Mapunda) timu ya Moro United ya Morogoro ambako alikaa msimu mmoja mpaka mwaka 2005 yeye na Ivo walipojiunga rasmi na Yanga na tangu wakati huo(mwaka 2005) hajahama Yanga licha ya misukosuko aliyoipata mara kwa mara akiwa na Yanga......

Kwa uchache naweza kusema huu ndio wasifu/historia ya Nsajigwa Shadrack
 
Umri unamtupa mkono sasa! Nguvu zaidi uwanjani akili kidogo....Siwezi mlinganisha na Ahmad Amasha, David Mwakalebela, Ken Mkapa, Yusuf Bana enzi zao
Masa
Ni nini kilichokuvutia kwa David Mwakalebela na Ken Mkapa, watu wakujiangusha angusha uanjani mwanzo mwisho
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom