Nahitaji eka 5 za shamba nje ya dar na ufukweni

Kitope

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
236
58
Heshima wakuu, ninahitaji kwa mwenye nalo shamba hata kama ni pori lenye ukubwa wa eka tano kama zimepungua pia tuwasiliane tu.. ziwe nje ya dar na pembezoni ama karibu ya ufukwe. natanguliza shukrani zote! bei isiwe ya kifisadi na ningependa kufanya biashara na mwenye shamba na sio madalali.
Ningeomba kwa mwenye nalo ama kumjua mwenye nalo anishtue kwa mtindo wa hapa na ku pm.
shukran.
 
Ipo eka kumi, mbele ya Bunju, ufukweni kabisa tena bonge la beach la mchanga mweupeeee pe (white sands) halafu pembeni kidogo ya kiwanja kuna mto unaingia baharini (msimu wa prawns, unawachota hata kwa khanga), ni pazuri sana kwa kuwekeza kiuhakika.

Bei ni US$ 1.5m (United States Dollars One Million and Five hundred thousand only). Fixed Price.

Hakuna mapatano. Unazo ni PM huna kaa kimyaaa.
 
Ina sound safi hiyo mkuu! lakini wacha nipite tu bei hiyo siiwezi. msemakweli mpenzi wa mungu
 
1. Mie ninalo nje ya dar,lipo baharini kabisa heka 3 nauza mil500

2.Pia nina heka 4 zipo bunju bei USD 1.6m

3.Nina Heka mbili mwongozo baharini bei mil50

Utalopenda niambie.
 
Wewe umejiandaaje,tangaza offer yako?

Hapo umenena ndivyo! nilisahau kuweka changu! Sio lazima kiwe ufukweni kabisa bali ukaribu ni muhimu! ofa yangu inategemea na shamba lilipo ndio maana sijaweka kiwango! umbali wa kutoka kwenye pirika zetu za mjini na kadhalika!!
Ila tu sitoweza kutoa dollar milioni. hiyo ni nje ya uwezo kabisa.
 
wewe kitope mbona hauko sereous? Ulinipm nikakupa cm ukapiga na ukasema upo mwanza ukirudi utakuja kucheki bt ua quite. Nahic wewe haupo sereous bt ngoja 2one mwisho wake.
 
Taja offer yako range yani uwezo wako tu,pia mtafute mama cha ni mdau sana wa hayo maswala,ila viwanja ni very xpensv vya baharini kama unataka cha baharini kipo nusu heka gezaulole nipe mil15 nikuachie.
 
wewe kitope mbona hauko sereous? Ulinipm nikakupa cm ukapiga na ukasema upo mwanza ukirudi utakuja kucheki bt ua quite. Nahic wewe haupo sereous bt ngoja 2one mwisho wake.

Asante mama cha! Kwani mimi nilisema nsharudi? na huko nilikukwambia ntakuja kupo karibu na ufukwe?!?! Tufanye sipo serious na usinisubiri ukapoteza muda wako mama cha. endelea tu na nina imani pia hivyo ndivyo unavyofanya kwani nimeona matangazo. asante na pole kwa usumbufu. Hili halihusiani na huko kwako tafadhali
 
Taja offer yako range yani uwezo wako tu,pia mtafute mama cha ni mdau sana wa hayo maswala,ila viwanja ni very xpensv vya baharini kama unataka cha baharini kipo nusu heka gezaulole nipe mil15 nikuachie.

Mama Cha kanitoa nishai anko King Kong. nilimuahidi ntapiga simu nikifika mjini na mpaka sasa mjini sijafika. mkulima nimekosea hapo kwa kutingwa na shughuli.
 
hahaha@kitope hujui unadeal na mtu wa aina gani. Ila ukweli lazima tuuseme hata kama wewe hutanunua plot haitaoza zaidi itapanda thamani. Ubabaishaji ni noma kama ulevi. Pole kama nimekutoa nishai
 
ipo beach/ocean view area, 6 acres at Changwahela mapinga, asking price 90M

very pottential for hotel and leisure investment
 
king kong11 nina mashamba mengi kiwanja cha kupima 50*50 na shamba hata eka 25. Namiliki kihalali anayetaka anijuze
 
Nina shamba heka 5 zipo misugusugu kongowe ya kibaha, limekaa vizuri 5km kutoka main road(morogoro rd) bei 8mil. Njia inapitika mwaka mzima. Kama upo tayari nijuze.
 
Nina shamba kubwa lipo kijiji cha kidimu wilaya ya kibaha mkoa wa Pwani. Tangaza ofa yako nikakukatie hekari unazohitaji, lina hekari 100. Barabara inayotoka kibaha mjini imekatiza pembeni ya hilo shamba.
 
hahaha@kitope hujui unadeal na mtu wa aina gani. Ila ukweli lazima tuuseme hata kama wewe hutanunua plot haitaoza zaidi itapanda thamani. Ubabaishaji ni noma kama ulevi. Pole kama nimekutoa nishai

Nadhani nshagundua nadili na mtu wa aina gani!! ni kweli shamba haliozi, wacha tu wengine wanunue ama kama ulivyosema lipande thamani. Asante nimeshapoa siku njema.
 
wababaishaji kama wewe mtu asipokujua anaweza ku-invest alot of energy and hope expecting to get positive returns. Am warning my people in this forum to be careful with such kind of people like kitope. He sound like cornman. Watchout because when he cal u he use private number i.e hiden why if you have good intetion?
 
Tangu utoto wangu hata ubuyu gengeni sijawahi kuiba! Leo hii mama cha unaniita conman! nakumbuka nilikwambia nikifika mjini ntakupigia simu na kama utauza kabla sijafika unijulishe kwa pm. na sijaahidi kitu. leo hii sina ruhusa kutangaza kwamba nahitaji sehemu zingine?!?! unaingia kwenye tangazo langu na kuniita majina ambayo hata wazazi, ndugu wala rafiki hawajawi kuniita ama kunifikiria hivyo. wapo wengi humu nimeongea nao na nimefanya nao biashara nyingi tu bila hata kuweka comment za aina yoyote humu. direct pm and phone calls. unaingia kwenye tangazo langu kwa kashfa na kejeli. Mimi ni muungwana siwezi kukufanyia hivyo na sina fikira za kumdhulumu mtu wa aina yoyote ile na nakula kwa jasho langu 100% na ni kitu najivunia sana hata kama sizalishi mamilioni. Sikuzuii kuendelea na haya hata hapa kwenye thread hii. endelea tu na sina la kukuambia ila kutoa shukrani. Ahsante na kila la kheri.
 
Back
Top Bottom