Nahitaji neno la wadada wote wa JF kwenye hili... Hata wanaume semeni pia!

Me semegi,ningemkubalia af nahama nchi, fight for ur happiness! Lolest
 
kama ningekuwa Amina.......shemeji halali yangu.....
Preta umenena...........
Waambie wasongeshe tu bana, shemeji kitu gani.... kwani huyo mwanamke alizaliwa tumbo moja na huyo mume mtesaji.
Nakushauri mwambie waoane na ikiwezekana wanishirikishe kwenye michango ya harusi nitawachangia.
 
Last edited by a moderator:
Preta umenena...........
Waambie wasongeshe tu bana, shemeji kitu gani.... kwani huyo mwanamke alizaliwa tumbo moja na huyo mume mtesaji.
Nakushauri mwambie waoane na ikiwezekana wanishirikishe kwenye michango ya harusi nitawachangia.

Si ndio hapo kwani nini bana
 
Ajaribu kufuta hisia kwa shemeji yake, nafikiri zimeambatana na kutaka kulipa fadhila zaidi kuliko mapenzi.
 
so offensive yaani wanaume wakishikwaga utasema wanakatwa vichwa anaweza kukugeuka mpaka ukasema lol is he thou one ,huyu dada ataleta ugomvi weye atulie tena apotelee mbali mume kitu gani bwana hata mende hutaga pasipokumjua mume lol kama hakumjali kwenye dhiki sio rafiki wa kweli mimi mtu akinipiga au kunitesa wakato wa ujauzito kajipa byebye mwenyewe
 
Mtu na kakaake wanaweza kuuana. Aanze maisha yake upya bila mume na shemeji abaki kuwa rafiki.
 
ukisikia mapenzi ni sumu ndio hii ishu,yaani akiwa na huyo shemeji yake ategemee familia zote mbili kuingia ktk mgogoro mkubwa sana,tena kwa taboo zetu za kiafrika huyo amina ataonekana hafai.
 
Cha msingi hapa naona aachane na wote
Kwanza akianza mahusiano na shemeji itaanza kuleta migongano katika familia zao kwa ujumla
Pili kama hana hisia na mmewe kabisa akae atulie inawezekana yupo mungu aliyempangia katika maisha yake
Lakini kuanza mahusiano na shemeji yake aachane na hilo wazo kabisa..
Uzuri wanaume bado wapo hawajaisha duniani kama hamuhitaji mmewe..
*****************shemeji NO***************************
Jamani mbona wakinadada mnajiaminisha sana kwetu!?Mi nadhani kuliko kuendelea kuumia bora amwambie huyo shemeji yake kuwa anampenda!Na shemeji kwa busara zake atamkataa kistaarabu(kwani c lazma dada akikwambia anakupenda ukubali).baada ya hapo dada atatulia.But akikaa kimya asimwambie kitu na shemeji anaendelea kumtembelea nyumbani kwake oneday(watasema shetani katupitia).Pole sana dadangu
 
Mimi nashauri kuhusu huyu mume , yaani asithubutu kurudiana nae, atakaporudiana nae ajue siku akibeba mimba si mme wake tena labda kama anataka mwanaume wa starehe sio wa familia,. mimi ninaushuhuda wangu nilibeba mimba ilivyokuwa tu mwaume akawa hashikiki vituko vya hapa na pale mara anaweza akaja usiku akalala asubuhi anakuambia umeniibia pesa zangu jana nilikuja na kiasi fulani mbona leo naona zimepungua, masikini wewe hujui kama alikuja na hewa wala nini kwanza kaja saa 8 au saa 9 usiku umelala hizo hela umeiba saa ngapi!? mpaka niljifungua vituko vituko vikaendelea nikawaza hivi nilizaliwa nae? mbona niliozaliwa nao niliwaacha sembuse yeye nikaondoka zangu.
 
Awe mbali na huyo shemejie ili kupunguza hisia zake maana maafa yanaweza kutokea kati yao watatu.
 
Kwn kuwa na mwanaume lazima? Take tme and do yo tingz bwn! Wao ndo hawawez bla sisi
 
Ajitahd kurudisha hisia zake wawe pamoja u never knw kashajifunz hawez kumtenda tena
 
Asirudiane na mumewe bali atulize akl atapata wa kumpenda na aachane na shemej yake
 
Haina haja ya kusambaratisha familia ya watu,akae mbali na shemeji mtu na wala asimuoneshe hisia zozote za kumpenda,kingine atalinda maisha yake naya huyo shemeji mtu kwani yeye ni mke wa mtu halali wa ndoa.
 
Namshauri aangalie sheria za dini yake zinasemaje, kama anaweza kuhamisha majeshi na afanye hivyo. Anaekupenda atakujali.
 
Amina hawezi kuolewa na aliekua shemeji yake kabisa, kwa mila na desturi za kiafrika, pia na dini .

Ajizuie kumpenda kimapenzi, amheshimu kama mtu muhimu kwake, aliemfaa wakati wa shida yake TUUUUUU!!!!!!!!!!
 
Aachane na hiyo kitu ya shemeji watauawa bure. Sana sana arudiane na mumewe kama anajisikia kunyanyaswa tena au hata kuambikizwa magonjwa kwani hajui mumewe kazoa nini

Sijakuelewa vyema hapa!!
 
Back
Top Bottom