Nahitaji sana Busara zako kwa hili.

Zipuwawa

JF-Expert Member
Nov 28, 2010
3,051
653
Wana JF poleni sana na Mihangaiko ya maisha na wale wa Arusha nawapa Pole sana kwa Matatizo yote yaliyowapata hadi kupoteza maisha ya watu basi Mungu azilaze roho za wapenda maendeleo wote waliokufa kwenye harakati.....Amen.

Lengo nikuwaomba ushauri kwenu najua mtanisaidia ili niweze kufanikiwa kwa hili ,sasa nataka kuagana na Ukapera na kuingia katika ndoa kama Mungu atanijalia.
Watu wengi wamekuwa wakisema kuwa ukioa lazima uwe na nyumba ndogo ili siku Mkeo akikuudhi basi uende nyumba ndogo ukajiliwaze, kwa kufanya hivyo basi unaweza kujikuta huwi na mgogoro na ndoa siku zote za maisha yako.Kwani nyumba ndogo inajua sana kufariji hasa pale unapokuwa umegombana na mkeo.

1..Je Ni kweli nikioa basi niwe na Nyumba ndogo?
2..Je Ni aina gani ya Nyumba ndogo niwe nayo? ( Mmama, Msichana mdogo,au shangingi?)
3. Na niwezaje kuficha mke wangu asijue?

Nisionekane natania kwa hili maana wapo wengi wameoa na wana nyumba ndogo kama una utaalamu wa kumiliki nyumba ndogo toa ushauri hapa na kama ni vibaya kuwa na nyumba ndogo pia nipe sababu.

Nawasilisha kwenu.........
 
kwa mtaji huu wala usioe,kwa nini mnapenda kuwaumiza wenzenu jamani?
 
Shosti sasa si ndio maana nimeomba ushauri mimi nataka kuoa kwanini unasema kama ni hivyo niache tu?
 
Yaani hata kuoa hujaoa umeshaanza kupanga mikakati ya nyumba ndogo!? Hivi utasikiaje kama ukifahamu mke unayetaka kumuoa naye akiwa anapanga mikakati ya kuwa na mwanaume wa nje ya ndoa na kufanya kila awezalo ili usimshtukie. Kwa maoni yangu ni bora tu uendelee na ukapera.
 
Babu nahitaji Busara zako sasa nishauri niache hili wazo au niendelee nalo? maana ndio maana nimeliweka mezani hapa na nimekutana na Babu Anataka kusema
Yaani hata kuoa hujaoa umeshaanza kupanga mikakati ya nyumba ndogo!? Hivi utasikiaje kama ukifahamu mke unayetaka kumuoa naye akiwa anapanga mikakati ya kuwa na mwanaume wa nje ya ndoa na kufanya kila awezalo ili usimshtukie. Kwa maoni yangu ni bora tu uendelee na ukapera.
 
Shosti sasa si ndio maana nimeomba ushauri mimi nataka kuoa kwanini unasema kama ni hivyo niache tu?

ndugu yangu inaonekana hata hujui ndoa ni nini,ila mpendwa usimuumize mwenzio kiasi hicho,wanawake wengi wanaishi kwenye ndoa ila nyingi zimewaletea matatizo mbalimbali........,samahani nimeshindwa kuendelea.
 
Hata mimi nimekuelewa na kuona huruma sana kwa hicho kitendo kwani kinaonesha si kizuri ndio maana umeshindwa hata kuendelea ila napaswa kuambiwa ukweli hasara zake mimi ni muaminifu sana ila watu wengi husema hayo ndio maana nimeuliza.

nimekulia kwenye nyumba ya namna hii kaka,fanya kuhadithiwa tu na mtu,usiombe
 
we oa baba na ikiwezakana kuwa na small house every coner ila cha msingi uweze kuonyesha mauwezo kwnye makoloni yote.
 
ChweChwe hapa inaonesha nyumba ndogo ni mbaya maana SHOSTI amesema daima hilo jambo si la kukumbana nalo kwani ni bora uwe unasimuliwa tu . Sasa wewe tena kunishauri kuwa niwe nao kila kona hilo tena ni gumu
we oa baba na ikiwezakana kuwa na small house every coner ila cha msingi uweze kuonyesha mauwezo kwnye makoloni yote.
 
Pole sana inaonekana nimekukumbusha machungu .....
yashapowa kaka watu tunaendelea na maisha yetu kama kawaida sasa,zimebaki hadithi tu,ila kama ni wewe acha kaka,au mweleze yoyote yule aache kabisa huu mchezo
 
Inaelekea unataka kuoa ili uwe na nyumba ndogo.
Kama vipi maliza mambo yako kwanza ukioa unatulia.
Utaitesema familia yako.
Ugawe upendo twice,
kipato twice,
muda twice,
sio vizuri kwa kweli.
 
Sitofanya hivyo tena nimekuelewa!

Nashukuru kwa ushauri wako hapa nimejua kuwa nitakuwa najiongezea matatizo tu kumbe. Lengo la kuoa si kuwa na nyumba ndogo ila nimesema kuwa wengi wa watu hudai kuwa nyumba ndogo zinasaidia ndio maana nikaliweka mezani ili nipate ukweli.

Inaelekea unataka kuoa ili uwe na nyumba ndogo.
Kama vipi maliza mambo yako kwanza ukioa unatulia.
Utaitesema familia yako.
Ugawe upendo twice,
kipato twice,
muda twice,
sio vizuri kwa kweli.
 
kwa mtaji huu wala usioe,kwa nini mnapenda kuwaumiza wenzenu jamani?

ndugu yangu inaonekana hata hujui ndoa ni nini,ila mpendwa usimuumize mwenzio kiasi hicho,wanawake wengi wanaishi kwenye ndoa ila nyingi zimewaletea matatizo mbalimbali........,samahani nimeshindwa kuendelea.

nimekulia kwenye nyumba ya namna hii kaka,fanya kuhadithiwa tu na mtu,usiombe

yashapowa kaka watu tunaendelea na maisha yetu kama kawaida sasa,zimebaki hadithi tu,ila kama ni wewe acha kaka,au mweleze yoyote yule aache kabisa huu mchezo

Sitofanya hivyo tena nimekuelewa!

Thats ma girl,hongera kwa kumpa ndugu yetu ushauri mzuri,hapo mimi wala sina cha kuongeza na senksi nimekugongea za kumwaga,maana naona jamaa yetu hapa alikuwa anataka kwenda kurogwa tu huko nyumba ndogo.

The Following User Says Thank You to shosti four times For These Useful Posts:
Paka Mweusi (Today)
 
Kwanini lakini wanaume mnapenda kuumiza mioyo ya wanawake??? Nyumba ndogo ya nini?? Na una mke ndani ukitaka muda wowote unapewa??? Hebu tuwe na huruma na wanawake saa nyingine bwana aakkhhh
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom