Nahisi nilimegewa

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,216
113,510
Miaka kadhaa iliyopita nilikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na msichana mmoja mrembo sana. Hakuwa mrembo tu bali pia alikuwa na akili zilizoendana na urembo wake. Nilimpenda sana kwani niliona hatimaye nimempata anayeendana na mimi.

Wakati tunakutana nilimkuta akiwa tayari ana mtoto mmoja. Mtoto huyo alikuwa na umri wa miezi tisa. Baba wa mtoto huyo aliachana na huyo msichana wakati akiwa bado mjamzito wa miezi mitano na hata alipozaliwa jamaa hakuwepo na hakuja kumwona mwanae hadi alipofikisha umri wa miaka miwili.

Ndani ya miaka miwili ya uhusiano wetu jamaa akaanza kumshinikiza demu wangu ampeleke mtoto Toronto ili akamwone baba yake. Demu wangu akawa kwenye mazingira magumu kwa sababu tokea amzae huyo mwanae, baba yake alikuwa hajamwona na alikuwa anataka sana mwanae amjue baba yake. Wakati huo huo uhusiano wetu ulikuwa umekolea na mimi fikara za kumvalisha pete zikawa zimeanza kutawala kichwani mwangu.

Kwa takribani mwezi mzima akawa anafikiria ni jinsi gani ataweza kwenda kumpeleka mtoto Toronto bila kuharibu uhusiano wetu. Kumpandisha mtoto ndege na kuwakabidhi watu wa ndege halikuwa wazo zuri kwa sababu mtoto alikuwa bado mdogo sana. Mwishoni kukawa hakuna jinsi zaidi ya yeye mama mtu kumpeleka mtoto kwenda kumwona baba yake.

Siku ya siku ikafika. Mama na mtoto wakapanda ndege kwenda Toronto kumwona baba wa mtoto. Nikaachwa nyuma peke yangu. Toronto walifikia kwa huyo jamaa. Na jamaa alikuwa akiishi kwenye condo ya vyumba viwili. Ufikiaji wao hapo haukunipendeza licha ya demu wangu kuniahidi kuwa atakuwa analala sebuleni huku jamaa akilala chumbani kwake na chumba kile kingine cha pili atalala mtoto.

Walikaa huko kwa wiki mbili. Kila siku akiwa huko alijitahidi kunipigia simu angalau mara moja kuongea na mimi. Ilikuwa wakati mgumu sana kwangu mimi kwani sikumwamini hata kiduchu eti kuwa atakuwa analala sebuleni. Nikamwambia amwambie hivyo mtoto wa chekechea na si mimi kwani ingawa nilizaliwa usiku, sikuzaliwa jana usiku!!

Baada ya kurudi nilimwuliza kama alimegwa na yeye alikataa katakata. Mimi kwa upande wangu sikumwamini hata kidogo na nikamwacha.

Wadau, hivi kweli mnadhani alikuwa ananiambia kweli? Mtu kafikia kwa jamaa halafu kakaa wiki mbili, hivi kweli hawakumegana? Komredi Fidel hebu nipe mawaidha yako...unalionaje hili? Nilimegewa? Mimi nadhani nilimegewa ingawa sina ushahidi wa bunduki inayofuka moshi.
 
Ila si unampenda? Assume lilitokea/hakuna lililotokea (50:50), then move on. Forget about the event. If you want to spend your life with her, start thinking about how to handle that child, that is, either jamaa akae na mwanae au awe anakuja kwenu kumtazama, na kwa kipindi maalumu mtakachokubaliana. Help her to set the rules. But remember, mtoto hana makosa, na msikilize mama anajisikiaje, maana kumpa mtoto huyo baba (ambaye namuaona sio responsible) halafu mama akae na mawazo juu ya mwanaye huko aliko itawasumbua sana.
Cheers.
 
NN hapa maumivu yako ni ya hisia tu. Lakini kwa kuwa mzigo ulikuwa wa jamaa na wewe ukaokoa ngoma nyavuni, ni vyema ungechunguza nini kilichosababisha waachane na je, ni kweli hawakuwa na mapenzi ya dhati kati yao.

Kimwana timamu alieachwa akiwa na ujauzito kamwe hawezi kuthubutu kumkribia mwanaume aliemtelekeza ktk hali hiyo tena akaenda kulala kwake hata ingekua kwa mtutu wa bunduki, hpo hesabu maumivu tupu, hata ungekuwa wewe ungeacha kuumega mzigo uliojileta wenyewe?.

Kama unavyomwona wewe katulia, jamaa nae ndivyo hivyo kwa huyo mzazi mwenzie bana, hapo mzee ushafanyiwa "UBUSHOKE". Angalia usiwe unatunza shamba la mtu uje kutoa chozi siku jamaa atakapokuja kuvuna mpunga wake.
 
Je, sababu ya kuachana kwao ilikuwa ni nini? Ni hatari kuoa mwanamke ambaye tayari ana mtoto/ watoto na baba yao/ zao wako bado hai kwa sababu itakusumbua sana wewe muoaji hasa yanapofika masuala ya watoto ambayo yatawataka wazazi wote wawili wakutane - send off au harusi, wewe utakaa meza gani? Au mama katikati baba mzazi kulia na baba mlishi kushoto?!

Kama huyo dada alirudi bila malalamiko tena kuhusu huyo jamaa wa Toronto elewa kuwa jamaa alimega kwa sana tu! Pia kama wewe huko bongo basi kwa jinsi wadada wengi walivyo atamzimikia sana jamaa kwa kuwa tu Toronto. Na ukute jamaa limeomba radhi na angeangalia jinsi ya kukuacha pabaya.

Nafikiri uliamua kwa busara kumwacha na hukufanya busara kutaka kudumu naye!!

Oa mwanamke ambaye hajazaa.
 
Daah...asante babu. Niliumia sana aisee. Usiku nilikuwa silali nikimpiga picha kichwani njemba iko juu ya kiuno chake. Usiombee ukutwe na hii hali aisee. Maisha utayaona machungu.

Kitakachokuumiza kichwa ni nini wakati jamaa kazaa naye! Kwani hiyo mimba si iliingia baada ya kummega kwa sana tu
 
NN hapa maumivu yako ni ya hisia tu. .
Ni kweli, hii thread awali ilikuwa imeanzishwa na Nyani Ngabu. Sasa niliporudi hapa tena, nikakuta jina lingine, eti imeanzishwa na Brasil. Na wakati mwingine anajiita Julius. Sasa MODs naomba wamdhibiti Mod mwenzao, kama itakuwa watu wanajibadilishia majina hovyo hovyo, wengine tutajikuta tumejiingiza kwenye name calling bila kupenda. Ukitaka kuamini kuwa awali alikuwa ni Nyani Ngabu, angalia hapo juu kwenye post ya Ngoshwe, ambapo alikuwa akimjibu Nyani Ngabu.
 
Daah...asante babu. Niliumia sana aisee. Usiku nilikuwa silali nikimpiga picha kichwani njemba iko juu ya kiuno chake. Usiombee ukutwe na hii hali aisee. Maisha utayaona machungu.

Yap ukitaka kujua utamu wa ngoma basi ingia ucheze.......!
 
Brasil, pole kwa yanayokukuta. ila huwezi kuwa na uhakika sana kama kweli huyo mpenzio alitembea na baba mtoto kwa kipindi hicho cha wiki mbili. Na kama anakuambia hakufanya kabisa anakataa basi itabidi umuamini tu hakuna namna nyingine ya kupata ukweli. next time huyo baba mtoto kama ana shida ya kumuona mwanaye aje huko mnakokaa amuone na wewe ukiwepo.

Huyo mpenzi wako na yeye kisa cha kushukia kwa huyo kaka mwingine ni nini? kwani hoteli zilikuwa zimejaa au vipi? Ndo yale yale FL1 alisema saa zingine wasichana tunajitakia matatizo.
 
Kwanza kwa nini alimpeleka mtoto kumuona baba na si baba kuja kumuona mwanae ?
Ila mambo ya kuibiana mie sisemi neno

Hapo ndiyo kwenye shida mama, Kama tayari walishasauliana hakukuwa na haja ya kumpeleka mtoto.Na wewe ulikosea kumruhusu aende uko hali ukijua kuwa lolote linaweza tokea, Uamuzi ni wako kusuka au kunyoa. Kwamba alimegwa au hakumegwa hilo alithibitishiki, pata msimamo wa mpenzi wako juu ya mahusiano yake na baba ya mtoto, than move on.
 
Back
Top Bottom