Nahitaji ushauri wenu zaidi juu ya hili

TaiJike

JF-Expert Member
Dec 14, 2011
1,483
666
Nyumba ninayoishi ni apartment ya family mbili, nimeishi nyumba hiyo kwa muda mrefu sasa. Mwezi wa kumi 2011 alihamia mpangaji mwenzangu ktk sehemu iliyokuwa imeachwa wazi na mtu ambaye alihama. Jirani huyu ni mwanaume na anaishi hapa bila mke ingawa mke anaye anadai mkewe huyo yuko mbali naye kwa sababu za kifamilia naye hapa yupo kikazi tu.

Toka alivyohamia hapa ninapoishi naye kama jirani kesha badili wasichana wa kazi za ndani wanne aliepo sasa ni wa tano. Msichana wa pili kabla hajaondoka alinifata na kunilalamikia tabia chafu za mbaba huyu za kumlazimsha amtimizie haja zake za zinaa, nikamshauri aondoke akatafute kazi sehemu nyingine. Jana msichana wa tano mwenye umri wa miaka 17 akiwa ana siku mbili tu alinifata na kunitolea malalamiko kama Dada na mwanamke mwenzie, kuwa mbaba yule anamlazimisha mapenzi kwa kumtisha na Bastola. Nilichomshauri binti huyo ni kwamba tutaweka mtego wa kumuadhirisha ili kuikomesha tabia yake chafu ya kuchezea watoto wadogo. Sasa ndugu zangu hapa ndipo ninapoomba msaada wa ushauri wenu nitumie polisi, majirani, ama mapaparazi?
 
nenda polisi au kwa msaada zaidi wasiliana na Gea wa Clouds.
 
Anza na polisi wakiomba rushwa wasiliana na chombo cha habari kinachofikia watu wengi. Au majirani wampe kichapo cha haja. . . . .
 
Dah! Bora kusema kuwasialiana na TNGP au TAWLA
Hainiingii akilini kukimbilia kwa kina Gea habibu

Wakati unamuumbua huyo baba in a way na wewe unahojiwa
Na wewe unaji-expose kwenye media bila ulazima wowote
Ila kama haimsumbui mhusika ni sawa
Lakini ningekuwa katika viatu vyake
siwezi hata kuota kuita akina Gea
Wasiliana na Gea wa cloudz ndio utakuwa mwisho wake.
 
Nakushauri mwite gea kwana aje na mpiga picha pamoja na majiran,coz polic wetu hawaaminiki kwan wanapenda rushwa na huyo muhusika km ana hela wala hiyo ishu haitafika popote hasa hasa utakuona adui na anaweza lipa kisasi,lkn ukimtumia gea itaruka redion watu wengi watasikia wakiwamo mapolic na ikifika kwao itawalazimu kuishuhulikia kwan jamii nzima na vyombo vya habari vitakua vinawafatilia!
 
Hao kina Gea mnaowataja sidhani kama watakuwa na msaada wa haraka ingawa ndo hasa wangefaa kumkomesha kwani mi niko mkoani. Sijajua kwa undani tabia yake kama ni ya visasi ila nachukulia tu mfano wa yeye kutishia bastola kwa vitoto hivyo napata picha yeye yuko vipi na polisi wetu walivyo watumwa wa kuongozwa na nguvu ya pesa nakosa imani nao.
 
  • Thanks
Reactions: bht
sasa akisha 'sutwa' na kina Gea nini kitafuata? staili ya Gea kama itafaa kutumika kama ushahidi, basi sawa...
mimi nadhani cha muhimu ni kuhakikisha muhusika ananaswa kwa ajili ya kupata ushadi wa jinsi anavyomdhalilisha binti ili utumike dhidi yake. Atanaswaje ndio swali la msingi nadhani mleta uzi anataka majibu yake...

Kesi ikiwa na usimamizi na ufuatiliaji wa karibu polisi wanaogopa kuchakachua, hasa ukishirikisha vyombo vya habari au vituo vya msaada wa kisheria.
 
pagumu hapo. Ila polisi inahusika. Na huyo mbaba kweli fataki,ataishije na hg wakati mkewe hayupo?
 
Du kazi kwelikweli, ila wanaume tuna matatizo makubwa sana,mbona wanawake wapo wengi tu uyo dawa yake ni kumtafuti mtego mzuuri wa police pamoja na media ili kumkomesha ,da ilo jamaa bazazi sana linatumia mpaka na bastolla,inaweza ikawa ilo jamaa ni jambazi,embu naomba unipm kama upo Dar lakini iyo kazi naweza ifanya ata mi mwenyewe
 
Back
Top Bottom