Nahitaji kufahamu namna ya kuweka link

Naomba pia nifahamu namna ya maelekezo yenye picha (zikiwa zimewekwa kwenye MS Word) kama yalivyowekwa kwenye attachment hapa chini!
 
Attachments

  • Namna%20ya%20Kuweka%20link%20katika%20threads%20na%20Posts[1].doc
    515 KB · Views: 49
Bado nasubiri kujua hizo picha zenye maelekezo ya namna ya kuweka link zinawekwaje kwenye MS Word? Tujulishane wandugu!
 
Mkuu Buchanan,
Kutegemeana na ilikotengenezwa PC yako, kuna mahali katika keyboard yako (assuming unatumia desktop) upande wa kulia juu, pana key imeandikwa "Print Screen" au 'Prt Scrn'. Sasa ukitaka kuchukua picha ya active window katika PC yako unabonyeza 'Alt+Print Screen' kwa pamoja, na ku-paste hiyo hiyo picha katika MS Word kama ilivyooneshwa katika faili nililoweka hapo juu!
Keyboards za laptops huwa zinatofautiana sana ndo sababu sijagusia.
Nadhani wenye ujuzi zaidi watakuelekeza.
 
Keyboards za laptops huwa zinatofautiana sana ndo sababu sijagusia. Nadhani wenye ujuzi zaidi watakuelekeza.

Nashukuru sana ndugu Idimi, nimefuata maelekezo yako na nimeweza kufanikiwa! Ubarikiwe sana and have a great day!
 
unatilisha aibu! hata kuweka link hujui?? janadume zima linataka msaada... looo
 
We Bwabwa, hatuendi hivyo!
Hata mbuyu ulianza kuota kama mchicha!
Si kila mtu ni mjuzi wa mambo haya!
 
Ndg Idimi, kuna burtons ambazo sielewi maana yake, naomba kupatiwa shule ndugu yangu, naomba usinichoke! Ni hizi zifuatazo:
1. Ile ya Print Screen ina maelezo ya ziada, imeandikwa hivi: Prt Sc SysRq, naomba tafsiri na matumizi yake, kama kuna zaidi ya Print Screen.
2. Pause Break: Naomba matumizi na maana yake.
3. Ins Num Lk: Naomba matumizi na maana yake.
4. Scr Lk: Naomba matumizi na maana yake.
Thanks in advance!
 
Ndugu Buchanan, sitakuchoka. Kimsingi, nyingi ya hizo keys zilitumika sana wakati wa Disk Operating Systems (DOS) commands, kabla ya hizi windows OS na Mac OS. Kwa operating systems za sasa, hizi keys hazitumiki sana.

1.Prt Scr - Hii nimeeleza kwamba inatumika pamoja na Alt- kwa ajili ya kuchukua picha ya active window ktk Pc yako.
2. SysRq/Sysreq - Hii ilitumika enzi za DOS commands kwa ajili ya kubadili majukumu mbali mbali ukiwa unafanya kazi zako (task switching). Kwa sasa haina kazi sana kwa mifumo hii mipya.
3. Pause/Break - Key hii hali kadhalika ilitumika katika DOS commands kwa ajili ya kusitisha ama kusimamisha maandishi yanapokuwa yanatembea kutoka juu kwenda chini au kinyume chake (scrolling). Kwa sasa nayo haitumiki sana.
4. Num Lk - (Number Lock) - Hutumika kuzuia namba zilizo kulia kabisa kwa keyboard zisiandikwe. Ikiwa on, taa ya kijani huwaka, na ikiwa off taa huzima. Huwa nayo haitumiki sana kwa sasa.
5. Scr Lk - Scroll Lock - Hii hali kadhalika ilitumika sana enzi za DOS commands kwa ajili ya kushusha ama kupandisha maandishi katika ukurasa ama kupeleka kushoto na kulia, kwa kutumia mishare iliyo kulia kwa keyboard (arrow keys). Kwa sasa huwa haitumiki sana.

Nadhani wenye matumizi nazo watatoa majibu zaidi!
 
huwa napenda kuweka links ila inakuwa tatizo kwangu. inategemea na kompyuta au ni ujuzi tu unatakiwa? kwa mfano unaambiwa bonyeza hapa inakupeleka kwenye site nyingine. ningependa kujua hivyo
Kingi na wengineo:

Niliandaa haya maelezo HAPA yangewasaidia SANA lakini hamkusoma; ni msingi wa mengi ndani ya JF!
 
Ndugu Buchanan, sitakuchoka. Kimsingi, nyingi ya hizo keys zilitumika sana wakati wa Disk Operating Systems (DOS) commands, kabla ya hizi windows OS na Mac OS. Kwa operating systems za sasa, hizi keys hazitumiki sana.

1.Prt Scr - Hii nimeeleza kwamba inatumika pamoja na Alt- kwa ajili ya kuchukua picha ya active window ktk Pc yako.
2. SysRq/Sysreq - Hii ilitumika enzi za DOS commands kwa ajili ya kubadili majukumu mbali mbali ukiwa unafanya kazi zako (task switching). Kwa sasa haina kazi sana kwa mifumo hii mipya.
3. Pause/Break - Key hii hali kadhalika ilitumika katika DOS commands kwa ajili ya kusitisha ama kusimamisha maandishi yanapokuwa yanatembea kutoka juu kwenda chini au kinyume chake (scrolling). Kwa sasa nayo haitumiki sana.
4. Num Lk - (Number Lock) - Hutumika kuzuia namba zilizo kulia kabisa kwa keyboard zisiandikwe. Ikiwa on, taa ya kijani huwaka, na ikiwa off taa huzima. Huwa nayo haitumiki sana kwa sasa.
5. Scr Lk - Scroll Lock - Hii hali kadhalika ilitumika sana enzi za DOS commands kwa ajili ya kushusha ama kupandisha maandishi katika ukurasa ama kupeleka kushoto na kulia, kwa kutumia mishare iliyo kulia kwa keyboard (arrow keys). Kwa sasa huwa haitumiki sana.

Nadhani wenye matumizi nazo watatoa majibu zaidi!

Nashukuru ndugu Idimi, leo nimepata darasa la kutosha! Ubarikiwe!
 
Kingi na wengineo:

Niliandaa haya maelezo HAPA yangewasaidia SANA lakini hamkusoma; ni msingi wa mengi ndani ya JF!

mkuu nakumbuka nilisoma ila nadhani kipindi kile akili ilikuwa bize sana. Tena nakumbuka somo lilikuwa jukwaa la elimu. Niliitafuta sana hiyo thread nikaikosa ndo nikaomba help. I will repeat the instructions thoroughly Nashukuru angalau somo sasa limekubali kiasi
 
unatilisha aibu! hata kuweka link hujui?? janadume zima linataka msaada... looo

Mbona sio yeye pekee yake? hapa tunaofuatilia maelezo hayo ni wengi na tumefaidika. tunahitaji kujua ku-post thread. Kuuliza ni kutaka kujua ni kijua tu sikulizi tena. Endeleeni kumwaga mautalaam yenu na sisi tuna mautalaam yetu mwaweza kuyahitaji
 
Mbona ni wengi tunahitaji maelekezo hayo. Kwanza tayari tumefaidika nayo na tumejua. endeleeni kumwaga mautalaamu yenu
 
Mbona sio yeye pekee yake? hapa tunaofuatilia maelezo hayo ni wengi na tumefaidika. tunahitaji kujua ku-post thread. Kuuliza ni kutaka kujua ni kijua tu sikulizi tena. Endeleeni kumwaga mautalaam yenu na sisi tuna mautalaam yetu mwaweza kuyahitaji

heri yeye kwani anajua kila kitu, hadi kupakuliwa
 
Mkuu Buchanan,
Kutegemeana na ilikotengenezwa PC yako, kuna mahali katika keyboard yako (assuming unatumia desktop) upande wa kulia juu, pana key imeandikwa "Print Screen" au 'Prt Scrn'. Sasa ukitaka kuchukua picha ya active window katika PC yako unabonyeza 'Alt+Print Screen' kwa pamoja, na ku-paste hiyo hiyo picha katika MS Word kama ilivyooneshwa katika faili nililoweka hapo juu!
Keyboards za laptops huwa zinatofautiana sana ndo sababu sijagusia.
Nadhani wenye ujuzi zaidi watakuelekeza.
Kwa simu je Mkuu inakuaje?
 
Back
Top Bottom